1.Kwamba Yanga wana matarajio hewa ya kupewa point 3 za mezani kwa mechi iliyofutwa.Wewe ni kati ya wanaoamini kuwa Yanga watapewa hizo points 3?
2.Kwamba Yanga wamewezaje kupeleka timu kwenye mechi iliyofutwa wakitegemea kupata point 3 za dezo?
3.Yanga wanawezaje kudai points 3 wakati kwenye mechi yao bodi haikupeleka waamuzi na maofisa wa mechi
4.Uchunguzi wa bodi haiwezi kubatilisha kuchezwa kwa mechi itakayopangiwa tarehe mpya
Ngoja nikujibu ndugu mwakilishi wa Bin Kazumari,
Kupewa point 3 inategemea na weledi wa mamlaka husika inayosimamia na kuongoza soka katika kusimamia na kutafsiri sheria na kanuni kwa haki na usawa.
Kutokana na madhaifu yaliyopo bodi ya ligi na TFF, Yanga hawawezi kupata point 3 hata wafanye nini. Lile tukio lingetokea kwa nchi za wenzetu wanaosimamia soka kwa kufuata kanuni wasingekaa kikao cha dharura ili kujadili tamko la Simba kuhusu kugomea mechi badala yake wao wangekaa kimya kusubiri muda wa kick off na taratibu za mechi zikibakia palepale.
Mamlaka ingefuata kanuni inasema nini kuhusu timu A kumzuia timu B ambaye ni mgeni kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja unaotumika kwaajili ya mechi. Na endapo kama itatokea huyu timu B kagoma kupeleka timu kwaajili ya mchezo hadi muda wa kick off basi watarejea katika kanuni zao kama kuna kipengele kilichoiruhusu kugomea mechi baada ya tukio ama lah. Kama ipo basi atakuwa na haki ya kugoma ila kama hakuna kanuni hiyo basi inatakiwa kanuni iangaliwe inasemaje kuhusiana na timu inayogomea mechi kwasababu ambazo hazijaanishwa kwenye kanuni.
2) Yanga walipeleka timu uwanjani kwa mechi iliyofutwa ili kutuma ujumbe kwa bodi ya ligi kuwa hakukuwa na uhalali kikanuni kuahirisha ule mchezo. Kama wewe nawe unaungana na bodi ya ligi kuwa ni halali kikanuni basi naomba nijibu maswali haya mawili tu
(i) Naomba kanuni inayoelekeza timu mgeni isipofanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja unaotumika kwa mechi, hapaswi kucheza mechi.
ii) kutokana na taarifa ya bodi ya ligi ni kwamba sababu iliyopelekea mechi kuahirishwa ni kufanya uchunguzi kwa matukio yaliyoletwa na afisa usalama je ni vipi kufanyika kwa mechi kungezuia huo uchunguzi kufanyika?
3) swali lako la tatu majibu yake yanafanana na ya pili, Yanga hawakukubaliana na maamuzi ya bodi ya ligi.
4) Kama uchunguzi unaweza kubatilisha mechi kuchezwa, mbona kuna matukio mengi yanayojitokeza viwanjani kabla ya mchezo au baada ya mchezo au wakati wa mchezo je lini tuliona mechi ikisitishwa kwaajili ya kupisha uchunguzi kama tu uchunguzu ni hoja nzito ya kufanya mechi isichezwe?