Huwezi Pinga Kuwa Dini (madhehebu yote) yamegeuka kuwa biashara zinangonya waumini. Kama una hoja utasikilizwa na kujibiwa

Huwezi Pinga Kuwa Dini (madhehebu yote) yamegeuka kuwa biashara zinangonya waumini. Kama una hoja utasikilizwa na kujibiwa

Tatizo watu wanaenda kanisani ili waonekane na wanatoa sadaka ili waonekane tu. Biblia inasema sadaka yako hata mkono wa kushoto usijue, cha ajabu zimewekwa bahasha zina majina kabisa yaan anayekuja kuhesabu anajua kabisa fulani leo katoa buku, huyu katoa laki
Duu hapo sasa wameenda mbali na wamefanya hivyo makusudi ili kuwadhibiti,kama wanajua shughuli yako inamaana wanakupimia hapo

Poleni sana jamani
 
Huyo aliyesilimu naona tayar mda mrefu alikuwa na mipango ya kuslim tu na hiyo michango kama imeharakisha huo uamuzi ufanyike mapema

Mtu mwenye imani yake thabiti hawezi hama dini kwasababu ya michango abadani

Mfano mimi leo eti nitoke katika imani ya kumwamini Mungu Mmoja kwasababu ya michango haitotokea abadani
Kabisa haiwezekeni. Mtu kubadiri dini kisa michango halafu mwanaume ni wakutilia shaka kubwa.
 
Ofkoz mkuu
Na sikuhiz wazwaz unambiwa kama ni masikini usiingie
Kanisan ni kwa matajiri
Kuna kanisa nyakumbu geita karibu na kituo Chaafuta Cha bageni kama huna kazi ya kueleweka hurusiwi kabisa kusali mle na kama mkeo mmeo sio wa dhehebu lile basi utashawishiwa Kwa kuambiwa huyo siyo chaguo lako maana hamuamini katika dhehebu Hilo wote.
 
Mkuu Hela yangu Kwasasa sipeleki kanisani Huwa napeleka Kwa wahitaji Moja Kwa Moja ukinunua hata mfuko wa sembe ukampa muhitaji hata kama uupeleke usiku wa manane. Lakini habar zako asubhi zitaenea mtaa mzima na utasemwa vizuri mno. Huko kanisani hata ukitoka m1 utaambiwa Mungu akujazie ulipo toa wanakula Hela Yako kizembe sana.

Acha kabisa kupeleka Hela wape wahitaji mimi ndo kanuni yangu hii inaenda miaka kadhaa Sasa.

Unajua laramu za 70k unagawa shule nzima na kubaki? Na Kwa sadaka hiyo hawatakaa wakusahau hao wadogo zetu popote ukipita watakuambia uliwahi kuja shule ukatupa karamu shule nzima!.
Huwa natoa msikitini aisee maana unaona kabisa kuna Watoto yatima pale unawachangia sio kanisani Askofu anaendeshwa na Nissan V8
 
Welcome to The system.
Kama ulizaliwa ukapewa jina na namba jua utaishi nao Mana wapo katika maumbo tofauti.
FB_IMG_17334822254864579.jpg
 
Nimeshawakomboa watu kama sita wanawake wawili na wanaume wanne, wamenishukuru sana.

Dini na mashehebu ni vyanzo vya kuzalisha hofu na uhasama kwenye jamii.
Mafundishi yao yako hivi

1. Wanakuroga ndio maana huolewi
2. Wanakuroga ndio maana biashara zako zinakufa
3. Wanakuwangia ndio maana unaumwa umwa.
4. Wanakuonea wivu majirani zako ndio maana watoto wamwkuwa wahuni.
5......yaani upuzi mwingi sana. Hata ndugu siku hizi hawakaribishani wala kutembelea kwa hofu ya kurogwa na mikosi
[/QUchOTE] y.
Design ya wachungaji kama hao tambua ya kwamba hamna kitu hapo ,wanapenda kuwatia waumini wao jamba jamba na vitisho kwa vitu ambavyo hata havipo na waumini wao walio wengi ni zile jamiii za watu wa imani za shiriki ambao wamegeuza kanisa kama vilinge na walio wengi, lengo lao wala sio kujiandaa na marejeo ya Yesu mara ya pili ,bali mchungaji ,nabii ,mtume kwao ni kama waganga kanisa ni kama kilinge cha kukutania.
 
