Huyu Jemedari Said ndio maana Yanga hawampendi, amenyooka sana

Utopolo mtupu
Huwezi nielewa kwa sabbu mmeshikiwa akili na watafuta hela waliyojifika usemaji.
Kwa akili yako ulishaona wapi CEO wa timu ya ligi akawa anazisema timu nyingine?
Ulishaona CEO wa Leicester anaisema vibaya Liverpool?

Halafu eti mnajiita mna akili, hizo akili au upepo?
 
Sababu za msingi? Uko timamu ww kichwani lakini?
 
Na ndio maana baada ya bodi ya ligi kuhairisha mechi, Yanga wao wakakomaa na bodi ya ligi kwa kitendo cha kuhairisha mechi bila sababu za msingi. Bodi ya ligi ndio imenunua kosa la Simba.
Kuhairisha ❌❌❌
Kuahirisha ✔✔✔
 
Kwa hiyo, kwenye mambo ya mpira shelia ni tofauti na za mahakama ya kawaida!!!
 
Zamalek wamezawadiwa mabao matatu hivyo ubao unasomeka zamaleck 3-0 Al ahly
 
Sasa kumbe viongozi wa Yanga wanadai points 3 zipi ikiwa wanajua walienda uwanjani mchezo ukiwa umefutwa na hakukuwa na ofisa yoyote yule wa mechi wala refarii
 
Bin Kazumari Mtipa ni mtu muhimu sana kwenye mpira wa nchi hii na ni bahati kama taifa kuwa na mtu makini na mwenye kujiamini kutoa maoni na kukosoa bila kujali ukubwa wa mtu au timu
Bin Kazumari amenyooka sana na ana mapenzi ya dhati na mpira wa nchi hii na sio timu kama ilivyo kwa wengne wengi
 
Sasa kumbe viongozi wa Yanga wanadai points 3 zipi ikiwa wanajua walienda uwanjani mchezo ukiwa umefutwa na hakukuwa na ofisa yoyote yule wa mechi wala refarii
Wameenda uwanjani kipinga kufutwa kwa mchezo na bodi ya ligi. Umeona nilichokiongea juu hapo kimekuja kutokea kama kilivyo katika ligi ya Misri kati ya Al Ahly na Zamalek. Al Ahly walitoa msimamo wao kuwa hawatocheza mechi dhidi ya Zamalek kwasababu mwamuzi hatoki nje ya nchi, lakini shirikisho lao na bodi yao ya ligi walivyo smart pamoja na ukubwa wa Al Ahly lakini hawakuitana kujadili kuhusu hilo bali wamekaa kimya na kuacha taratibu zote za mechi ziendelee kisha watatoa maamuzi kulingana na kanuni zao.

Zamalek kapewa point 3 na magoli 3 kisa Al Ahly kugoma mechi.
 
Ni watu wasio na maarifa na wasiojua taratibu na kanuni za mpira ndio watamuona Kazumari kanyooka kwenye tukio la mechi ya derby, na ndio maana alifeli mitihani ya FIFA.

Wewe, bodi ya ligi yako na huyo Bin Kazumari mkajifunze kufuata kanuni pasipo kuangalia ukubwa wa timu kupitia sakata la Al Ahly. Pamoja na Al Ahly kutoa msimamo wao wa kutocheza mechi na sababu wakaweka wazi lakini viongozi wanaosimamia mpira na ligi yao hukuona wakikutana kujadili bali wameacha sheria itaamua
 
Mechi ya Yanga Vs Simba imeghairishwa tarehe kwamaana hiyo bado haijachezwa sasa Yanga wanapataje points 3 za mezani

Mechi unayoitaja ya El Zamalek vs Al Ahly ni mechi halali na haikughairishwa na bodi yao ya ligi hivyo Zamalek wana haki zote za kupewa ushindi wao
Zamalek walifika uwanjani kukiwa na Officials wote wa mechi wakasubiri kwa dk 20 mpinzani wao hakutokea then wakawa awarded ushindi na magoli 3 kitu ambacho ni tofauti kabisa kwa Yanga

Yanga wamefika uwanjani wao wenyewe bila uwepo wa ofisa yoyote yule wa mchezo husika na bado wanataka wapewe points 3 hivi huo ni utaratibu wa wapi?
 
Sisi mechi yetu haijachezwa hiyo ya Misri imechezwa ndio maana kulikuwa na officials wote wa mechi husika
Sasa Yanga mnataka mpewe points 3 kwa kanuni gani?
Mmefika uwanjani bila uwepo wa mwamuzi yoyote na bado mnaona mnastahili kupewa points za mezani
 
Point yangu ni weledi katika vyama vinavyoongoza na kusimamia mpira wa miguu katika kusimamia katika kanuni bila kuangalia ukubwa wa timu. Je umeona chama cha soka cha Misri au bodi ya ligi ya Misri wakiteteleka kwa kukutana ili kujadiliana baada ya Al Ahly kuweka msimamo wao wa kugomea mechi? Hapo ndio uone tofauti kati ya chama kinachoondeshwa kwa uoga wa Simba na Yanga na chama kinachofuata misingi ya kanuni na sheria ya soka bila kujali ukubwa wa timu. Al Ahly ana historia kubwa katika soka Africa kuliko timu yeyote ile Africa ila hakuweza kutetelesha chama chao kuangaika kukaa vikao.
 
Na mimi point yangu ilikuwa Yanga wanadai points 3 kwa kanuni ipi?
Maana wameandika barua wakisema wanadai points zao 3 wanazostahili ambazo ni zipi hizo na za mchezo upi?
 
Na mimi point yangu ilikuwa Yanga wanadai points 3 kwa kanuni ipi?
Maana wameandika barua wakisema wanadai points zao 3 wanazostahili ambazo ni zipi hizo na za mchezo upi?
Wanadai point 3 kwasababu bodi ya ligi imefanya makosa kuahirisha mechi yao wakati hakuna kanuni inayoelekeza hivyo. Kesi ni Yanga vs bodi ya ligi
Ili bodi ya ligi ionekane ina uhalali wa kuiahirisha ile mechi inapaswa ioneshwe kanuni inayohalalisha kuwa timu ngeni ikinyimwa kufanya mazoezi ya mwisho basi inapaswa kugomea mechi.

Swali linarudi kwako, je walichofanya bodi ya ligi ni sahihi? Na ni sahihi kwa kipengele kipi kinachoruhusu mechi isichezwe kama timu ngeni isipofanya mazoezi ya mwisho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…