Huyu hapa ni Katibu Mkuu wa UVCCM, Je huyu naye ni kijana?

Ila huko uvccm sielewi umri wao wanahesabu vipi ?hata uncle wangu uvccm tangu nipo mwanafunzi wa primary na leo nimeshaanza kuwa mtu mzima ila still yupo kwa cheo chake.
 
Uvccm ni umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi, hv inakuweje mtendaji wao anakuwa mzee??? Hv ccm kwenye hili hamjatumia akili, waacheni vijana wajisimamie wenyewe,.. mtu ana miaka 50 mnampa kz ya kwenda kuwatumikia vijana wkt huo vijana wapo wenye uwezo huo, au uvccm hakuna vijana wa kuisimamia hiyo idara mpk mchukue mtu mzima kutoka chadema??? ccm kama vp ombeni vijana kutoka chadema waje wawaendeshee hiyo jumuiya kuliko kuwapachika vizee na kuvifanya ni vijana
 

Ni libabu !! Litakua na wajukuu kadhaa wako chekechea au hata darasa la kwanza
 
Nafasi ya Katibu wa UVCCM haihitaji kuwa lazima awe kijana. Kuna makatibu wa UVCCM wa wilaya na mikoa wana miaka hadi zaidi ya 55
 
Ccm kila mtu ni kijana. Makamba, Nape, Mwigulu, Kigwangalla ambao wanautafuta miaka 60 wanaitwa vijana.
Neno vijana linategemea linatoka kwa mtu wa umri gani, mfano wazazi wangu wapo above 80 na mimi naelekea miaka 40 hivyo kuniita kijana wao siyo mbaya japo umri wangu umepita kwenye rika la ujana...
Kuitwa kijana haimaanishi kuwa wewe ni kijana, bali muda mwingine inamaanisha kuwa wewe mdogo kiumri kulingana na huyo anaekuita kijana..
 
Kwamba hata John Malecela anaweza kuwa Katibu wa UVCCM , na kwamba atakaposoma risala ya umoja huo mbele ya Mh Samia ataanza na neno "sisi vijana tunaunga mkono uwekezaji wa bandari" ?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ujumbe umefika kwa mamlaka za juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…