Design ya wachungaji kama hao tambua ya kwamba hamna kitu hapo ,wanapenda kuwatia waumini wao jamba jamba na vitisho kwa vitu ambavyo hata havipo na waumini wao walio wengi ni zile jamiii za watu wa imani za shiriki ambao wamegeuza kanisa kama vilinge na walio wengi, lengo lao wala sio kujiandaa na marejeo ya Yesu mara ya pili ,bali mchungaji ,nabii ,mtume kwao ni kama waganga kanisa ni kama kilinge cha kukutania.
Absolutely
 
Lengo la kutoa sadaka kama dini zinavyo fundisha ni lengo nzuri sana sema sasa binadamu zaidi hii ngozi nyeusi imegeuza makusudio mema ambayo Mungu alikusudia katika utoaji kama sehemu ya kujinufaisha wao na matumbo yao .Haingii akilini waumini wajenge shule ila shule ikikamilika watoto wa wachungaji wao wanasoma bure ila katika kanisa kuna kundi la watu ambao hawana uwezo hata kidogo ila hawapo katika mpango wakusoma kwenye hizo shule . Sadaka zingetumika vizuri kama jinsi ambavyo vitabu vya dini vinafundisha ingekuwa ni jambo la kumtukuza Muumba lakini badala yake viongozi wa dini ndio wanataka wawe wanatukuzwa sababu ya kuendesha magari ya kifahari na kuishi katika majumba mazuri.
 
Nipo tiyari kukosolewa lakini Kwa uthibitisho tu na sio mbwembwe zingine.

Kwanza hakuna kwenye biblia sehemu yoyote Ile watu walifanya harambee ya kumnunulia mtume ama nabii punda ama farasi Kwa Wakati huo maana hapakuwa na magari Wala pikipiki.

Hivyo usafiri wao ulikuwa Punda,Ngamia au farasi. Lakini bado sijawahi ona waumini/washiriki wa kipindi hicho wakifanya changizo Ili wanunue japo punda ya nabii/mtume wao.

Kwanini na sema haya? Saivi dini zimegeuka kuwa biashara kubwa sana na wengi wamekuwa wakitoboa ndani ya muda mfupi.

Sababu zake ziko wazi tu.

Hapa nitataja makanisa makubwa mawili tu kama mfano achana na miradi binafisi ya wakina Geodavie, Malisa, Mwamposa, Sunguye nk.

Tangu ni zaliwe na kukulia katika Ukristo bado sijawahi ona eti kanisa limejengwa na mtu mmoja ama hata wao wenyewe makao makuu.

Katika Kijiji chetu tulikuwa tunasalia darasani miaka ya 90 Na badae tukaanza michango tukanunua kiwanja wenyewe bila msaada wa paroko ama katekista baada ya kununua kiwanja tukafyatua matofali ya tope sisi wenyewe.

Hatimaye tukaezeka kwa nyasi. Ukumbuke mafundi ilikuwa Bure kufyatua nk Kila kitu tulifanya juu yetu wenyewe watu wakijitoa Hadi misosi Wakati wa ujenzi wa kanisa Hilo.

Baada ya kukamilisha watu walizidi kuongezeka mara dufu na hatimae tukafanya harambee na kuezeka Kwa bati na kujenga Kwa cement.

Katika kipindi hicho chote tulikuwa tunatoa sadaka na zaka tu michango ilikuwepo kama tu hapo kanisani Kuna muumini anahitaji msaada na tulikuwa tunatoa shilingi kumi ishrini na wenye uwezo watatoa shilingi200 hata 500 kabisa.

Sasa baada ya kuwa wengi na kuwa tumejenga michango ikaanza maradufu sijui ilitokea wapi hasa miaka ya 2006-2009 michango ilikuwa mingi mara imetoka jimboni au parokiani. Hapohapo tunaambiwa kumtegemeza katekista nk.

Ketekista huyu huyu mnaishi nae anakwakwe analima na kufanya Kila kazi lakini Cha ajabu anategemezwa(kuchangiwa)

Hadi Sasa michango imekuwa mingi sana na kutajirisha watu wengine tu.

Hapa ni makanisa yote hata Kwa wasabato mambo ni Yale Yale wanaweza wakaanza wao huita kundi Hilo kundi linakuwa la watu hata7 tu au chini/zaidi ya hapo.

Lakini punde wakiwa wengi tu michango na harambee kuuziwa vitabu vya roho ya unabii lesoni nk ukipiga hesabu unaona wazi kabisa hapa hizi ni biashara.

MFANO Kwa wasabato Kila baada ya miezi3 wanakuwa na lesoni mpya na wananunua na usiponunua Kuna mafungu kadhaa wakadhaa utasomewa ukitishwa kuwa hutakua kiroho utabaki Hivi Hivi miaka nenda Rudi.

Ukija kwenye vyombo vya mziki(choir) mtachangishwa kama kawaida kununua vyombo vya mziki vya kisasa. Yaani Kila kitu kinacho li husu kanisa mtachangishwa.

