Sijawahi kuelewa akili za wanaoshabikia hizi timu. Wote ni jamii moja wanaofanana uzuzu ila utawakuta kila upande wakiwaponda upande pinzani kwa kukosa akili nk.
Kuna kipindi nilijikuta natamani Yanga iitese sana Simba kimafanikio ili tu mdogo wangu aliyetopea kwenye ushabiki wa kitaahira aumie hadi apunguze ushabiki maandazi akili imrudie afanye mambo ya maana. Dogo alikuwa chuo kikuu lakini ilikuwa kawaida kumsikia alisema "yaani mashabiki ya Yanga hayajitambui kabisa nchi nzima", na haongei kwa utani kamaanisha kabisa. Ukimuuliza ina maana ninyi Simba na Yanga mnakaa sehemu tofauti au kuna lecture maalum mnakula zinazowatofautisha kiuelewa wa mambo? Mbona nyote mna sifa na tabia za kufanana kabisa?" Basi hapo umemchokoza, utabishana naye mpaka keshokutwa.simamo wake ni uleule. Ukimuuliza chochote juu ya mambo muhimu ya nchi hii hata yanayomgusa direct hana chochote cha kusema, yeye ni Simba na Yanga na kubet tu. Bahati nzuri kweli timu yake ikayumba sijui miaka mingapi hawabebi kombe sasa, na chuo kamaliza yupo mtaa vyuma vimekaza, kidogo akaanza kujitambua.