Huwezi nishawishi Nyerere alikuwa Rais bora

Halafu ukiona jitu linaamka linawaza Nyerere ndiye sababu ya upumbavu wake basi jitu hilo ni bora lingekuwa ng'ombe tu.

Nyerere hakuikuta nchi hii mikononi mwa bibi yako.Aliikuta mikononi wa wakoloni na yeye akadhani ni vizuri kupigania Uhuru.

Kwa sasa Nyerere hayupo tena miaka mingi sana.Kwa nini usiganie unachoona Nyerere hakukifanya badala yake unalala njaa unaanza kuota Nyerere?

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Ukiweka Unafiki pembeni, lazima utakubaliana na ukweli mchungu sana kwamba Hali ya maisha nyakati za Utawala wa Mkoloni Mwingereza ilikuwa afadhali zaidi kuliko hali ilivyo baada ya Mkoloni kurudi kwao Ulaya.
Ukweli huu mchungu bado unaendelea kuthibitika hadi mpaka hivi sasa, miaka zaidi ya 60 baada ya Mkoloni kuondoka hapa nchini Tanzania.
 
Kwamba sera haisababishi mafanikio au anguko,umevaa chupi mzee!?
Sera yyte inaweza leta mafanikio hasa ikipata watendaji!
Tanzania ni nchi ya 10 africa kwa uchumi!!
Je hizo nchi zilizokua na sera tofaut na ujamaa ziko wap leo??
Uwezo na akili ni muhimu!!
Kenya ilikua ni capitalist country tangu kuanza leo iko wap?? hata GDP ya 200
Na bado kila mwaka iko kwene list ya nchi zenye njaa, umasikini, kusafirisha vibaraka nchi za watu kifupi hata uo uchumi wa kenya ni wa wahindi na foreigners
 
Njia kuu za uchumi china zimeshukwa na serikali?.. serikali ndiyo inayogawa mahitaji muhimu kwa raia bure?.. remember communism is the highest stage of socialism
Jifunze kutoongea kama huna takwimu
 
Attachments

  • 716BF0F9-DAED-4C3D-B518-D3B560E0558F.jpeg
    716BF0F9-DAED-4C3D-B518-D3B560E0558F.jpeg
    171.9 KB · Views: 2
Sera yyte inaweza leta mafanikio hasa ikipata watendaji!
Tanzania ni nchi ya 10 africa kwa uchumi!!
Je hizo nchi zilizokua na sera tofaut na ujamaa ziko wap leo??
Uwezo na akili ni muhimu!!
Kenya ilikua ni capitalist country tangu kuanza leo iko wap?? hata GDP ya 200
Na bado kila mwaka iko kwene list ya nchi zenye njaa, umasikini, kusafirisha vibaraka nchi za watu kifupi hata uo uchumi wa kenya ni wa wahindi na foreigners
Ujamaa uliotopea ulikuwepo USSR,ukafeli, ujamaa ulikuwepo sweden, ukafeli,sisemi ubepari ndiyo sera nzuri,la hasha,mimi ni muumini wa soko huria na si ubepari, china walifuata ujamaa, wakaona haufai,wakaamua kufuata soko huria,wapo pale leo
 
Jifunze kutoongea kama huna takwimu
Communism
Political ideology

Overview
Disadvantages

Communism is an economic ideology that advocates for a classless society in which all property and wealth are communally owned instead of being owned by individuals. Visions of a society that may be considered communist appeared as long ago as the 4th Century BCE.
1726300442321.png

What Is Communism? Definition and History - Investopedia

Wewe unaliona hili huko uchina?​

View attachment 3089373Ni ngumu kunishawishi kuwa Nyerere alikuwa kiongozi bora ngumu sana.

Mtu aliyetengeneza taifa la misukule kamwe hawezi kuwa kiongozi bora.

Propaganda kubwa imefanyika kumchora Nyerere mtakatifu na genius Taifa halijawahi kupata mtu wa hivyo.

Indoctrination imefanyika toka utotoni Nyerere kuonekana bora kila upande.

Jinsi watanzania tulivyo ni masikitiko akili zimeoza.

Huwezi kuwa bora kama unageuza watu wako misukule ili uwatawale vyema.

Kwani ungependa indicators gani ndugu?

Remarks of Welcome at the White House to President Nyerere of Tanganyika | The American Presidency Project

Kwamba hata kuwa huyo ndiye pekee wetu aliyewahi kukata nondo kwenye viunga vya lawns za White house bado hakukuashilii lolote?

