Huwezi nishawishi Nyerere alikuwa Rais bora

Huwezi nishawishi Nyerere alikuwa Rais bora

View attachment 3089373Ni ngumu kunishawishi kuwa Nyerere alikuwa kiongozi bora ngumu sana.

Mtu aliyetengeneza taifa la misukule kamwe hawezi kuwa kiongozi bora.

Propaganda kubwa imefanyika kumchora Nyerere mtakatifu na genius Taifa halijawahi kupata mtu wa hivyo.

Indoctrination imefanyika toka utotoni Nyerere kuonekana bora kila upande.

Jinsi watanzania tulivyo ni masikitiko akili zimeoza.

Huwezi kuwa bora kama unageuza watu wako misukule ili uwatawale vyema.
Ni kweli kabisa kwa sababu hukuwepo Enzi za Utawala wake !!

Lakini ukiona Rais anayetukuzwa na Africa Union mpaka wakaamua kuweka Sanamu yake pale makao makuu Addis Ababa ujue yule alikuwa ni habari nyingine kabisa !!

Mapungufu hayakosekani!
Kwa sababu nobody is perfect 👍
Ila subiri uone kama yupo mwingine atatokea wa kuwekewa sanamu yake pale AU Addis Ababa. 🙏🙏

Kama wale wanautambua Uongozi wake mimi na wewe ni nani wa kutusikiliza tukimponda ???!!!
 
Tatizo ni sisi wenyewe tumejawa na hulka mbovu za ubinafsi, ufisadi kila taasisi.

Nyerere ni aibu hata kumzungumzia wakati huu ripoti ya CAG ikituumbua, ni madudu matupu yanafanyika kila mahali.
Mkuu niseme tu "unaisumbua sana akili yangu." Tuache hayo ya Nyerere, kamwe sioni ni wapi ninapoweza kutofautiana na wewe kufuatana na maneno uliyo andika hapa!
Najuwa kuna sehemu nyingine pia ume yaandika kuwa na maana hii hii!
 
Mtoto mdogo wewe ndio maana huwezi kuelewa kazi aliyoifanya Mwalimu hapa TZ.
Ajabu ni kwamba leo ninakusikiliza/ninakusoma na bado sielewi vizuri!

Hilo tuliachie hapo.

Sasa jaribu kuwaza ni sababu zipi hasa zinazoibua wakati huu kundi la watu lenye fikra zilizo lenga pale pale wanapoona panafaa kuchokonolewa.
Nisome kwa uangalifu, usichukulie majibishano ambayo huwa tunayo kati yetu mara kwa mara yakufunge fikra zako huru.
 
Swala Muungano alikosea vibaya Taifa Bora na tajiri watu million 60 kujiunga na watu Million 2 maskini ni aibu kubwa
nyerere halufeli kwenye muungano kwasababu nyinyi ni mazwazwa ndio maana mnafikiri hivyo!, nyinyi ndo mmeferi kutokana na kishindwa kuelewa Africa kabla ya ukoloni sasa kutakuwa na maana gani kutoa ukoloni bila kuungana kwa Africa yenyewe..?
ila binadamu wengine hamna fikra kabisa nyerere kaunganisha kilichotenganishwa na wakoloni, Nyerere kafanya aliyofanya je wewe zbukuku umelifanyia nini taifa hapo usikute umeshika udini na ukabila zwazwa kabisa yani wewe ni jinga la majinga kichwa sifuri!!!!!!!!!!!!!!
 
una rahisi analalamika akishuka kipaza sauti anahbir umaskini km sifa yeye kuleta maneno km tuo vitani asa km taifa huoni majanga mara urais mgumu acha kalee wajukuu kijijini
 
View attachment 3089373Ni ngumu kunishawishi kuwa Nyerere alikuwa kiongozi bora ngumu sana.

Mtu aliyetengeneza taifa la misukule kamwe hawezi kuwa kiongozi bora.

Propaganda kubwa imefanyika kumchora Nyerere mtakatifu na genius Taifa halijawahi kupata mtu wa hivyo.

