Huyu Lunyamila inaonekana enzi zake alikuwa moto wa kuotea mbali

Huyu Lunyamila inaonekana enzi zake alikuwa moto wa kuotea mbali

Lunyamila aliwaliza Sports club villa ya Uganda hawatakaa wamsahau
 
Edibily lunyamila,Alfred kategile,
marco john hawa walikuaga RTC shy kabla hawajashine simba na yanga
 
Waganda hawawezi kumsahau Lunyamila...Moja ya mawinga bora Afrika ishawahi kuwa nao...

Halafu kuna wakati alipata timu Ujerumani, lakini mechi ya Simba na Yanga ilimpotezea hiyo nafasi maana alitoroka huko ughaibuni kabla ya kusaini ili tu arudi kuichezea Yanga...
Natizama mechi ya maveterani hapa Azam tv, huyu Lunyamila yupo ubavu wa kushoto kwa namna anavyocheza inaonyesha ana akili sana na Fundi.

Sijui enzi zake alikuaje huyu veterani.
 
Naomba nizungumze yafuatayo. Nilikuwa kwenye kikosi cha kikapu cha kanda ya Mashariki kwenye michezo a UMISETA mwaka 1991/1992. Edibily Lunyamila alikuwa kwenye kikosi cha mpira wa miguu cha kanda ya Magharibi. Hii ndio ilikuwa mara kwanza kumuona. Tuilkuwa tunacheza michezo yetu (kikapu) nje ya uwanja wa Amaan. Baada ya mechi zetu, ukisikia kanda ya Magharibi wanacheza, tulikuwa lazima tuende kumuangalia. Kwa jinsi alivyokuwa machachari na jinsi alivyokuwa anacheza, sikuwa na shaka kuwa atakuwa miongoni wa wachezaji bora kabisa kutokea Tanzania. Haikupita muda tuliporudi Dar es salaam, nikamuona uwanja wa zamani wa Taifa anaingia na kwenda jukwaa la Yanga (baada ya kusajiliwa).
Mimi ni mpenzi wa kutupwa wa Simba SC. Nikajua tutapata matatizo sana nae tukikutana. Pamoja na ushabiki wangu wa Simba SC, hakuna mchezaji wa Yanga aliyekuwa ananikuna kama yeye. Nilikuwa tumbo joto wakati wa mechi za watani wa jadi kwa sababu yake. Mchuano na purukushani zake na Kasongo Athumani zilikuwa kabambe. Kasongo ilibidi atumie ubabe na nguvu nyingi kumzuia. Alikuwa na kasi, uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, na chenga. Angeweza kabisa kucheza mpira wa kulipwa zaidi ya kuchezea Yanga na baadae Simba. Ningependa sana nikutane nae siku moja nipate fursa ya kuongea nae.
 
Nilishiriki UMISETA Songea na Zanzibar. Kumbukumbu zinanitoka kidogo. Sina uhakika nilimuona Songea au Zanzibar. Umri umeshapita sana!!!
 
Nilishiriki UMISETA Songea na Zanzibar. Kumbukumbu zinanitoka kidogo. Sina uhakika nilimuona Songea au Zanzibar. Umri umeshapita sana!!!
Duh! Mlienjoy sana aiseee!! Nilikuwa Songea form one nilitamani niwe miongoni mwenu. Wachezaji kipindi kile mliishia kwenye umaarufu na kutoka na mademu wakali, """Msiniumizieeee""" nilitamani sana niwe mkubwa fasta nienjoy km nyie vile[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na medali, na makombe aliyochukua, na heshima ya miaka mia nane ijayo.
Lunya na mpira...
Acha wivu wa kipuuzi.
usipende kujipendekeza..! Kiazi mbatata wewe.. Naona unawashwa nitakutia cha kati bila ky mazafaka

Jr[emoji769]
 
Lunyamila ndo mchezaji bora tangu kuumbwa kwa Tanganyika(Tanzania)
 
Alikuwa na kipaji hasa, inasikitisha leo yupo hoi kimaisha....maisha kitendawili aisee.
 
Back
Top Bottom