Basi pilika pilika za kila Mara kwenda polisi, upelelezi na kuwafatilia wezi wale, kusafirisha na kuzika msiba wa mlinzi wangu.
Bas nikakosa utulivu kisaikolijia. Hivyo almost wiki 2 zote zile tukawa hatuwasiliani kabisa. Niko bize na ishu za zangu.
Baada ya kutulia nikaamua kumpigia Simu kumjulia hali,
Akaikata na kunitumia ujumbe.
"Yaan wee mwanaume unaroho mbaya Sana, umenikosesha ile fremu Sasa unanitafuta wa Nini Sasa"
Nikamwambia
" pokea sim kwanza tuongee kwanza"
Basi nikapiga akapokea nikamwambia
"Hivi Kwan mi na wee tuna ugomvi? Ni halali Unaleta habar za kuniomba Ela wkt unajua kabisa ndo nmetoka kuibiwa. Ulishindwa nn kunisubiri nitulize Akili ndo uniletee hizo habar zako?"
Akasema,
"Kwan hizi habar za frem sinilishakwambia mapema, hii ilkua Ni dharura mweyewe alkua na shida ?
Istoshe wee mwenyewe si ndo ulniambia MDA wowote nikipata fremu Ela iko tayar nikwambie?
Sasa kuibiwa kwako kunahusiana vipi na bajeti ya fremu langu maana mi najua tayar ilkua ndani ya bajeti yako na halihusiani kabisa na kuibiwa kwako.
Kuibiwa uliibiwa usiku wake, Ila iyo Ela bajeti yake ilkuepo benki MDA mrefu. Sasa nakuelewaje mimi"
Nikamwambia,
"Kwaiyo Mimi kuibiwa dukan kwangu haikuhusu sio? Hivi unajua kwamba Ela ya kula unayopewa kila siku inatoka hapo hapo dukan nilikoibiwa. Aisee Wee mwanamke Ni mbinafs na una roho mbaya Sana."
Akasema,
"Yaan mi kukwambia ukweli nishakua na roho mbaya? Basi sawa Kama nna roho mbaya niache ukatafte hao wenye roho nzuri. Kwani nmekung'ang'ania?"
Nikasema "sawa" Kisha nikakata Simu.
Na kiukweli nilimchukia Sana mwanamke Yule, na kukubaliana kiroho Safi na uamuz wake wa TUACHANE.
Tulikaa almost wiki hatuna mawasiliano, siku moja Sina hili Wala Lile ikaingia namba mpya inapiga.
Nikapokea na kuuliza "Nani"
Akasema "mimi rose, shemej ako kwa Jacky nilikua nakusalimia"
Nikasema,
"sawa, chuo unaendeleaje uko?"
Akasema
"naendelea vizur, msimu wa test huu ndo zimetubana ndo maana sijaja uko kuwaona. nilikua nakusalimu shem angu na pole sana nakuibiwa dukani, dada alnambia"
Nikasema,
"Asante Nishapoa, kawaida tu Iyo ni mitihani ya dunia."
Akasema,
"Aya pole, mi nilikua nakusalimu"
Basi tukaagana, akakata simu ikawa imeisha ivyo.
Baada hapo ikawa kila Mara mdogo wake ananitumia sms zakunijulia Hali, nyingine nazijibu, nyingine nazipotezea TU sababu ya ubize na kutokujali Sana.
Siku moja kanipigia akiniomba nimsaidie ela kidg akanunue dawa,
Nikamuuliza "kwani unaumwa Nini?"
Akasema, "tumbo"
Nikauliza "kwani linaumaje?"
Akasema "hapa chini ya kitovu"
Basi kwa Akili ya kawaida nikajua uyu atakua kaingia blidi, anataka Ela ya pedi
Nikamjibu "Kwann usimwambie dada ako mbona, Hilo naona liko ndani ya uwezo wa dada ako, SI umwambie TU akusaidie. Au unamuogopa?"
Akasema,
"Hamna shemej, nmeshaogea na dada yee ndo kasema nikwambie wewe. Yeye hana Ela kabisa. Kasimamishwa kazi wiki ilopita."
Nikamuuliza,
"Kwani ulkua unahitaj Kia's gan?"
Akasema "elfu 50"
Basi Pale pale nikamfanyia muamala wa elfu 50 NMB-TiGO PESA
Akanitaarifu na kunishukru.
Kesho yake nikaona kanichek wasap na kanipigia picha ya daftar la vipimo na dawa alizoandikiwa wasap.
Nikagundua kumbe alkua anasumbua U.T.I na sio blidi Kama nilivowaza mwanzo. Basi ikawa imeisha ivo.
Inaendelea....