Indoctrination imefanyika toka utotoni Nyerere kuonekana bora kila upande.

Jinsi watanzania tulivyo ni masikitiko akili zimeoza.

Huwezi kuwa bora kama unageuza watu wako misukule ili uwatawale vyema.
Kati ya kitu ninachokubaliana na Uzi wako ni Muungano!
Utatutesa,utatusumbua kama mtoto wa kambo kwenye familia.
 
Sidhani kama nitaweza kukubaliana na mtazamo kwamba Julius Nyerere alikuwa Rais bora. Ingawa alikiriwa kama kiongozi mwenye maono, kuna mambo mengi ambayo yanaweza kuangaziwa ili kuelezea jinsi alivyoshindwa katika baadhi ya maeneo muhimu.

Kwanza, ni wazi kwamba Nyerere alipenda kuenziwa. Aliweka msingi wa utawala wake kwa kujenga taswira nzuri ya uongozi, lakini mara nyingi alijitenga na ukweli wa maisha ya wananchi. Katika harakati zake za kuleta umoja, aliweza kuungana na makundi mbalimbali, lakini hatimaye alijikuta akijenga muungano ambao umekuwa na athari mbaya kwa nchi. Muungano huu na Zanzibar, ambao wengi wanauita "muungano wa maskini," umeonekana kama chanzo cha matatizo mengi yanayoikabili Tanzania leo.

Muungano huo ulitokana na wazo la kuleta umoja, lakini katika ukweli, umekuwa na muundo wa unyonyaji.

Serikali ya muungano ilijenga mfumo ambao umewanyima watu wa Tanganyika haki zao za msingi. Tofauti za kisiasa na kiuchumi kati ya Zanzibar na Tanganyika zimekuwa chanzo cha migogoro, na matokeo yake ni kwamba watu wengi wa Tanganyika wanahisi wamesahaulika katika utawala wa muungano.

Hii ni shida kubwa ambayo Nyerere alipaswa kuzingatia zaidi, lakini badala yake alijikita katika kuimarisha mamlaka yake.

Aidha, sera za kiuchumi zilizotekelezwa na Nyerere, kama vile Ujamaa, zilisababisha matatizo makubwa ya kiuchumi. Ingawa alijaribu kujenga jamii yenye usawa, sera hizo zilishindwa kutekelezwa kwa ufanisi.
Mifumo ya kilimo na viwanda vilivyokuwa na lengo la kuleta maendeleo yalishindwa, na matokeo yake ni kwamba wengi walikosa ajira na kipato. Hali hii ilichangia katika kuingizwa kwa nchi katika hali ya umaskini, ambayo bado inashuhudiwa katika maeneo mengi ya Tanzania.

Nyerere pia alikumbana na changamoto za kisiasa. Ingawa alijitahidi kuimarisha umoja wa kitaifa, alishindwa kukubali tofauti za kisiasa na mawazo mbalimbali.

Aliweza kuondoa wapinzani wengi wa kisiasa, na hivyo basi alijenga mfumo wa siasa ya chama kimoja, ambacho hakikutoa nafasi kwa mawazo tofauti. Hii ilileta hali ya kutokuwepo kwa demokrasia na uhuru wa kujieleza, na matokeo yake ni kwamba watu wengi walijikuta wakiishi katika hofu na woga.

Katika mazingira haya, ni vigumu kuweza kusema kwamba Nyerere alikuwa kiongozi bora. Ingawa alijaribu kuleta umoja na maendeleo, njia alizotumia zilikuwa na upungufu mkubwa.

Kila mtu anaweza kuona kwamba kumekuwa na matatizo mengi yanayoambatana na utawala wake, na haya ni mambo ambayo yanahitaji kuangaziwa kwa kina.

Kwa hivyo, ni muhimu kutathmini uongozi wa Nyerere kwa njia ya kiukweli. Ingawa alikumbukwa kwa malengo mazuri, ni muhimu kufahamu kwamba matendo yake hayakuwa na matokeo chanya kwa kila mtu.

