Huyu Jamaa naye ana jambo gani kuhusu CHADEMA, tumpuuze au tumsikilize?

Kwahio huwa unasikiliza watu na sio hoja nyuma ya hayo watu ?

Nadhani unakosea kufanya hivyo, be objective even a Broken Clock is right twice a Day..., Vilevile yoyote yule anaweza kutoa Pumba...., Hence Usijadili watu Jadili Hoja...
 
Shamra Shamra kwani hii ni Kitchen Party ? No wonder haya yanaendelea kutokea....

Wanahangaika na kubadilisha chupa wakati mvinyo ni ule ule..., politicians wote wamekuwa self serving they do not care about people zaidi ya kuwatumia kama ngazi ya kupata kura kwenda kula...
 
Wote Mwajiriwa na Mwanachama wote wanatakiwa kufuata kanuni na taratibu za taasisi waliyomo. Kuwa mwanachama hakukupi haki yakuitisha press conference chini ya taasisi yako na kuzungumzia mambo ya taasisi na sasa hivi yupo live anazungumzia mambo ya taasisi (uchaguzi).

Kama mwenyekiti wake ameonyesha kutoridhishwa na utaratibu wa Makamu Mwenyekiti wake kuzungumza na vyombo vya habari na kusema amekiuka taratibu za chama kwamba kuna watu wanaotakiwa kuzungumzia mambo ya chama, je Malissa hajakiuka huo utaratibu ?

Mwanachama kama binadamu ana haki ya kujielezea kama yeye lakini si kwa kutumia jina na nafasi aliyonayo katika chama kwa maana inaweza kuchanganya umma kwa kudhani kauli yake ndio msimamo wa chama. Kuna haki lakini kuna wajibu pia kama mwanachama anaotakia kuutimiza.

Ntobi alikuwa na haki ya kutoa maoni yake kuhusu Lissu kupitia mtandao wake lakini alikiuka taratibu na kanuni za chama na kuwajibika.

Bado Lema ana press conference nayo inakuja, picha tunayoipata ni kuwa sasa kila mmoja anaweza kuzungumzia chama na hakuna utaratibu maalumu unaoeleweka kwa umma kupata taarifa sahihi

 
Tatizo huelewi uhuru ni nini wala demokrasia ni nini.

CHADEMA inakataza wanachama kufanya press conference? Unaposema "chini ya chama" maana yake nini?

Kanuni gani ya CHADEMA inamkataza mwanachama kufanya press conference na kuongelea mambo ya chama?

Ntobi alitoa kashfa. Kaadabishwa kwa kanuni za chama. Sasa unataka kumzima mdomo Malissa kabla hajasema? Muache atukane halafu akitukana muadabishe. Hakuna sheria ya kumfunga mtu kabla hajafanya kosa. Ikiwapo sheria hiyo itakuwa haina haki.

Tatizo la Tanzania si press conference nyingi, tatizo hatuna uburu wa kufanya press conferences za kutosha.

Sasa Malisa kashasema. Watu wamepata kumsikia na yeye kapata kuongeza uwazi anafikiri nini.

Umepata nafasi ya kupinga au kukubali alichosema.

Hiyo nafasi usingeipata kama Mqlissa angezuiwa kusema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…