Huyu jamaa yangu ni mchawi au ni roho mbaya tu?

Huyu jamaa yangu ni mchawi au ni roho mbaya tu?

Kuna nyakati huwa tunawachukia wanaotuambia ukweli.

Lakini kama una uhakika na unachokifanya basi pambania mpaka mwisho.

Ila kwa ulichoandika hapa ni maisha ya wengi mtaani, sio Kila anayekuambia hautafanikiwa ni mchawi, ila wengi wao wamekata tamaa na wanaona hata wewe hautafanikiwa pia na utaishia kuwa kama walivyoishia wao yaani utashindwa.
 
Huyu mshikaji wangu nashindwa kumuelewa,tuko nae kwenye harakati kitambo tu ila naona ni kama kaanza kuwa na roho ya kichawi hivi.
Yeye ameanza hizi harakati za kupiga paper za ajira za serikali kitambo tu na kwa maelezo yake hajawahi kufika oral hata moja.
Sasa me mwaka huu nilimuambia tukaze tuingie hata oral tu.picha lilianza mwaka huu mwezi wa tatu tumepiga written ya tanzania airports authority tukachemka coz marks hazikutosha,hapo kwa sababu tulidunda wote sikuona any bad sign kutoka kwake.
Then tukaja tukapiga written ya gaming board yeye akachemka mimi nikaitwa oral nikaanza kuona jamaa kama ananipa kauli flani za kejeli na kunikatisha tamaa,sikujali sana me nikajiandaa fresh tu nikapiga oral then nikatulia ila kila siku ananipigia kuniuliza vipi majibu ya oral yametoka nikimuambia sijasikia lolote mpaka sasa jamaa anaanza kuniambia hapo hutoboi fanya mambo mengine tu,nikawa nawaza huyu jamaa kaanza kuwa mchawi wangu nini?
Sasa ngoma ni ya hivi karibuni,baada ya matokeo ya tra kutoka ilionyesha mimi na yeye wote hatukuchaguliwa,nakumbuka siku hiyo mimi niliumia sana moyoni ila jamaa yeye alikua fresh tu tena ndo kwanza akanialika hadi kunywa bia,bahati nzuri tra wakatoa nafasi ya kukata rufaa,jamaa nikamwambia kuna issue za rufaa kama vipi tukate yeye kaanza tena kunikatisha tamaa,mimi nikajilipua nikakata rufaa,jamaa kila siku ananifuatilia kujua kama rufaa yangu ishajibiwa nikimuambia bado anaanza tena maneno ya kukatisha tamaa.
So jana ndo akanichosha zaidi,rufaa yangu jana ikajibiwa kuwa imekubaliwa,nikampigia jamaa kumwambia ile nimemwambia tu kuwa nimefanikiwa jamaa akajibu tu unapoteza muda then akakata simu.
Nimemuwaza sana jamaa nikajiuliza ameanza kupaa na ungo nini maana sio kawaida yake hii?

Wachawi wapo very technical, maswali Yao hayapo wazi hivyo
 
Ishu inayohitaji mafanikio kwa juhudi zako, kaa kimya usimshirikishe mtu yeyote kwenye utafutaji na wewe unatafutwa, hivyo ukiona Kuna Hali ya hatari basi ongeza kiwango cha umakini zaidi!
 
Ukisha mjuaa mchawii wako upati tabu unaishiii nae kw akilii, tatizo wew ten unamshirikisha mambo yako
 
Mimi nakumbuka kuna kipindi getto hata TV nilikuwa sina kwa sababu ilikuwa sii kipaumbele changu.
Sasa mwanamke ambae mpaka sasa naishi nae kipindi hicho ndio mapenzi yalikuwa yameanza sasa alikuwa akija getto anaboeka sana akalazimisha ninunue tv.
Nikaenda kko nikatafuta 32 inches nikafunga na dstv.
Sasa kuna jamaa yangu wa damu damu mishe mishe nyingi tulikuwa tunafanya nae kuna siku kaja kunitembelea alivyokuta kale ka tv alikunja sura waziwazi akauzunika sana kisha akashika kiuno akanambia joooh umenipiga na kituu kizitoo kichwani daa nilifikiria sana huyu jamaa siku akisikia nimenunua hata gari sianakuua kabisa sasa hivi mambo yangu ni kimya kimya.
mimi nina project ninayoo ni ujenzi wa hotel, basi kuna huyo mama ni mkubwa sana kwangu ila ndo huwa ananiulizia sana progress ya project, sikuwahi kuwaza kwa nini anafatilia sana, juzi sasa eti ananimbiaje eeh sasa kwa nini unajenga hotel ukifa mume wako si atavichukua nikamwambia sifi katika jina la yesu,, lol bado nawaza mpka leo kwa nini anawaza nitakufa halafu mume atachukua mirathi, ka hiyo anataka nisifanye investment yoyote kwa sababu kuna siku nitakufa.
 
