Huyu mshikaji wangu nashindwa kumuelewa,tuko nae kwenye harakati kitambo tu ila naona ni kama kaanza kuwa na roho ya kichawi hivi.
Yeye ameanza hizi harakati za kupiga paper za ajira za serikali kitambo tu na kwa maelezo yake hajawahi kufika oral hata moja.
Sasa me mwaka huu nilimuambia tukaze tuingie hata oral tu.picha lilianza mwaka huu mwezi wa tatu tumepiga written ya tanzania airports authority tukachemka coz marks hazikutosha,hapo kwa sababu tulidunda wote sikuona any bad sign kutoka kwake.
Then tukaja tukapiga written ya gaming board yeye akachemka mimi nikaitwa oral nikaanza kuona jamaa kama ananipa kauli flani za kejeli na kunikatisha tamaa,sikujali sana me nikajiandaa fresh tu nikapiga oral then nikatulia ila kila siku ananipigia kuniuliza vipi majibu ya oral yametoka nikimuambia sijasikia lolote mpaka sasa jamaa anaanza kuniambia hapo hutoboi fanya mambo mengine tu,nikawa nawaza huyu jamaa kaanza kuwa mchawi wangu nini?
Sasa ngoma ni ya hivi karibuni,baada ya matokeo ya tra kutoka ilionyesha mimi na yeye wote hatukuchaguliwa,nakumbuka siku hiyo mimi niliumia sana moyoni ila jamaa yeye alikua fresh tu tena ndo kwanza akanialika hadi kunywa bia,bahati nzuri tra wakatoa nafasi ya kukata rufaa,jamaa nikamwambia kuna issue za rufaa kama vipi tukate yeye kaanza tena kunikatisha tamaa,mimi nikajilipua nikakata rufaa,jamaa kila siku ananifuatilia kujua kama rufaa yangu ishajibiwa nikimuambia bado anaanza tena maneno ya kukatisha tamaa.
So jana ndo akanichosha zaidi,rufaa yangu jana ikajibiwa kuwa imekubaliwa,nikampigia jamaa kumwambia ile nimemwambia tu kuwa nimefanikiwa jamaa akajibu tu unapoteza muda then akakata simu.
Nimemuwaza sana jamaa nikajiuliza ameanza kupaa na ungo nini maana sio kawaida yake hii?
mimi nina project ninayoo ni ujenzi wa hotel, basi kuna huyo mama ni mkubwa sana kwangu ila ndo huwa ananiulizia sana progress ya project, sikuwahi kuwaza kwa nini anafatilia sana, juzi sasa eti ananimbiaje eeh sasa kwa nini unajenga hotel ukifa mume wako si atavichukua nikamwambia sifi katika jina la yesu,, lol bado nawaza mpka leo kwa nini anawaza nitakufa halafu mume atachukua mirathi, ka hiyo anataka nisifanye investment yoyote kwa sababu kuna siku nitakufa.Mimi nakumbuka kuna kipindi getto hata TV nilikuwa sina kwa sababu ilikuwa sii kipaumbele changu.
Sasa mwanamke ambae mpaka sasa naishi nae kipindi hicho ndio mapenzi yalikuwa yameanza sasa alikuwa akija getto anaboeka sana akalazimisha ninunue tv.
Nikaenda kko nikatafuta 32 inches nikafunga na dstv.
Sasa kuna jamaa yangu wa damu damu mishe mishe nyingi tulikuwa tunafanya nae kuna siku kaja kunitembelea alivyokuta kale ka tv alikunja sura waziwazi akauzunika sana kisha akashika kiuno akanambia joooh umenipiga na kituu kizitoo kichwani daa nilifikiria sana huyu jamaa siku akisikia nimenunua hata gari sianakuua kabisa sasa hivi mambo yangu ni kimya kimya.
mshana ww roho ya kichawi ilikuchukua mda gan kukutoka maana Kuna Uzi uliwahi kusema ww ulikuwa ukitongoza mwanamke akikukatalia basi unaloga asiolewe milele wanaume wakimuona waone ni kama baba level.Wachawi wana namna yao ya kufanya mambo yao.. Huyo sio mchawi bali ana roho ya kwanini
Mimi nipo tofauti Sana na NEGATIVE MOTIVATION ndio imenifanya niweze kuachieve vingi.Mchawi hapo ni wewe, unajiloga mwenyewe kuna haja gani ya kumshirikisha mambo yako na umeshajua fika anakukatisha tamaa? Mshirikishe Mungu inatosha.
Tatizo lipo kwako punguza kumwambia mambo yako.
Hiyo tunaita kupruvu wrongMimi nipo tofauti Sana na NEGATIVE MOTIVATION ndio imenifanya niweze kuachieve vingi.
Ukinambia HUWEZI ,HUTOFANIKIWA, WALIKUWEPO ZAIDI YAKO, KAPYALU, HUNA LOLOTE..NDUGU HAPO NDIPO NAPATA ENERGY YA KUFANYA KWA BIDII ILI KUFANIKISHA LENGO/ MALENGO.