Mkuu umeandika vingi sana kwa upande wako unaweza kuwa na hoja but kwangu hainiingii akilini,miaka ya nyuma Kanisa Katoliki lilikuwa linapata misaada kutoka nje ila toka 2000s misaada ikakatwa so waamini wenyewe sisi ndiyo tunapaswa kulisimamia,kutoa sadaka hakufilisi kama unatoa kwa akili ulizojaaliwa na Mungu,watu hela tunahonga,tunakula beers michango ya harusi tunachanga vitu vya hovyo kabisa lakini kuiheshimu imani tunashindwa.
Lengo siyo kujisifia,hapo chini nimeenda leo kununua column speakers kwa ajili ya Kanisa lililonilea kijijini kwetu baada ya kuhudhuria ibada mwezi august nikasikia moja ya mipango ya Paroko ni kubadilisha spika zilizokuwepo
(za radio) hazifai zinunuliwe nyengine,nimewiwa tu kushiriki ktk hilo na siyo kwamba nina hela nyingi sana.picha nilizipiga kwa ajili ya kumbukumbu zangu ila bahati mbaya sana nazitumia hapa naweza kuonekana kama najivuna but sivyo lengo langu ni ili watu wajue hata kama imani zao zimelala wapo bado ambao zipo hai.
View attachment 3178197View attachment 3178198