Huyo Mpenzi uliyenaye atakuvumilia katika Matatizo? Mpenzi wa Fei Toto aliolewa wakati wa Sakata la Fei na Yanga

Akizungumza katika 'Intavyuu' maalum na Mwananchi Feisal Salum maarufu Fei Toto amefunguka yafuatayo kuhusu mahusiano yake.

"Lile sakata liliniathiri kwenye mambo mengi sana sio kwa upande wa kucheza pekee, wakati niko kwenye wakati mgumu kama ule kila wakati unafikiria hii kesi itaishaje, nikakutana na pigo lingine la kukimbiwa na mpenzi wangu ambaye niliamini ningekuja kumuoa.

"Aliona kama maisha yangu ya soka tena basi ndio yameishia pale alishindwa kuvumilia na kuamua kutafuta mtu mwingine kitu kilichoniumiza zaidi ni hatua mbaya zaidi kwangu ikawa kwenda kuolewa tena nikiwa katikati ya lile sakata, sikuwa nimemuoa ila tulikuwa na mipango mingi ya maisha kati yetu, hakutaka kuvumilia kabisa nililazimika kuyapokea maamuzi yake hakukuwa na namna na sasa nimerudi uwanjani maisha mengine yataendelea tu."
HAKUMTAFUTA BAADA YA SAKATA KUMALIZIKA

"Hapana hakunitafuta na wala mimi sikumtafuta nilikubaliana na maisha au maamuzi aliyoyachukua na bahati mbaya sana mimi huwa sina hulka ya kuangalia nyuma eneo ambalo nimeondoka nilikubaliana naye maisha lazima yaendelee kwake na kwangu nikipata mwingine nitashukuru Mungu.📌📌📌📌📌📌
 
Asitafute kisingizio cha matatizo yake na Yanga. Huyo binti aligundua mtu aliyekuwa naye ameshikwa akili na masikio, na mama yake! Hivyo aliona hakuna future nzuri mbele yake.

Fei Toto akubali tu maamuzi yake aliyoyachukua kipindi kile yalikuwa ni ya kipuuzi. Na madhara yake yameshaanza kuonekana! Na pia yatamtesa kwa miaka mingi.

Akizungumza katika 'Intavyuu' maalum na Mwananchi Feisal Salum maarufu Fei Toto amefunguka yafuatayo kuhusu mahusiano yake.

"Lile sakata liliniathiri kwenye mambo mengi sana sio kwa upande wa kucheza pekee, wakati niko kwenye wakati mgumu kama ule kila wakati unafikiria hii kesi itaishaje, nikakutana na pigo lingine la kukimbiwa na mpenzi wangu ambaye niliamini ningekuja kumuoa.

"Aliona kama maisha yangu ya soka tena basi ndio yameishia pale alishindwa kuvumilia na kuamua kutafuta mtu mwingine kitu kilichoniumiza zaidi ni hatua mbaya zaidi kwangu ikawa kwenda kuolewa tena nikiwa katikati ya lile sakata, sikuwa nimemuoa ila tulikuwa na mipango mingi ya maisha kati yetu, hakutaka kuvumilia kabisa nililazimika kuyapokea maamuzi yake hakukuwa na namna na sasa nimerudi uwanjani maisha mengine yataendelea tu."

HAKUMTAFUTA BAADA YA SAKATA KUMALIZIKA

"Hapana hakunitafuta na wala mimi sikumtafuta nilikubaliana na maisha au maamuzi aliyoyachukua na bahati mbaya sana mimi huwa sina hulka ya kuangalia nyuma eneo ambalo nimeondoka nilikubaliana naye maisha lazima yaendelee kwake na kwangu nikipata mwingine nitashukuru Mungu.

Chanzo: Mwanachi
Ebu tuseme tu ukweli.