Utakuwa kiazi mbatata kweli kweli!
 
Communism
Political ideology

Overview
Disadvantages

Communism is an economic ideology that advocates for a classless society in which all property and wealth are communally owned instead of being owned by individuals. Visions of a society that may be considered communist appeared as long ago as the 4th Century BCE.
View attachment 3095492

What Is Communism? Definition and History - Investopedia

Wewe unaliona hili huko uchina?​

mkuu mi siwezi kubishana na mjinga tafuta wajinga wenzio!!
 
Nyerere alikuwa dictator. Benevolent dictator (dikteta mhisani au mfadhili). Alikuwa na nia njema ya kujenga taifa makini la Tanzania. Hakuwa mbinafsi kwenye matumizi ya rasilimali za nchi; hakuwa mwizi; hakuwa fisadi wala mhujumu uchumi wa taifa.

LAKINI alikuwa mbinafsi sana wa fikra, mawazo na mipango. Hakutaka kabisa mawazo mbadala kuhusu mustakabali wa taifa. Aliamini Tanzania inaweza kuendelea kwa kutekeleza siasa na sera za ujamaa (aina ya ukomunisti) na kujitegemea pekee. Hapo, hakutaka hata kusikiliza mawazo mbadala, hata yale ya kuboresha namna ya utekelezaji wa sera hizo zaidi ya maamuzi yake. Aligombana sana na waliojaribu kupendekeza mawazo mbadala. Hakuamini hao walikuwa na nia njema na Tanzania. Aliamini kuwa walikuwa ama na lengo la wizi/ufisadi au wanatumwa na "mabeberu" kuhujumu uchumi na uhuru wa nchi.

Hivyo, akaamua kuvunja mfumo wa vyama vingi vya siasa, kuunda chama dola (TANU>CCM), na uongozi wa kiimla ambapo, kiuhalisia, Rais anakuwa na madaraka yote ya kidola (imperial presidency). Ni mfumo uliomuwezesha yeye kutekeleza anayotaka bila kuingiliwa na athari zozote asizotaka wakati ule. Kwa jinsi alivyokuwa, ni mfumo uliomfaa sana akaweza kufanya mengi makubwa ya kunufaisha raia japo taratibu, uchumi ulianza kutetereka.

TATIZO kubwa alilotusababishia ni kuondoka madarakani akirithisha mfumo ule kama ulivyo bila kuufanyia mabadiliko ya msingi. Mfumo wa chama dola na imperial presidency ulimfaa yeye kama dikteta mhisani lakini sio wengine waliomfuata. Ni risk kubwa sana kumuachia mtu madaraka ya aina hiyo. Ni binadamu wachache sana wanaweza kuwa kama Nyerere. Alikuwa ni mtu wa aina yake.

Waliorithi huo mfumo walijua una manufaa makubwa sana kwao binafsi na jamaa zao. Hivyo, waliamua kuuendeleza (na naamini) kuulinda kwa damu na jasho maisha yao yote. Ndio maana leo hii ajenda ya katiba mpya itakayopunguza madaraka ya Rais na kuimarisha mihimili na taasisi inapata pingamizi kubwa sana toka kwa watawala. Dana dana zitaendelea hadi mwisho wa dunia.

Bila shaka mfumo huo hauwezi kubadilishwa kwa amani. Yanayoendelea yanaonekana dhahiri. Damu inachuruzika taratibu. Leo nyakati za chaguzi za nchi ni nyakati za maumivu makubwa na misiba. Hiyo ndiyo legacy ya Nyerere ambayo wengi hawataki igusiwe kwa vile aliondoka madarakani na kufariki miaka mingi iliyopita. Njia pekee ya kuirekebisha ni vita ya wenyewe kwa wenyewe. Sijui wangapi wako tayari kwa hilo.
 
Tuseme Nyerere hakuwa bora.

Tuambie wewe Rais aliye bora aliyepita kisha tukuonyeshe hao unaotaka kuwataja jinsi walivyouza rasilimali za taifa letu kwa wageni.

Halafu Ooooh Nyerere hakuwa genius. Umeenda pale Makerere University kufuatilia performance yake ukilinganisha na Marais wengine waliokuongoza waliokuwa wanapata makarai ya kutosha na ku-carry course wakiwa Vyuo Vikuu?

Unajua Nyerere alishatunukiwa Degree za Heshima za Udaktari ila wala hakuwa na mbwembwe za kutaka aitwe Dr.Nyerere kama hao wengine wanaoringia digrii za kutunukiwa?
 
