Nikiwa mdogo nilikuwa naitwa minjino...ilikuwa experience mbaya sana, nilijichukia sana. Mwaka 2009 nikaamua kuweka braces baada ya kujichanga kwa muda kiasi. Niliambiwa na daktari chanzo cha meno yangu ya juu na ya chini kukaa vibaya ni kuwa nilikuwa nayasukuma nje kwa ulimi. Kabla ya kuwekewa braces nilifanyishwa mazoezi ya namna ya kuegemeza ulimi ili nisiwe nauegesha kwenye meno. Mwaka 2012 nikatolewa braces na sasa navaa retainers kila usiku asubuhi natoa. Retainers zinahakikisha meno yanabaki kwenye position inayotakiwa. Siku hizi huduma za kurekebisha meno zipo kwa wingi nchini kwa watoto na kwa watu wazima.Wenye tatizo la dental formation mbovu wasikate tamaa