Endapo asingepata matatizo, angekimbiwa na crush wake?
Hakukimbiwa kwa ajili ya nyakati alizopitia kwenye lile sakata, bali lile sakati lilimdhihirisha yeye ni mtu wa aina gani.
Huyo msichana aliishi na Fei vyema sana na huenda aliona alivyoipenda yangu na alivyoupenda mpira.
Lilipoibuka lile swala, ndipo akagundua kumbe alikua anajidanganya, ila kiuhalisia alikua hamjui Fei, wala hakuwa akimjua mama Fei. Hapo bado hajachanganya na maneno ya watu pembeni, maana hadi ushirikina ulihusishwa. Pia Fei alijilalamisha sana kuhusu Hersi mpaka watu tukaanza kuguna, yule Wakala wake ndiyo akaenda mbali zaidi kwamba watu hawajui uchungu anaousikia Fei ni mtoto wa kiume, yeye pia ana mtoto wa kiume hivyo hafurahishwi kabisa na anayopitia Fei na watu wawe makini watoto wao yasije yakawapata. Hii kauli pekee ukiichanganya na na jinsi Fei alivyokuwa akijiliza kuhusu Hersi, zinatosha kabisa kumkimbiza mtoto wa kike, maana hapo tayari bint anaona anaenda kuolewa na mwanamke mwenzake.

Binafsi lilipoanza nilitamani Yanga wamuachia, ila likipoendelea ndipo nikaona kumbe ni mpumbavu kiasi kile?
Dogo angekomaa acheze mpira arudishe kiwango chake, hizi story anazozileta hizi za kutaka kuingelewa kwa huruma, ajiandae huyo aliyekua Mpenzi wake atakapoibuka kujibu mapigo ili kuweka rekodi sawa.
 
Nje ya Mada, Hivi waisilamu mnaruhusiwa kuimba nyimbo kama afanyavyo Diamond na Kiba, na pia kwa mashabiki kufuatilia nyimbo zao? Maana niliona kuna kipindi baadhi ya masheikh walimshikia bango Mzee Yusuf, ila sijaona kwa akina Diamond
Msomi na mwanazuoni wa Kiislamu al-Qaradawi anasema kwamba kuimba na muziki yenyewe ni halali na ya kupendeza. Hata hivyo, anaweka vikwazo kadhaa juu yake. Maudhui ya wimbo huo hayapaswi kuwa kinyume na maadili na mafundisho ya Uislamu au nyimbo zisiambatane na mambo mengine yaliyokatazwa katika Uislamu kama vile pombe namengineyo yasiyo na maadili ya Kiislam.
 
Basi mnatofautiana mahali. Kuna class mate wangu mmoja Mzanzibari, alikuwa hataki kuikaribia kabisa shughuli yoyote yenye mlio wa ngoma ngoma, hata iwe ya kiisilamu
 
mpongezeni Diamond na hamonize kwa zile nyimbo zake zinazoharibu maadili ya watoto wa kitanzania, zilizomfanya akapata pesa na kujengea msikiti. mpeni maua yake.
 
Kutofautiana ndiyo heri zenyewe hizo, zinatufanya kila mmoja wetu kuchimba na kutafuta elimu ya ukweli.

Wewe unangoja nini kuwa Muislam?
 
Wanawake huwa tunaona mbali, wee mtu anawanyambua mabosi wake hadharani, mara anasema walikuwa wanamlisha ugali na sukari ndo angeweza kumstiri mke?
Siku vingeumana angeenda klauzi kusema mke alikuwa anampa nyama mbichi (elewa neno nyama) 🤣🤣🤣🤣

Mwanaume kifua bwana, mwanaume koromeo, mwanaume hasusi.... lile sakata lilionesha ana umama mwingi, kiasi akimbiwe.
Tamaa zinawasumbua, huyu hakumpenda Feitoto Bali alipoenda umaarufu wa Feitoto. Feitoto ashukuru hili sakata lake na yanga kwani limemsaidia kumjua vizuri mwanamke aliyetaka kufunga naye ndoa.
 
mpongezeni Diamond na hamonize kwa zile nyimbo zake zinazoharibu maadili ya watoto wa kitanzania, zilizomfanya akapata pesa na kujengea msikiti. mpeni maua yake.
Wewe ukimpa inatosha, si walewale.
 
