Huyu Kamanda wa Jeshi anatukera sana wakazi wa Mbezi

Naona kamuiga boss wake. Hawa wote wamekataa kukaa kambini kwenye nyumba za jeshi ili waje wafanye 'fujo' mitaani. Wabongo wanasema, raha ya pesa, uitumie kule wanapokujua... Hata mkuu wa majeshi anakaa Segerea... Kiukweli amesaidia kuipaisha Segerea sasa panaonekana pa kishua... Maana inaonekana hata vigogo wanakaa huko... Zamani haya mambo tuliyazoe kuyaona Masaki tu!
 
Wanasema mzee aligoma kuhamia huko ushuani Masaki,mpk barabara imetengenezwa fresh kabisa sababu ya mzee baba.Safi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani hakuna ulemvi mbaya kama wa cheo na madaraka kama mwenye navyo hana hekima na utu. Hawajui kuwa hivi vyeo ni vya muda tu na baada ya hapo tutakutana gengeni au ununio kwenye soko la samaki. Ni karaha kubwa mno na inaudhi kwa kweli. Waziri wake Mhe. Mwinyi hana hizo tabia, waambiwe waache kulewa madaraka hayo. Kuna watu wana nafasi kubwa kuliko yeye na majukumu nyeti kuliko yake lakini wana hekima na ustaarabu na wanakuwa kwenye foleni kama sisi waajiri wao. Atambue na kukubali kuwa hiyo ni dhamana tu na analipwa kwa kodi zetu sisi tunaotishiwa na kutukanwa barabarani. Ninaamini mamlaka husika zitalipokea hili na kumshauri au kumwelekeza huyo kiongozi kutotumia ofisi yake vibaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijeshi ni Luteni Jenerali (Lieutenant Geneal; 3-star General) just nyuma ya Mkuu wa Majeshi (Jenerali - 4-star General). Chief of Staff ni cheo cha utendaji ambacho anaweza akapewa kamanda mwingine yeyote mwenye cheo sawa cha kijeshi.
Tuna maluteni general wawili tu,kwahiyo tunaweza kumjua huyo hahhahhaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…