Muungano wa Tanzania umekuwa na historia ngumu, na ni wakati wa kuangalia kwa makini jinsi uongozi wa Nyerere ulivyoshiriki katika kuunda hali hii. Ukweli ni kwamba, ingawa Nyerere alikuwa na maono, utekelezaji wake ulikuwa na kasoro nyingi, na matokeo yake ni kwamba watu wengi wa Tanzania wanaendelea kuishi katika hali ngumu.

Kwa hivyo, kusema kwamba Nyerere alikuwa Rais bora ni suala la mtazamo, lakini ni muhimu kuangalia picha pana zaidi. Kiongozi yeyote anapaswa kutathminiwa kwa matendo yake na athari zake kwa wananchi. Katika hali hii, ukweli wa historia unapaswa kuzingatiwa ili kuelewa vyema urithi wa Nyerere na jinsi ulivyoathiri maendeleo ya nchi.

Hivyo basi, ni muhimu kujifunza kutokana na historia ili kuepuka makosa ya zamani, na kuhakikisha kuwa viongozi wa sasa na wa baadaye wanajifunza kutoka kwenye changamoto zilizojitokeza wakati wa utawala wa Nyerere.
 
Alifanya Kwa nafasi Yake kajipumzikia,,Nawe fanya Yako Kwa nafasi yako then jipumzikie acha lawama Kwa Wakhfuu.
 
View attachment 3089373Ni ngumu kunishawishi kuwa Nyerere alikuwa kiongozi bora ngumu sana.

Mtu aliyetengeneza taifa la misukule kamwe hawezi kuwa kiongozi bora.

Propaganda kubwa imefanyika kumchora Nyerere mtakatifu na genius Taifa halijawahi kupata mtu wa hivyo.

Indoctrination imefanyika toka utotoni Nyerere kuonekana bora kila upande.

Jinsi watanzania tulivyo ni masikitiko akili zimeoza.

Huwezi kuwa bora kama unageuza watu wako misukule ili uwatawale vyema.

Hayo maharage uliyokula leo usirudie, YATAKUMALIZA.

Nyerere ndo rais bora mpaka sasa, na alikuwa na maono sana yakulifikisha taifa mbele.

Kipindi cha Nyerere, nchi ilikuwa ina uwezo wa kuzalisha sukari, nguo, na mahitaji mengine vyakutosheleza ndani ya nchi.

Leo na utandawazi wenu mpaka toothbrush, toothpick, matchboxes mnaagiza kutoka China na kwingineko.

Vijana kazi yenu kulalamika tu. Haya kanunue tissue paper ya mchina ujitawaze.
 
Mambo kadhaa yanayoathiri uhalali wa muungano huo:

1. Usawa wa Haki:
Katika muungano, ni muhimu kuhakikisha kuwa kila nchi ina sauti sawa katika maamuzi, bila kujali idadi ya watu.

2. Rasilimali na Uchumi:
Nchi kubwa inaweza kuwa na nguvu zaidi kiuchumi, lakini ni muhimu kuangalia jinsi rasilimali zinavyoshirikiwa ili kuepuka ukandamizaji.

3. Tamaduni na Mifumo ya Kiserikali:
tofauti za kitamaduni na kisiasa zinaweza kuathiri uhusiano.

4. Mkataba wa Muungano:
Muungano unapaswa kuwa na mkataba wa wazi unaokubaliwa na pande zote, ukiweka masharti na wajibu wa kila nchi.

5. Majukumu ya Kiserikali:
Ni muhimu kuweka wazi majukumu ya kila nchi katika muungano ili kuepuka mivutano.

Hivyo, muungano unaweza kuwa na maana, lakini ni lazima uwe na misingi imara ya usawa na ushirikiano.
 
Nyerere Kama binadamu mwingine yoyote yule, alikuwa ana mazuri yake lakini pia alikuwa ana mabaya yake, ingawaje kwa kiasi kikubwa mapungufu yake mengi yalikuwa yanavumilika ukimlinganisha na wenzake wengine wote waliomfutia.


Baadhi ya mabaya au ubovu wa Mwl. Nyerere:-
1. Kuiga, Kuanzisha na kuendeleza Sera na Itikadi Mbaya kabisa ya Siasa za Ukomunisti/Ujamaa hapa Tanzania.