Mkuu ukitaka kupata jibu lako fanya hii mbinu mm niliitumia nikaachwa ..

Nenda hospitali ya private uchwara.. bonga na dr pale mpe kama 15k, mwambie nataka kumpima mpenzi wangu hivyo nataka uufunge huu mkono misili ya umevunjika.. atakupiga piop safi akimaliza mpandie demu wako hewani mwambie umeanguka na kuvunjika mkono ndani kwa ndani.

Huyo mwanamke wako atajitahidi kukuona akijifanya anakuhurumia sana usiogope mvute aje gheto alafu akisha kuona baada ya siku kadhaa utakua umepata jibu.

Hilo gongo usikae nalo zaidi ya siku tatu maana litapindisha mfupa hakikisha kakuona kabla ya hizo siku..

Alafu leta mrejesho hapa
 
Kweli matatizo katika mahusiano ni majaribu na kipimo cha uvumilibu!!
 
Mkuu ukitaka kupata jibu lako fanya hii mbinu mm niliitumia nikaachwa ..

Nenda hospitali ya private uchwara.. bonga na dr pale mpe kama 15k, mwambie nataka kumpima mpenzi wangu hivyo nataka uufunge huu mkono misili ya umevunjika.. atakupiga piop safi akimaliza mpandie demu wako hewani mwambie umeanguka na kuvunjika mkono ndani kwa ndani.

Huyo mwanamke wako atajitahidi kukuona akijifanya anakuhurumia sana usiogope mvute aje gheto alafu akisha kuona baada ya siku kadhaa utakua umepata jibu.

Hilo gongo usikae nalo zaidi ya siku tatu maana litapindisha mfupa hakikisha kakuona kabla ya hizo siku..

Alafu leta mrejesho hapa
Hiyo hela si bora nikalewe bar
 
Huyu kijana ni mjinga sana.

Haelewi hata nini cha kuongea kama kijana wa Kiislam.

Waislam hatutakiwi kuwa na "wapenzi" nje ya ndoa.

Unaruhusiwa kuwa na mchumba tu, tena mnayekutana na kuongea mbele ya maharim wake.

Nje ya hivyo ni kinyume na Uislam.
Lwa hiyo vijana wa kiislamu wao sio waasherati, wanaoa na kuelewa wakiwa bikra?

Dunia ya sasa haiangalii dini ya mtu, inatuadhibu wote kwenye kapu moja, wengi wetu bila kujali dini na imani ni wazinzi wa kufa mtu.
 
sahihi 100%
 
Ukweli ni kwamba, Mdogo wangu feitoto, Alikua anachapiwa huyo demu kitamboo sana !!.
 
Lwa hiyo vijana wa kiislamu wao sio waasherati, wanaoa na kuelewa wakiwa bikra?

Dunia ya sasa haiangalii dini ya mtu, inatuadhibu wote kwenye kapu moja, wengi wetu bila kujali dini na imani ni wazinzi wa kufa mtu.
Hakuna dunia ya sasa na ya zamani, dunia ipo, utakuja na utaondoka utaiacha kama ilivyo. Tia akili kidogo.
 
Huyu kijana ni mjinga sana.

Haelewi hata nini cha kuongea kama kijana wa Kiislam.

Waislam hatutakiwi kuwa na "wapenzi" nje ya ndoa.

Unaruhusiwa kuwa na mchumba tu, tena mnayekutana na kuongea mbele ya maharim wake.

Nje ya hivyo ni kinyume na Uislam.
Acha kumuonea Fei, Dubai kwenyewe tena kipindi cha Mwezi wa Ramadhani, bint mrembo maridhawa wa kiarabu tena swala tano nikajifanya muungwana kwa kumwambia ni mwezi wa Ramadhani, yeye akanitamkia kwamba "Ramadhani ipo huko nje, humu ndani hakuna Ramadhani"

Sasa ndiyo unataka umbebeshe hu mzigo Fei ambaye ni kijana kutoka sijui Pingwe , sijui Kizimkazi...usimuonee bana
 
Back
Top Bottom