Huyu jamaa anaitwa Kuringe kaingia mjini

Huyu jamaa anaitwa Kuringe kaingia mjini

Kuna jamaa anaitwa Kuringe, kaingia mjini Dar es Salaam na shoka.
Na ana kata kulia na kushoto akiwanunua watu na viwanja vyao kama hana akili nzuri.

Ukienda wilaya ya Kinondon i utamkuta yupo tele kila mahali.
Mitaa ya Goig Mbezi Beach kanunua mtaa mzima.

Kama utafika Mbezi NSSF road ile RED Hall ni yake.
Ile Kuringe Sports Bar kulekea Baraza la Mitihani haya tena, na hivyo ni baadhi tu ya vitega uchumi na viwanja alivyonunua Kinondoni.

Jina halisi la Kuringe nasikia ni somebody Edward Mushi, kijana mdogo ambaye zimemtembelea.

Nimeona hii clip mahali, nikaona nimpe ushauri wa bure.

Namshauri tu, bwana Kuringe , aste aste brother, taratibu jiji hili la Chalamila, wengi wametajirikia hapa, ila wengi pia wamefilisikia hapa DSM.
Kula na kipofu, gusa mkono wa mwanasiasa wa Kinondoni, ndo utalijua Jiji.

======
Mwekezaji Joanna Chifunda aeleza kuhusu uvamizi wa eneo lake la biashara liliopo Mikocheni kwa Nyerere Jijini Dar es salaam. Inadaiwa kwamba fremu saba katika plot namba 27 zilivunjwa na Watu waliojitambulisha kwamba wametumwa na Kuringe ambaye anadai kwamba amenunua eneo hilo baada ya kuingia makubaliano na kumlipa Mmiliki aitwaye Zacharia Maftah.

Joanna Chifunda anaeleza kwa kirefu zaidi alipofanya mahojiano na Waandishi wa habari siku ya Jumamosi, Oktoba 12, 2024 mbele ya fremu hizo zilizovunjwa.

Abdulmajid Zakaria Maftah ambaye amejitambulisha kama ni mmojawapo wa watoto saba wa mzee Zakaria Maftah akieleza kuhusu uvamizi na mgogoro wa ardhi katika eneo liliopo kwenye plot namba 27, Mikocheni kwa Nyerere Jijini Dar es salaam.
Inadaiwa kwamba fremu saba katika eneo hilo zilivunjwa usiku wa kuamkia Oktoba 12, 2024 na Watu waliojitambulisha kwamba wametumwa na Kuringe ambaye anadai kuwa amenunua eneo hilo baada ya kuingia makubaliano na kumlipa Mmiliki aitwaye Zacharia Maftah.
Kuringe ni Bilionea wa Kibosho mwenye fedha za manyoka!! Ana utajiri ambao hauna tija. Believe me
 
Huyo jamaa ni wa kitambo sana kwenye figisu za Ardhi sema watu kama hawa wanapenda sana watu wasiokua na nguvu wao wanafanya chochote ukiingia kwenye miguu ya huyo mzala hautoki hata mahakamani ana nguvu za chini chini kama jeshi la China niliwahi kushuhudia mtu akiamishwa kwa nguvu kwenye eneo ambalo walikua na kesi nae na baadae akaja kushinda huyo Kuringe kwa nguvu za fedha vurugu nyingi alifanya 2006 mpaka 2014..
Sema anajiwekea mazingira mabovu siku hizi watu hawapendi kuonewa
 
Nakuamini asilimia 100 huyo jamaa nilishawahi kumfanyia kazi moja. Pesa alizonilipa hata nilichofanyia sijui mpaka leo
Ananunua biashara au nyumba za watu, wakati wa kulipa hata kama ni Tsh 500 Millioni anakuletea kwenye maboksi.

Wengi aliowanunua hawafaidiki na fedha hizo, yaani wanarudi nyuma kiuchumi au wanakufa kiuhai. Ninayo mifano
 
Kuna mdau kwetu21 hapo juu kagusia.jambo la.muhimu.sana.la.kujenhwa.fremu nyingi kuliko wateja.katika jiji la.dsm.

Mfano Mbezi beach kuanzia Rainbow mpaka kona ya kilongawima kwa mwamunyange kuna utitiri wa fremu za biashara. Nadhani hizi fremu zingine ni pesa chafu zinasafishwa kwa mtindo wa kujenga fremu japo waturuki nao.wameibuka.sana kukodi viwanja na kujenga fremu halafu rent.inakuwa.dola 700 per.month.

