Mkuu 'Stevo', napita tu na kujikumbusha.
Hayo maneno ndani ya mstari huo najuwa yametukoroga sana wewe na mimi; pamoja na kwamba naelewa unacho kisema hapa.
Kwangu, hayo ni maneno ya kisingizio tu cha rahisi rahisi tunapo tafuta njia za mkato kueleza kushindwa kwa viongozi wetu kuongoza wananchi wake.
Nilisha sema mara kadhaa, katika majibishano yetu humu. Hakuna nchi hata moja duniani isiyo kuwa na watu wenye tabia kama hizi zetu. Ubinafsi, ufisadi, majungu tele, n.k., Tofauti pekee kati ya baadhi ya nchi na nyingine ni uongozi unao amua kuwa na mwelekeo tofauti na tabia hizo mbovu tunazo semekana sisi tunazo.
Wachina ni wezi sana; kama tunavyo wajuwa sasa baada yao kuwa miongoni mwetu. Lakini nenda China uchunguze tabia hiyo ya wizi waliyo nayo na jinsi inavyo zimwa humo nchini mwao. Kuna baaddhi ya nchi ambazo tume aminishwa wao hawana tabia za hovyo hovyo, kutokana na imani zao za kidini. Lakini pamoja na kuwa na imani hizo tabia hizo mbovu zinazimwa kutokana na sheria na adhabu zilizopo zinazotishia hadi uhai wa watu hao wenye tabia mbovu.
Kwa nini sisi hapa tunataka watu wetu wawe kama malaika wakati hakuna juhudi na mikakati ya kuwaondolea ushawishi wa kufanya maovu?
Huo ni mfano mmoja tu wa tabia za kifisadi/wizi/ukwapuzi.
Hali ni hiyo hiyo hata katika kukosa wajibu wa kusimamia shughuli zao za kimaendeleo. Siyo kwamba ni wavivu, la hasha uongozi wetu haujaweka jitihada za kuwafanya waTanzania waweke juhudi zaidi katika ufanisi wa kazi zao, iwe maofisini, au hata kazi binafsi
Hakuna nchi ambayo haikuwa na wavivu, watu wasiopenda kujibidisha zaidi ya kuwa na chakula cha milo michache; lakini uongozi wa nchi unapambana na kuibadili hali hiyo.
Usinielewe vibaya. Sisemi kila mtu ndani ya nchi atakuwa sawa na mwingine, la hasha, lakini kimwelekeo wa jumla, nchi inakuwa na mwelekeo wa kufanya vizuri na siyo hao wavivu, majizi ndio wawe mifano ya kuigwa kama inavyo elekea kuwa kwetu hapa.
Nimekusoma toka mwanzo wa mada hii, na nina hakika kuwa kimsingi tunakubaliana kwa sehemu kubwa. Tatzo letu lilipo sasa nalielewa vizuri zaidi.
Nimekwisha sema leo na jana mara kadhaa kwamba tumemalizana; lakini nashangaa kujikuta nikirudi kuendelea na maongezi haya baina yetu. Lakini kwa vile nina ufahamu mpana kidogo juu yako sasa, nadhani yale maneno ya kichokonozi "upuuzi, mpumbavu, huna akili" yatapumzika sasa!
Lakini naomba usinichokoze tena, kwa kuwadharau waTanzania. Lawama zielekezwe mahali zinapo stahili kuelekezwa; hata kama ni kwa viongozi tunao waheshimu sana wakishindwa kutimiza wajibu wao wa kuongoza.