Huwezi Pinga Kuwa Dini (madhehebu yote) yamegeuka kuwa biashara zinangonya waumini. Kama una hoja utasikilizwa na kujibiwa

Duu hapo sasa wameenda mbali na wamefanya hivyo makusudi ili kuwadhibiti,kama wanajua shughuli yako inamaana wanakupimia hapo

Poleni sana jamani
 
Kabisa haiwezekeni. Mtu kubadiri dini kisa michango halafu mwanaume ni wakutilia shaka kubwa.
 
Ofkoz mkuu
Na sikuhiz wazwaz unambiwa kama ni masikini usiingie
Kanisan ni kwa matajiri
Kuna kanisa nyakumbu geita karibu na kituo Chaafuta Cha bageni kama huna kazi ya kueleweka hurusiwi kabisa kusali mle na kama mkeo mmeo sio wa dhehebu lile basi utashawishiwa Kwa kuambiwa huyo siyo chaguo lako maana hamuamini katika dhehebu Hilo wote.
 
Huwa natoa msikitini aisee maana unaona kabisa kuna Watoto yatima pale unawachangia sio kanisani Askofu anaendeshwa na Nissan V8
 
Design ya wachungaji kama hao tambua ya kwamba hamna kitu hapo ,wanapenda kuwatia waumini wao jamba jamba na vitisho kwa vitu ambavyo hata havipo na waumini wao walio wengi ni zile jamiii za watu wa imani za shiriki ambao wamegeuza kanisa kama vilinge na walio wengi, lengo lao wala sio kujiandaa na marejeo ya Yesu mara ya pili ,bali mchungaji ,nabii ,mtume kwao ni kama waganga kanisa ni kama kilinge cha kukutania.
 
Absolutely
 
Ukisoma historia ya ukoloni na ukristo, utashangaa sana kama ilikuwaje hata waafrika wakawa wakristo. Udhaifu wa mwanzo wa nchi hizo za Afrika ni huo ukristo wa leo
 
Lengo la kutoa sadaka kama dini zinavyo fundisha ni lengo nzuri sana sema sasa binadamu zaidi hii ngozi nyeusi imegeuza makusudio mema ambayo Mungu alikusudia katika utoaji kama sehemu ya kujinufaisha wao na matumbo yao .Haingii akilini waumini wajenge shule ila shule ikikamilika watoto wa wachungaji wao wanasoma bure ila katika kanisa kuna kundi la watu ambao hawana uwezo hata kidogo ila hawapo katika mpango wakusoma kwenye hizo shule . Sadaka zingetumika vizuri kama jinsi ambavyo vitabu vya dini vinafundisha ingekuwa ni jambo la kumtukuza Muumba lakini badala yake viongozi wa dini ndio wanataka wawe wanatukuzwa sababu ya kuendesha magari ya kifahari na kuishi katika majumba mazuri.
 
Ulichokiandika hapa ni kweli Tupu Makanisani Michango Mingi sana na sadaka Zimekua kibao, yaani Mungu Kila mtu amuombe kwa binafsi yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…