Wachawi utawaweza basi si ndiyo kama hawa njaa 55 wanaokataa talaka ya chadema kwa nguvu.
 
Wachawi wana namna yao ya kufanya mambo yao.. Huyo sio mchawi bali ana roho ya kwanini
mshana ww roho ya kichawi ilikuchukua mda gan kukutoka maana Kuna Uzi uliwahi kusema ww ulikuwa ukitongoza mwanamke akikukatalia basi unaloga asiolewe milele wanaume wakimuona waone ni kama baba level.
 
Mchawi hapo ni wewe, unajiloga mwenyewe kuna haja gani ya kumshirikisha mambo yako na umeshajua fika anakukatisha tamaa? Mshirikishe Mungu inatosha.

Tatizo lipo kwako punguza kumwambia mambo yako.
Mimi nipo tofauti Sana na NEGATIVE MOTIVATION ndio imenifanya niweze kuachieve vingi.

Ukinambia HUWEZI ,HUTOFANIKIWA, WALIKUWEPO ZAIDI YAKO, KAPYALU, HUNA LOLOTE..NDUGU HAPO NDIPO NAPATA ENERGY YA KUFANYA KWA BIDII ILI KUFANIKISHA LENGO/ MALENGO.
 
Wahenga wanasema usimshirikishe mtu mambo yako jambo lako mpaka likae sawa yaaan utaanza kusema watu wachaw kumbe umejiroga mwenyewe
Rafiki yako anaroho ya kwann upate wewe na sio yeye sio roho mbaya ila ni ya kwann wewe?
 
Huyo sio mchawi ila ameathirika na vibuti vya interview ameshajikatia tamaa.

Haya mambo ya ajira usipokuwa shupavu unaweza kuwahuka unakuta umesoma ukafaulu vyema uwezo upo ila kazi hupati na umri unasonga hatari sana yasikieni tu omba yasikukute.
 
Wewe ndio mchawi, na dawa ni huyo
Unamshirikisha kila jambo huku ukijua ni nyoka.
Nakushangaa wewe unaeshangaa
Unamuita kabisa rafiki huyo
 
Mimi nipo tofauti Sana na NEGATIVE MOTIVATION ndio imenifanya niweze kuachieve vingi.

Ukinambia HUWEZI ,HUTOFANIKIWA, WALIKUWEPO ZAIDI YAKO, KAPYALU, HUNA LOLOTE..NDUGU HAPO NDIPO NAPATA ENERGY YA KUFANYA KWA BIDII ILI KUFANIKISHA LENGO/ MALENGO.
Hiyo tunaita kupruvu wrong
 
Washkaji wa hivyo ni wengi mbona mkuu hata sie tunao mtu unamuomba CV tuu uedit anaona utatoboa ila mwisho wa siku tunawapotezea maisha mengine yanaendelea
 
Achana naye huyo. Adui wako hatoki mbali, ni yule anayekufahamu. Hakuna mtu wa kukutakia jema zaidi ya wazazi wako kama ulikuwa mtoto msikivu. Waliobaki hakuna anayejali mafanikio yako mkuu.

Marafiki wa kweli ni wale wasiokujua. Bora marafiki wa JF kuliko ulionao kitaa.
 
Jaribu kumficha ikiwa unaona hana furaha na hatua zako Mkuu .

Hamna uchawi hapo
 
Fanya kazi kwenye ushauri uliopewa,

Ila watu wana roho mbaya, chuki, wivu, husuda,

Mimi ni binadamu Niko na mapungufu kadhaa Ila hayo Mungu niepushe nayo kwa wengine.
 
Maisha yako ya mapambano ni matangazo kwa rafiki. Harakati zako pia ni matangazo kwa rafiki wako.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom