Huyu Jemedari Said ndio maana Yanga hawampendi, amenyooka sana

Huyu Jemedari Said ndio maana Yanga hawampendi, amenyooka sana

Nilisikia watu wana msifia kanyooka, nilitamani nione kipi kipya cha maana alichoongea. Kumbe hoja zenyewe ndio hizi halafu watu ndio wanaona jamaa kichwa haswa. Kama huyu ndio anaonekana ni mtoa madini basi Watanzania wana upungufu wa maarifa
Shambulia hoja na sio mleta hoja
 
Wameweka kanuni ila hakuweka sababu za msingi katika hiyo taarifa. Katika kanuni waliyoweka ina state kuwa mechi inaweza kuhairisha kama kuna sababu za msingi ama dharura. Sasa hao bodi ya ligi wangekuwa na uweledi kama wangesema hizo dharura au sababu ya msingi katika tukio lile ni lipi.

Tayari juu bodi ya ligi walisha declare kuwa Simba hawakufanya mawasiliano na maofisa wa mechi, meneja wa uwanja pamoja na timu mwenyeji kwaajili ya kuandaliwa mazingira ya wao kufanya mazoezi hapo tayari bodi ya ligi limekiri swala la usalama limetokana na uzembe wao Simba.
Mkuu sababu za dharura na za msingi aziwezi kuwa hizo zinazosemwa na bodi Wala uyo jemedari,,sababu za msingi na za dharura zinatakiwa ziwe sababu nzito ambazo zinaweza kupelekea kutochezwa mechi mfano ugaidi, wachezaji kupata ajali mbaya etc, kwa maana iyo bodi ya ligi aikuwa na sababu yoyote ya msingi ya kuahirisha mechi na sababu za kiusalama Wenye mamlaka ya kutoa ripoti ya kiusalama ni jeshi la polisi kama kungekuwepo na jambo kama ilo kwaiyo kanuni wanayoegemea vilaza walio wengi aitoi mpenyo huo!
 
Huyu Jemedari mnayemsifia na yule anayejiita mzee wa jambia ndo watetezi wa simba. Hawa jamaa ndo wanawapoteza simba kwa kuamini kwamba propaganda zao na chuki zao kwa Yanga zitawapa mafanikio.

Anyway Tanzania wananchi wake wanaamini kwenye propaganda. Na wanaamini propaganda za media ndo kila kitu. Ndo maana hata hapa JF tangu simba wagomee mechi kumekuwa na mada nyingi sana za kutetea yale maamuzi ya kipambavu walioyafanya wanaoitwa viongozi wa Simba.

Kwa ujinga na upambavu huu tutaendelea kusheherekea mafanikio ya kufika robo fainali mara 6 mfululizo na ujinga wa namna hiyo.
Kuna la uongo alilosema hapo? Tuacheni ushabiki Yanga wanajipotosha sana.
 
Wameweka kanuni ila hakuweka sababu za msingi katika hiyo taarifa. Katika kanuni waliyoweka ina state kuwa mechi inaweza kuhairisha kama kuna sababu za msingi ama dharura. Sasa hao bodi ya ligi wangekuwa na uweledi kama wangesema hizo dharura au sababu ya msingi katika tukio lile ni lipi.

Tayari juu bodi ya ligi walisha declare kuwa Simba hawakufanya mawasiliano na maofisa wa mechi, meneja wa uwanja pamoja na timu mwenyeji kwaajili ya kuandaliwa mazingira ya wao kufanya mazoezi hapo tayari bodi ya ligi limekiri swala la usalama limetokana na uzembe wao Simba.
Wameweka sababu za msingi za kiusalama lakini jicho lako la ushabiki limechagua kutoziona, Usalama ni jambo la kipaumbele kuliko hata mchezo wenyewe.Jenga mazoea ya kusoma taarifa neno kwa neno.
 
Attachments

  • markup_43409.png
    markup_43409.png
    221.2 KB · Views: 1
Wameweka sababu za msingi za kiusalama lakini jicho lako la ushabiki limechagua kutoziona, Usalama ni jambo la kipaumbele kuliko hata mchezo wenyewe.Jenga mazoea ya kusoma taarifa neno kwa neno.
Wewe waache wajizime data kwa mihemko. Hivi kama wale makomandoo wa Yanga wasingeleta lile valangati na kuwaacha Simba waingie uwanjaani Bodi ya Ligi ingepata wapi nguvu ya kuahirisha mechi? Na kwa nini Uongozi wa Yanga kwenye tamko lao hawakulaani uhuni uliofanywa na makomandoo wao, ni dhahiri makomandoo walitumwa na uongozi kuwaprovoke Simba wakijua kuwa lazima Simba watasusa ili wapewe point za bure.
 
Wameweka sababu za msingi za kiusalama lakini jicho lako la ushabiki limechagua kutoziona, Usalama ni jambo la kipaumbele kuliko hata mchezo wenyewe.Jenga mazoea ya kusoma taarifa neno kwa neno.
Naomba pigia mstari kwenye hiyo taarifa ni wapi walipoanisha kuwa mechi imeahirishwa sababu ya usalama. Mimi nimesoma hiko kipengele kimesema mechi imeahirishwa ili kupata taarifa zaidi za kiuchungizi.

Taarifa imesema kuwa bodi imepokea taarifa ya ofisa usalama wa mchezo iliyoanisha matukio kadhaa yanayoambatana na Simba kufanya mazoezi.

Sijui hoja ya kiusalama mmeitoa wapi
IMG_20250311_105724.jpg
 
Ukweli ni kuwa Simba imekimbia kwa sababu ya kuhofia kufungwa kutokana na majeruhi walio nao! Upuuzi Mwingine wowote ni bullshit!

Mechi itachezwa tena, na Simba atafungwa kwa sababu wameshaingiwa na woga!

Bodi ya league itavunjwa kama sio leo basi hata mwisho wa msimu!
 
Naomba pigia mstari kwenye hiyo taarifa ni wapi walipoanisha kuwa mechi imehairishwa sababu ya usalama. Mimi nimesoma hiko kipengele kimesema mechi imehairishwa ili kupata taarifa zaidi za kiuchungizi.

Taarifa imesema kuwa bodi imepokea taarifa ya ofisa usalama wa mchezo iliyoanisha matukio kadhaa yanayoambatana na Simba kufanya mazoezi.

Sijui hoja ya kiusalama mmeitoa wapiView attachment 3266411
Unajua majukumu ya Afisa Usalama wa mechi? Unategemea taarifa ya Afisa Usalama wa mechi itabeba mambo yanayohusu "biashara ya mitumba Buguruni"?Unategemea waandike kila kitu wakati uchunguzi wa "kiusalama" unaendelea? Ukivua hiyo miwani ya kiushabiki utaielewa vizuri taarifa ya bodi kwani imetumia lugha rahisi sana.
 
Usianze kuonesha kupaniki mkuu kujibu majibu ya mipasho na short cut ni kama umeanza kuingia na hasira. Umeleta hoja ijadiliwe kwa kutumia mstari kwa mstari taarifa ya bodi ya ligi hivyo relax halafu jibu tu kwa utulivu

Swali langu la kwanza, kutokana na bodi ya ligi kusema kuwa sababu ya kuahirisha mechi ni kufanya uchunguzi kwa matukio yaliyoletwa na afisa usalama je
Ni kivipi kufanyika kwa mechi kungezuia huo uchunguzi kufanyika?

Taarifa ya afisa usalama ilikuwa inahusiana na siku ya mazoezi na ndio maana kwenye hayo maelezo ya bodi ya ligi wamesema "inayoambata na Simba kushindwa kufanya mazoezi " key point ni " kushindwa kufanya mazoezi "
Je kushindwa kufanya mazoezi ni halali mechi kuahirishwa? Kama ni halali ni kwa kanuni ipi inayosema kuwa timu isipofanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja husika, hapaswi kucheza mechi?
 
Rais wa Yanga amekaa na kamati yake ya utendaji wanadai hawatacheza mechi itakayopangwa.Yaani vichwa vyote vile vinatarajia kupewa point 3 za mezani!
Maswali Matatu muhimu
1) Je wale Makomandoo wa Yanga wana akili timamu?

2) Yanga waliendaje uwanjani wakati Mechi imeahirishwa?

3) Meneja wa Uwanja wa Taifa aliwafunguliaje Yanga milango wakati Mechibimeahirishwa?

Kuna matatizo makubwa kwenye uongozi wa Yanga na uongozi wa uwanja wa Mkapa
 
Naomba pigia mstari kwenye hiyo taarifa ni wapi walipoanisha kuwa mechi imehairishwa sababu ya usalama. Mimi nimesoma hiko kipengele kimesema mechi imehairishwa ili kupata taarifa zaidi za kiuchungizi.

Taarifa imesema kuwa bodi imepokea taarifa ya ofisa usalama wa mchezo iliyoanisha matukio kadhaa yanayoambatana na Simba kufanya mazoezi.

Sijui hoja ya kiusalama mmeitoa wapiView attachment 3266411
Yani unashindwa kuona kabisa swala la kiusalama limehusika hapo? Embu fikiria Simba walifanyiwa fujo wasifanye mazoezi,Endapo mechi ingechezwa na simba wangefungwa huoni kama kuna fujo zingetokea kwakuhisi simba wamefanyiwa hujma?.
 
Usianze kuonesha kupaniki mkuu kujibu majibu ya mipasho na short cut ni kama umeanza kuingia na hasira. Umeleta hoja ijadiliwe kwa kutumia mstari kwa mstari taarifa ya bodi ya ligi hivyo relax halafu jibu tu kwa utulivu

Swali langu la kwanza, kutokana na bodi ya ligi kusema kuwa sababu ya kuhairisha mechi ni kufanya uchunguzi kwa matukio yaliyoletwa na afisa usalama je
Ni kivipi kufanyika kwa mechi kungezuia huo uchunguzi kufanyika?

Taarifa ya afisa usalama ilikuwa inahusiana na siku ya mazoezi na ndio maana kwenye hayo maelezo ya bodi ya ligi wamesema "inayoambata na Simba kushindwa kufanya mazoezi " key point ni " kushindwa kufanya mazoezi "
Je kushindwa kufanya mazoezi ni halali mechi kuhairishwa?
Unajua mechi inaanza kuchezwa lini kikanuni? Unajua kiwango cha vurugu tarajiwa,unafahamu lengo la kufanya uchunguzi? Unafahamu iwapo Simba kwa kufanyiwa vurugu kama nao wangeamua kuja na mabaunsa wao kwenye mechi au usiku ule nini kingetokea?Yanga siku zote hupitia mlango uliokatazwa kikanuni pamoja na kujua kuwa watalipa tu faini,vipi Simba nao wawe wanakuja na mabaunsa wao kuwazuia kupitia geti la nyuma, usalama utakuwepo kweli? Ndio maana bodi wanafanya uchunguzi ili kutoa hukumu ya haki pengine hata kukomesha uhuni huo.Sasa wewe na viongozi wa Yanga badala ya kuona na kukemea uhuni wa makomandoo wa Yanga,nyie mnaona kosa la Simba kuonesha nia ya kugomea mechi tu,hayo sasa ndio macho ya kishabiki.Simba wasingepeleka timu uwanjani wangekuwa wamekosea kweli kikanuni,lakini mgomo pia ni njia ya kuonesha kutoridhika na hali fulani hata kama utapoteza.Mwaka 2021 Yanga pia wakionesha msimamo wao kwa kugomea mechi iliyosogezwa muda bila kufuata kanuni.Unaweza kunieleza sababu moja tu ya Yanga kutoingia kupitia mlango rasmi kila mechi pamoja na faini ambazo huwa wanalipa?
 
As
Usianze kuonesha kupaniki mkuu kujibu majibu ya mipasho na short cut ni kama umeanza kuingia na hasira. Umeleta hoja ijadiliwe kwa kutumia mstari kwa mstari taarifa ya bodi ya ligi hivyo relax halafu jibu tu kwa utulivu

Swali langu la kwanza, kutokana na bodi ya ligi kusema kuwa sababu ya kuhairisha mechi ni kufanya uchunguzi kwa matukio yaliyoletwa na afisa usalama je
Ni kivipi kufanyika kwa mechi kungezuia huo uchunguzi kufanyika?

