Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Clatous Chotas Chama. Jamani huyu mchezaji ni muongo, ni muongo sijapata kuona. Muongo sana. Na uongo ni dhambi ambayo katika amri kumi ipo. Usiseme Uongo.
.
Chama anaweza kukudanganya kuwa anaenda mbele kumbe haendi. Anarudi nyuma. Anaweza kukudanganya kuwa anapiga kumbe hapigi. Anaweza kukudanganya anataka kufunga kumbe anatoa pass afunge mwingine.
Ni muongo. Jamaa yangu siku moja alikuwa anaangalia mpira anamwangalia Chama. Akasema kumbe kucheza mpira ni jambo rahjsi sana. Nikamuuliza kwa nini. Akasema mwangalie Chama anavyocheza. Hamna ugumu. Nikamwambia huyu jamaa usimwamini hata kidogo. Ni mwongo sana. Akabisha.
Nikaja mwonesha anavyocheza Aziz Ki. Akakubali akasema kama unataka jifunza kucheza mpira Chama siyo mwalimu mzuri. Atakudanganya....anaufanya mpira kuwa ni jambo jepesi sana. Ukimuangalia Aziz Ki unagundua mpira si jambo jepesi kama anavyoonesha Chama.
Chama bishoo....anacheza Dont Touch me. Tucheze mpira. Anatema kushoto anafukia kulia. Anaenda mbele hatua tatu anarudi nyuma moja. Jamaa huwez mwelewa. Anatizama kulia anapita kushoto.
.
Jamaa mwili unaenda kushoto miguu inaenda kulia. Yaani si mchezaji wa kumwamini. Ni muongo tu. Hana lolote. Mchezaji anakuwa muongo mpaka basi. Si mfano wa kuiga kwa wachezaji chipukizi. Anawadanganya wataona mpira ni jambo jepesi kumbe si kweli.
Chama hawezi kwenda Mbinguni kama asipoacha huu uchezaji wake. Hawezi. Mi nawaambia kabisa. Sababu ni muongo.