Wazee wa.mipango miji.sijui wamelala.wapi.usingizi niaibu.sana mji kutokuwa na maeneo maalum yaani residential, openspace kama lile eneo baa ya.didiz ilipowekwa haya.mambo yameibuka.magufuli amefafiki
Uchumi wetu unategemea uchuuzi
Huoni mpaka lugalo pale kuna frame

Ova
 
Ukisikiliza vizuri ni kwamba maftah alikuwa na mke ambae alifariki ambae ndo alikuwa mama wa wale watoto wakubwa...Maftah amezeeka sana..mke mdogo alimshawishi wakauza plot yenye jina la mkewe marehemu na wakamuuzia kuringe na fedha kuringe aliweka kwenye akaunti ya huyo bi mdogo ambae ni mama wa Kambo wa vijana... Wale vijana wakaja juu na kwenda mahakaman kupinga mama wa Kambo kwanini kauza kiwanja Cha marehemu mama Yao...basi kwa pembeni ndo kuna huyo mwekezaji aliejenga kwa mkataba wa miaka kumi na ambae kiwanja kile alichojenga mwekezaji ndo kina jina la maftah, ndo Mzee maftah akaamua kumpa kuringe mbadala... MAANA wale vijana wataishinda tu kesi...
Na huyu mwekezaji pia atashinda tu...kupanga na kujenga Kisha baada ya miaka kumi uwekezaji unarudi kwa mwenye plot Wala sio hatari..hata NHC Kuna sehemu waliwapatia matajiri wakajenga magorofa kwa mkataba wa miaka 30 halafu nyumba inarudi kwa mwenye plot...aliejenga anakuwa amerudisha gharama zake halafu anaendelea kuwa mpangaji
Ninachokiona huyu maftah alitapeliwa, huwezi mpangisha MTU nae apangishe MTU mwingine bila maridhiano, huyu Dada nae anaisemea kampangisha MTU mwingine, hata NHC hii haikubaliki, Maftah katapeliwa
 
Familia ipo upande wa mwekezaji
Hili suala la uzee unaweza Kuta mpangaji wa mwanzoni Ndio alitumia Kwa kumrubuni Mzee Kwa pesa za uji na mkataba wa miaka kumi!! My Goddess!! Sasa Familia imeshtuka na kuona Bora kuuza, unaweza kukuta familia inapambana na mkataba wa miaka kumi wa mwanzoni wa kinyonyaji na sio mauziano na kuringe, huyo mpangaji anatakiwa amlalamikie maftah na sio Kuringe mnunuzi mpya
 
Ukisikiliza vizuri ni kwamba maftah alikuwa na mke ambae alifariki ambae ndo alikuwa mama wa wale watoto wakubwa...Maftah amezeeka sana..mke mdogo alimshawishi wakauza plot yenye jina la mkewe marehemu na wakamuuzia kuringe na fedha kuringe aliweka kwenye akaunti ya huyo bi mdogo ambae ni mama wa Kambo wa vijana... Wale vijana wakaja juu na kwenda mahakaman kupinga mama wa Kambo kwanini kauza kiwanja Cha marehemu mama Yao...basi kwa pembeni ndo kuna huyo mwekezaji aliejenga kwa mkataba wa miaka kumi na ambae kiwanja kile alichojenga mwekezaji ndo kina jina la maftah, ndo Mzee maftah akaamua kumpa kuringe mbadala... MAANA wale vijana wataishinda tu kesi...
Na huyu mwekezaji pia atashinda tu...kupanga na kujenga Kisha baada ya miaka kumi uwekezaji unarudi kwa mwenye plot Wala sio hatari..hata NHC Kuna sehemu waliwapatia matajiri wakajenga magorofa kwa mkataba wa miaka 30 halafu nyumba inarudi kwa mwenye plot...aliejenga anakuwa amerudisha gharama zake halafu anaendelea kuwa mpangaji
Sure unanajua story vizuri. Maftah ni mzee kweli yule mke wake mdogo ni mshenzi kweli

Hiyo sehemu mwanzoni kuna mtu alinunua hakukamilisha pesa akarudishiwa
 
Back
Top Bottom