Taarifa ya afisa usalama ilikuwa inahusiana na siku ya mazoezi na ndio maana kwenye hayo maelezo ya bodi ya ligi wamesema "inayoambata na Simba kushindwa kufanya mazoezi " key point ni " kushindwa kufanya mazoezi "
Je kushindwa kufanya mazoezi ni halali mechi kuhairishwa? Kama ni halali ni kwa kanuni ipi inayosema kuwa timu isipofanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja husika, hapaswi kucheza mechi?L
Mkuu Wala ukuwa na haja ya kumuelewesha zaidi kiufupi akuna sababu ya msingi kikanuni ambayo bodi imeainisha hapo kwamba wamesimamia iyo kuahirisha mechi aipo! Umemaliza Kila kitu,,unajua Kuna watu wanapotosha sana wengine wanajua lakini wanataka kupindisha mambo,,wengine awajui na wanajifanya wanajua,,hapo ndipo kwenye shida,,Shida kubwa hapa ni kanuni iliyotumika na bodi ya ligi kuahirisha mechi ni ipi? Na Simba wametumia kanuni ipi kugomea mechi? Kwasababu kuzuiwa kufanya mazoezi akutoi mwanya wowote kwa timu yoyote kugomea mechi!
 
Yani unashindwa kuona kabisa swala la kiusalama limehusika hapo? Embu fikiria Simba walifanyiwa fujo wasifanye mazoezi,Endapo mechi ingechezwa na simba wangefungwa huoni kama kuna fujo zingetokea kwakuhisi simba wamefanyiwa hujma?.
Tumehama kwenye sheria na kanuni sasa tumeamia katika mawazo binafsi? Nimeomba kanuni inayoelekeza timu isipofanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja unaotumika kwa mechi, hapaswi kucheza mechi.

2) kutokana na taarifa ya bodi ya ligi ni kwamba sababu iliyopelekea mechi kuahirishwa ni kufanya uchunguzi kwa matukio yaliyoletwa na afisa usalama je ni vipi kufanyika kwa mechi kungezuia huo uchunguzi kutokufanyika?
Hapa key point ni "uchunguzi " hayo uliyoandika wewe hayahusiani hoja ya "uchunguzi"
 
Hao wote wanapiga kelele ili wapeleke mkono kinywani tu maana siku hizi ajira zinazolipq ni hizi za midomo. Ukweli wa kilichotokea wanaujua Yanga na Simba na watakutana kucheza. Hakuna mtu kutozwa faini wala kupokwa point. Yanga na Simba hazifanyi biashara ya mpira peke yake.
 
sema nuli
Maandishi mengi lakini hakuna hata sehemu moja umejibu hoja za Jemedari,bila shaka wewe ni kati ya wanaoamini kuwa Yanga watapewa points 3 za mezani kama viongozi wa Yanga,haishangazi kuona kila kesi inayohusu mpira wanaangukia pu

Kuna la uongo alilosema hapo? Tuacheni ushabiki Yanga wanajipotosha sana.
sema nilichelewa kuandika uzi wenye maneno km ya jamaa uenda ningesifiwa na mm Nina akili kwnz yanga akili wenye nazo wawili tu unaewezaje kupeleka timu uwanjani wakati hamna hata refa kamisa na hata chochote cha kuongoza mchezo huo yaani mijinga Sana aisee lkn pia alowaruhusu waingie nae nani wakati taarifa imetoka hamna game! huo utemi wao ndio maana Simba akili nyingi hawataki kuburuzwa na wajinga
 
Halafu kuna watu humu wanaona viongozi wa Yanga wako sahihi kwenye hili
 
YANGA WAMETUMIA MBINU YA MABAUNSA KUSUDI ILI SIMA ASUSIE MECHI WAPATE ALAMA TATU ZA MEZANI LAKINI BADALA YAKE WAP NDO WAMEJIINGIZA KWENYE MTEGO WA KUPOKONYWA ALAMA TATU ZA MEZANI IWAPO WATAKQZA FUVU NA KUSUSIA MECHI ITAKQYOPANGWA UPYA.
HII NDO MAANA HALISI YA UBAYA UBWELA.
 
Rais wa Yanga amekaa na kamati yake ya utendaji wanadai hawatacheza mechi itakayopangwa.Yaani vichwa vyote vile vinatarajia kupewa point 3 za mezani!
Hata Arajiga Simba hawampendi uwanjani amenyooka sana
 
Back
Top Bottom