Hao ni almaarufu wapigania uhuru mamboleo kwenye ubora wao:

Tuwatambue wapigania ukombozi mamboleo wasiokuwa na mchango wowote kwa taifa hili
 
Tuseme Nyerere hakuwa bora.

Tuambie wewe Rais aliye bora aliyepita kisha tukuonyeshe hao unaotaka kuwataja jinsi walivyouza rasilimali za taifa letu kwa wageni.

Halafu Ooooh Nyerere hakuwa genius. Umeenda pale Makerere University kufuatilia performance yake ukilinganisha na Marais wengine waliokuongoza waliokuwa wanapata makarai ya kutosha na ku-carry course wakiwa Vyuo Vikuu?

Unajua Nyerere alishatunukiwa Degree za Heshima za Udaktari ila wala hakuwa na mbwembwe za kutaka aitwe Dr.Nyerere kama hao wengine wanaoringia digrii za kutunukiwa?
Hatujawahi kuwa na Rais bora wote wendawazimu waliopewa madaraka makubwa.
 
View attachment 3089373Ni ngumu kunishawishi kuwa Nyerere alikuwa kiongozi bora ngumu sana.

Mtu aliyetengeneza taifa la misukule kamwe hawezi kuwa kiongozi bora.

Propaganda kubwa imefanyika kumchora Nyerere mtakatifu na genius Taifa halijawahi kupata mtu wa hivyo.

Indoctrination imefanyika toka utotoni Nyerere kuonekana bora kila upande.

Jinsi watanzania tulivyo ni masikitiko akili zimeoza.

Huwezi kuwa bora kama unageuza watu wako misukule ili uwatawale vyema.
Katika kipindi cha miaka 19 kuanzia 2005 mpaka mwaka huu hakuna mwaka hata mmoja kwa mujibu wa CAG umekuwa na afadhali katika suala zima la mahesabu ya taasisi zote za kiserikali. Pote anapofika mhasibu mkuu anakutana na wizi na ufisadi wa kila aina.

Enzi za Ludovick Utoh hesabu za serikali zilikuwa chafu.
Enzi za Profesa Assad hesabu za serikli zilikuwa chafu.
Kaja huyu wa sasa bado uchafu ni mwingi kwenye mahesabu ya serikali.

Nyerere kafa 1999, unaweza vipi kumhusisha moja kwa moja na madudu mengi yaliyomo serikalini marehemu asiyeweza kujitetea?.

Nyerere alisomesha watanzania kwa nguvu zake zote, kujitafutia maisha bora ni jukumu letu sisi tuliosomeshwa bure miaka hiyo ya nyuma,

Kumchafua hayati ni ukosefu wa fikra mpya zenye kuweza kujenga nchi, ni kukubali kushindwa wakati mtu akiwa bado anazo nguvu za kufanya kitu chenye kuonekana.
 
Ukiweka Unafiki pembeni, lazima utakubaliana na ukweli mchungu sana kwamba Hali ya maisha nyakati za Utawala wa Mkoloni Mwingereza ilikuwa afadhali zaidi kuliko hali ilivyo baada ya Mkoloni kurudi kwao Ulaya.
Ukweli huu mchungu bado unaendelea kuthibitika hadi mpaka hivi sasa, miaka zaidi ya 60 baada ya Mkoloni kuondoka hapa nchini Tanzania.
Laumu watu milioni 64 wanaoshindwa kujisimamia masuala yao wenyewe. Mwalimu alishatangulia mbele ya haki miaka 25 imepita.
 
View attachment 3089373Ni ngumu kunishawishi kuwa Nyerere alikuwa kiongozi bora ngumu sana.

Mtu aliyetengeneza taifa la misukule kamwe hawezi kuwa kiongozi bora.

Propaganda kubwa imefanyika kumchora Nyerere mtakatifu na genius Taifa halijawahi kupata mtu wa hivyo.

Indoctrination imefanyika toka utotoni Nyerere kuonekana bora kila upande.

Jinsi watanzania tulivyo ni masikitiko akili zimeoza.

Huwezi kuwa bora kama unageuza watu wako misukule ili uwatawale vyema.
Naunga mkono hoja yako 100%

Nyerere alikabidhiwa Tanganyika ikiwa ni nchi ya kwanza katika Afrika kwa kusafirisha mazao ya kilimo.

Kang'atuka kaiwacha nchi masikini wa mwisho duniani. Mpaka chumvi ya unga kuipata kwa foleni, tena uotee tu.
 
Back
Top Bottom