Huu ndio ulikuwa mwanzo wa Kujenga Msingi mbovu wa Taifa la hovyo kabisa lililopo hivi sasa.
Itikadi na Sera ya Ukomunisti/Ujamaa ikaja kushindwa vibaya Sana huku yeye mwenyewe akishuhudia kwa macho yake kushindwa kwa itikadi yake aliyoileta hapa Tanzania kutoka kwa marafiki zake wa China, Urusi na Cuba.

2. Kutengeneza Taifa la Watu waoga, Wanyonge, dhaifu wa fikra wasiojitambua na Wala wasioweza kuhoji. Taifa la watu 'misukule'.

3. Kutengeneza au kuunda nchi isiyokuwa na Mipango-miji, hususani kupitia kwenye Sera yake mbaya kabisa ya ujamaa/Ukomunisti. Sera au Itikadi hiyo ya Ujamaa/Ukomunisti ndio ilikuwa chanzo Cha Kuanzishwa kwa Azimio la Arusha na Operesheni Vijiji, the Worse Operation that completely destroyed the Country and Town Planning process within the Country.
Arusha Declaration and Operation Vijiji also led to the Death of Real Estate Industry and its development.

Kupitia Itikadi hiyo ya Ujamaa/Ukomunisti, Azimio la Arusha na Operesheni Vijiji, Watu wengi sana walinyang'anywa Ardhi zao pamoja na majumba yao waliyokuwa wakimiliki. Nyumba nyingi sana za Watu zilitaifishwa, Leo hii nyumba hizo zinamilikiwa na Shirika la Nyumba (NHC).

4. Kutuletea Katiba ya nchi ambayo ni mbaya kabisa, isiyofaa na ambayo imesababisha na inaendelea kusababisha madhara makubwa sana kwa Raia. Katiba mbaya ambayo imewatengeneza Watawala wa nchi hii kuwa 'Miungu Watu.'
Umeelezea vizuri sana
 
Pamoja na mazuri yake mengi sana kwa Taifa lakini hakuna jambo alichemka kama kueneza sera za kishamba na kinafiki kama ujamaa. Tupo hapa tulipo kwasababu ya sera zake za ujamaa
ni akili ndogo ndio inadhan sera ndo inasababisha umasikini kama yako.
Nadhan huelewi ujamaa ni nini
 
Tunaujua ujamaa wa kisovieti uliopuyanga vibaya sana

Wewe elezea ujamaa ni nini
Ule vitasa vya kutosha
Ujamaa hauko wa aina moja
Ni kama vile watu ambavyo hawauelewi ucommunist lakin ndo huo huo kautumia china kuzipiku nchi zote had kawa wapili kwa marekan kiuchumi
 
Ujamaa hauko wa aina moja
Ni kama vile watu ambavyo hawauelewi ucommunist lakin ndo huo huo kautumia china kuzipiku nchi zote had kawa wapili kwa marekan kiuchumi
China imeendelea kutokana na ku-adopt mchanganyiko wa sera na itikadi katikà Utawala wa nchi hiyo. Watawala wa China walishituka mapema na waliamua kuweka mchanyato au mseto wa itikadi za Ujamaa/Ukomunisti, Upebari, ubeberu, n.k., that's why wameweza kuendelea haraka sana na kuzipita hata baadhi ya nchi za Ulaya ambazo ziliwahi mapema zaidi kuwa na maendeleo makubwa sana.
 
Nani kasema Nyerere genius?
Nyerere alikuwa anahutubia mkutano Jangwani 1959 anasema yeye peke yake Tanganyika ndiye mwenye degree.
Sasa unadhani Watanganyika walipokuwa wanamtafuta rais wangemchagua nani?
Acha uhuni unaweza kutupa hotuba hiyo mwongo mkubwa wewe?
Nyerere hakuwa na tabia za kishamba kujisifia elimu yake na wala hakuwa mwongo. Alijua wapo wasomi wengine aliotofautiana nao mtizamo na itikadi

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom