View attachment 3089373Ni ngumu kunishawishi kuwa Nyerere alikuwa kiongozi bora ngumu sana.
Mtu aliyetengeneza taifa la misukule kamwe hawezi kuwa kiongozi bora.
Propaganda kubwa imefanyika kumchora Nyerere mtakatifu na genius Taifa halijawahi kupata mtu wa hivyo.
Indoctrination imefanyika toka utotoni Nyerere kuonekana bora kila upande.
Jinsi watanzania tulivyo ni masikitiko akili zimeoza.
Huwezi kuwa bora kama unageuza watu wako misukule ili uwatawale vyema.
Kizazi cha vijana waoga na machawa wote hakikuwepo wakati wa Mwalimu Nyerere .
Kizazi cha mwalimu kimeishia kwa kina Jenerali Ulimwengu.
Kikwete ,Kinana, Padri Kitima ,Askofu Bagonza, Askofu Shoo n.k.,Dr. Mwakyembe n.k . Pombe Magufuli n.k.
Hiki kizazi kingine ni kizazi cha kina , Mwinyi kizazi cha kupenda fedha ,Mkapa kizazi cha 10%, Kikwete Kizazi cha mafisadi , JPM kizazi cha ubabe, Samia kizazi cha kila mtu kula kwa urefu wa Kamba yake .
Wanasiasa Waliotengeneza vijana waliopo leo ni akina :- Mbowe, Maalim Seif,Lipumba , Slaa , Zito Kabwe, Akina Msigwa ,Sugu, Mnyika , Tundu Lisu, Lema , Makonda ,Magufuli , Kikwete Chalamila , Sabaya , Tulia Aksoni n.k. Hawa ndio Kioo cha siasa za kizazi hiki kilichojaa usanii na woga kila sehemu. Kwa hiyo kila mtoto au kijana mdogo alimuita mwanasiasa aliyempenda na wengine hawakupenda siasa wakapenda miziki ,mpira , ushoga ,usagaji ,kujipendekeza pendekeza n.k alimradi apate chakula .
Lakini Pia Tanganyika ilikua na maadili yake na miiiko yake na mila yake .
Tanganyika dira yake ni ya Kijamaa kutokana na uwepo wa dini tofauti tofauti na makabila tofauti huku pakiwa na rasilimali kila mkoa jambo ambalo lingeweza kujenga ubaguzi mkubwa sana. Zanzibar inamfumo wa Kisultani na kifalme unaopelekea wetu wachache au mmoja kumiliki RASILIMALI ZOTE NA WENGINE KUWA KAMA Watoto wake tu wa kupewa kila kitu.Mfumo wa Zanzibar ni mfumo unaofanana na mifumo ya nchi za kiarabu.
Sasa tumekosa dira kutokana na kuwa na nchi mbili zenye Muungano wa kinafiki zaidi kwani moja haikua inataka kupoteza nchi yake ili kujenga dira moja. Kutokana na ukweli kuwa waasisi wake walilenga siasa na usalama wa nchi kwa wakati huo dhidi ya wakoloni waliokua wanaipenda sana Tanganyika na pia Zanzibar kutokana na rasilimali nyingi zilizopo zinazoifanya Tanganyika kuwa kama shamba la bibi la kuchota tu.
Nyerere alijenga vijana wa waliokua na Elimu kiasi lakini wenye uwezo mkubwa sana na wazalendo sana.
Tulianza kupotea kama taifa kisiasa ,kijamii na kiutamaduni baada ya Mwinyi kuruhusu kila kitu kifanyike bila utaratibu kutokana na woga wa kupinduliwa maana Hata Polisi na jeshi yalikua na maisha magumu. Ujambazi ulikua mkubwa sana . Mpaka Treni walikua wanaweka magogo ili ipinduke na watu waibe mali za abiria. Mabasi yalikua yanatekwa mita chache kutoka kituo cha polisi na watu wenye silaha za Kivita na waliovaa sare zinazofanana na za majeshi mengine huko kwenye nchi zinazofanana na za kwetu. Magendo yalikua yanapita kila boda bila ushuru ,viwanda vya ndani vikafa. Rushwa ikawa kubwa sana ,uhalifu mkubwa sana na hali ikawa ni ngumu sana kwa watumishi wa umma na mabanki kama NBC ikawa ni shamba la bibi la wafanyabiashara kukopa kwa dhamana feki na kutokomea ,watu waliaminishwa kuwa ili uwe tajiri ni lazima udhulumu ,uibe, ufanye biashara za magendo ,ukwepe kodi.
Kwenye Jeshi la Kule Burundi kuna kambi zilikua ni kiwanda cha kutengeneza Pombe haramu ya Gongo maana wanajeshi wa Burundi walikua na maisha magumu sana na mishahara wakati mwingine walikua wanakopa kwa mfanyabiashara wa ngano na sembe n. k. Polisi wa Burundi na wanajeshi walikua na uhasama mkubwa sana kutokana na kuwa kamba za polisi kula zilikua ndefu sana mpaka kwa wauza gongo ambao walikua kwenye Makambi ya jeshi kule Bujumbura .