Lakini ikumbukwe kuwa Zaka na sadaka mnatoa Kila Leo na iwapo ikionekana matoleo yamekuwa kidogo atakuja kiongozi wa juu huko kuja kuhimiza watu wamtolee Mungu matoleo.


Kwa upande wa Roma wao wameenda mbali zaidi usipotoa michango na ikatokea ukapatwa na maswahibu basi tegemea hutapata msaada kutoka kanisani.

Ikumbukwe kule utauziwa Kila aina ya sanamu uitakayo japo sio lazima ila rozali ni muhimu utanunua Kuna kanga za bikira maria na batiki zenye picha ya yesu kabeba kondoo utauziwa. Sijui kanga za Wawata nk

Sasa Hivi tuna barua ya zawadi ya mtoto yesu ambayo tumepangiwa kiasi Cha kutoa Kwa waajiriwa!?

Ikifika kiangazi pia Huwa tunatoa shukuran ya mavuno (matomoro)
Pia Kuna matoleo maalumu Kila Misa hapa hutolewa Kila aina ya mazao inayopatikana maeneo hayo

MFANO wa matoleo hayo ni kama
Ndizi,tikiti mahindi,tambi,Mvinyo kama dompo,asali,mbuzi,kuku,mchele nk

Lakini michango Iko palepale na hawana huruma na maisha Yako.
Ukipata tatizo wewe utaombewa ila wao wakipata shida watahitaji Hela. Tuamke.

Kwa kifupi mambo ni mengi sana ambayo tunayafanya wenyewe tu bila kutegemea msaada wa wazungu (makao makuu) lakini punde tu tukikamilisha Hela zinaenda huko zote.

MFANO mkajichangisha mjenge shule ama hospital (jambo zuri ) Mtachangishana Kwa kushikana mashati Hadi shule/hospital mtamaliza lakini usitegemee eti Kwa sababu mlichangia Kwa kuuza kuku na mbuzi wako Ili ijengwe Ile shule utapata japo discount kidogo tofauti na yule hajachanga kabisa Bali ada utatoa kama kawaida na mtoto wako atarudishwa tu iwapo utachelewa kumlipia ada yake.

Cha ajabu ni kwamba Watoto wa wachungaji watasoma Bure Watoto wa maaskofu watasoma Bure kabisa licha kuwa hawo wachungaji wanalipwa mishahara minono kuwazidi Hadi waalimu.

Hapohapo wanaosomeshewa Watoto wao Bure usafiri wananunuliwa,nyumba anaishi Bure Tena nzuri chakula umeme na maji washiriki wanalipia.

Choo kikijaa kanisa litahusika kutoa Hela ya mzibuaji. Sasa unakaa unajiuliza inakuwaje hii na watu Bado hatuzinduki na kupinga haya mambo. Na hata itokee kanisani labda Kuna mtoto wa masikini asiye jiweza kusomesha na ana akili na hata kanisani ana mahudhurio mazuri namna Gani hawezi soma Bure otherwise washiriki washikane mashati kumchangia la sivyo hata soma abadani.

Nimesikia wasabato Hadi wamepelekana mahakamani Kwa kula rushwa mamilion ya kanisa. Hao wanaitwa watumishi wa Mungu wamemuibia Mungu Hela na suruhisho ni mahakamani Wala sio Kwa Mungu Tena.

Nimezungumzia makanisa mawili haya kama mifano achana na wajasiriamali wa hadharani kama nilivyo wataja hapo juu Hawa wameiga na kuja kiubunifu zaidi.

Ndio maana wanauza maji,vitambaa, mchanga na mafuta ya upako.Hawa wameiga tu.

Ifike mahala Sasa tutoke usingizini tupinge maana niliwahi kusikia mchungaji wa kisabato akisema michango itazidi kurindima Hadi yesu arudi. Kwa maana ya haraka yesu asiporudi mapema kazi tunayo na pona yetu yesu arudi mapema.

Nimeekeza Kwa uchache sana lakini yapo mengi zaidi yanafanyika.

Waafrica Vijana wenzangu wapo tiyari kuunda kwaya wakachangishana na kununua vyombo vya mziki vya mamilio ya shiringi. Lakini hao hao hawawezi kujichangisha walau wawe na kiwanda japo Cha kutengeneza sabuni kamwe hawawezi.

Tupingeni biashara hizi zilizo kuja Kwa mgongo wa dini.


Kwa maelezo haya yote naomba kujuzwa wapi kwenye biblia kumewahi kuwa na mshike mshike kama tulio nao Sasa?

NB: Usilete habari za Anania na safira hapa.View attachment 3178150
Ulichokiandika hapa ni kweli Tupu Makanisani Michango Mingi sana na sadaka Zimekua kibao, yaani Mungu Kila mtu amuombe kwa binafsi yake
 
Back
Top Bottom