Hali hiyo ya Kikolombia iliibua matajiri wengi wenye asili ya Kiasia na wachache watanganyika walioamua kuwa mabeduli,majambazi , waporaji ,wakwepa kodi n.k . Wakaibuka wanaharakati wa kidini na maandamano ya kidini kudai haki za dini fulani fulani ikiwemo kuibuka kwa madhehebu yenye imani kali za kilokole na Pia upande wa kiislam kudai kujiunga na OIC ,wengine kudai haki ya elimu eti walidhulumiwa kusoma , wakaanza kudai kuvaa nguo zinazoashiria imani za kidini kwa lengo la kujuana .Misaada ikawa inakuja kinyemela kufadhili shughuli za kidini kama Kareti kwenye nyumba za ibada. Chuki za kidini zikaanza chini chini . Kama kawaida ya siasa za nchi za Kiafrika Lawama zikaangushiwa Rais aliyetangulia baada ya aliyepo kukosa mikakati mipya ya kulinda uchumi imara ,kulinda kuporomoka kwa thamani ya pesa ,kudhibiti mfumuko wa bei . Pakaanza kuibuka nyaraka za kanisa , huku zikiibiwa na wanaharakati wa dini zingine kuitetea serikali kwa maslahi ya wanasiasa wanaowafaddhili na au kuwatafutia wafadhili toka nje . Hapo ndipo paliipoibuka kitu kinachodaiwa kuwa Tanzania inaendeshwa kwa mfumo Kristo hivyo waislam wakandamizaji . Matatizo ya wananchi hayakuwa yanashughulikiwa tena kitaifa bali kidini na kwa hisia za kidini. Yaani harufu ya Udini inakua kwa kasi sana . Maandamano ya kudai mfumo wa vyama vingi yakawa yanafukuta vyuo vikuu wakati huo wasomi walikua wa chache wanyeuwezo wa kufikiri wenyewe bila kufikiriwa na hapakua na machawa kwani wote walikua na Kadi ya CCM lakini walikua wanahoji serikali na kuandamana na migomo mpaka kwenye mashule ya sekondari.
Pakawa na Mihadhara ya kukashifu dini nyingine . Watanganyika wakaletewa utamaduni wa Kubaguana kutokana na dini. Mfumo wa vyama vingi ukaanzishwa wakati ambapo nchi ilikua imeshaparaganyika hasa kidini . Pakaibuka siasa za kudai haki za kidini kwa kusema kuwa serikali inapendelea dini moja huku lawama ikitupiwa kwa Nyerere kwa sababu aliyekuwepo alikua ni wa dini tofauti na ya kwake . Sasa lengo likawa kama vile aliyepo ndiye anabalance dini zote kumbe ni kutokana na hulka aliyoizoea kule Zanzibar kutokana na serikali ya kule kuwa na watu wa dini moja tuu. Sasa walipofika huku wanakutana na watu mchanganyiko matokeo yake wanashangaa mbona kama kila mahali kuna misalaba shingoni . Basi huku inaelekea wa dini nyingine wamezidiwa . Kumbe ni ile hali ya kuchangamana na kule hawakuzoea hali hiyo kabisa . Wakawa wanajaribu kumchanganya mara OIC mara elimu ,mara teuzi zifuate dini mara ,Bucha ,mara ,kitimoto . Seikali ikasema Ruksa kila mtu kufanya anachotaka .
Likaibuka azimio linalofeva hulka za ubinafsi na kuua umoja ,uzalendo,utu na siasa za kuamini kiwa cheo ni dhamana.
Badala yake cheo ni Fursa ya kujilimbikizia mali.
Kweli wakafanikiwa kulimbikiza mali nyingi . Pakaibuka Kundi la wanasiasa matajiri wanaofadhili michakato ya chaguzi ndani ya CCM na hata vyama vingine kama UDP. Hili kundi likawa linatumia fedha wakati wa uchaguzi . Huna pesa hupati uongozi . Madiwani wa CCM wakaiba mali za vyama vya ushirika huko vijiji na kuzigeuza kuwa mali zao binafsi .Uongozi ukawa unanunuliwa kila idara pakawa na biashara kubwa ya kuuza mitihani mashuleni kwenye vyuo na kila mahali. Polisi wachache walioshirikiana na wahalifu wamegeuka kuwa mabilionea . Wale waadilifu wa kizazi cha Nyerere wakawa wanakopa tu kwenye maduka ya watu kwani mabenki hayakuwa na uwezo wa kukopesha wafanyakazi kutokana seikali kuwa mufilisi kabisa na pesa zimehamia kwa mifumo isiyo rasmi ikiwemo watu kutorosha dhahabu na mke wa mkubwa alituhumiwa kufanya hiyo biashara wakati Nyerere hakuruhusu .
Sasa hali hiyo imebadili kabisa dira ya nchi na kupoteza kabisa moyo wa kulitumikia taifa kuanzia kisiasa ,kiuchumi na kiutamaduni
.
Kifupi Nyerere ukurasa wake ulifungwa siku aliyokua anastaafu na kufunguliwa dira na mrengo tofauti kabisa .Hii ni kutokana na Mamlaka makubwa anayokuwa nayo Rais aliyekua madarakani. Kwani anaweza kubadili chochote anachotaka bila kuzuiliwa au kuulizwa na yeyote .
Mfano Rais aliyepo leo ameamua tu kujenga taifa la vijana machawa na wabinafsi wanaowaza mambo yao binafsi tuu ,starehe ,mpira ,mziki na Pombe kiasi kwamba wamekua kama nyumbu mpaka mtu anashushwa kwenye gari na kuuawa wao wanaangalia tu.Kisa hayo hayaruhusu. Watawala wao wameletewa chakula mezani na katiba lakini wanawadanganya watu kuwa Katiba achaneni nayo haiwezi kuwaletea chakula mezani huku wao wakiwa wana magodown ya chakula kutokana na katiba 😆😆😆