Huyu mdogo wangu yupo form four, oneni anavyoandika

Huyu mdogo wangu yupo form four, oneni anavyoandika

Me huyu kesha maliza form 4 ni vile ni mdogo Wangu, lakini MTU mwenye uandishi wa Aina hi huwa simzingatii

Nafikiri kuna tatizo kubwa
Screenshot_20240606-093712~4.png
 
Me huyu kesha maliza form 4 ni vile ni mdogo Wangu, lakini MTU mwenye uandishi wa Aina hi huwa simzingatii

Nafikiri kuna tatizo kubwa
View attachment 3009880
Mabadiliko yanaanza na wewe na watu walio karibu yako,unaposema unamzingatia huyo kwavile ni mdogo wako ila wengine huwazingatii inakua still bado unasapoti huo uandishi,

Anza kumbadilisha huyo mdogo wako kisha nae atabadili wenzake.
 
Changamoto kubwa inayopelekea haya yote kuwepo ni kukipuuza Kiswahili.

Watoto wanajifunza kiswahili sanifu kwanzia kidato cha kwanza wakiwa tayari wamekomaa kwenye Kiswahili cha hovyo kinachozungumzwa mitaani kwasababu hawakufundishwa vyema kiswahili sanifu wakiwa shule ya msingi ambako mazingira ni rafiki kujifunza na kukiendeleza Kiswahili kwasababu lugha ya kufundishia na mawasiliano ni Kiswahili.

Wanapoanza kujifunza Kiswahili sanifu kidato cha kwanza, wanakutana na masomo magumu wasiyoyaelewa tena yakifundishwa kwa lugha wasiyoielewa, nguvu yao kubwa huielekeza huko kwenye hayo masomo na hatimae Kiswahili wanasoma kwa nguvu ndogo sana wakijipanga kujibu mtihani tu nasio kuielewa vizuri lugha husika.

Hata ufatiliaje kwa lugha husika ni mdogo sana na umejikita kwenye kufatilia mitihani nasio kufatilia ukomavu wa lugha husika kwa watoto kwenye nyanja mbalimbali kama mawasiliano na uandishi.

Hatimae huyu kijana anafika chuo hawezi kutofautisha herufi, matamshi na mengineyo yanayohusu Kiswahili.

Maoni yangu Kiswahili sanifu kianze kufundishwa kwanzia darasa la tatu tena kwa mkazo mkubwa ili mtoto apate muda wa kutosha kukiishi Kiswahili sanifu kwasababu sekondari mazingira si rafiki kujifunza na kukiendeleza Kiswahili, mawasiliano na mambo mengine yanaendeshwa kwa lugha ya kingereza kwa takribani 70%.
 
Usimjaji kuandika hivyo, kaandika kutokana na mazoea aliyonayo kwako, kama vipi usingemfanaya akuzoee.
 
Mabadiliko yanaanza na wewe na watu walio karibu yako,unaposema unamzingatia huyo kwavile ni mdogo wako ila wengine huwazingatii inakua still bado unasapoti huo uandishi,

Anza kumbadilisha huyo mdogo wako kisha nae atabadili wenzake.
🙏🙏 Mkuu kwa ushauri mzuri ngojea nianze kuchukua hatua
 
Hatari sana.
Non sense teachers.
Na huyo dogo mwakani Form 5 ataingia
Usiwalaumu waalimu.Hakuna mwl. anayefundisha hayo kamwe. Ni ujinga wa mwanafunzi mwenyewe. Anadhani anamwandikia rafiki yake wa kaliba yake.
Hana adabu na heshima kwako.
 
Wanabagaza lugha ya kiswahili. Itabidi tuwashtaki kwa profesa Kabudi.
Wanalazimisha matumizi ya x kwa vile tu kwenye kiswahili hakuna x, 😲
 
Hatari sana.
Non sense teachers.
Na huyo dogo mwakani Form 5 ataingia
Kiongozi kwani huo ujumbe kaandika mwalimu? Hii "non sense teachers" ndio nini? "Non sense" hii gap nani ajaze au mwalimu wako nae lugha za mataifa zilikuwa shida.Wapumuzisheni walimu asee hii shida ya mtoto na jamaa yake haina link na mwalimu au shule anakosomea
 
Xaxa xi umjb kk? Ha ha ha ha ha ha
Mkuu, kiukweli huo ni uandishi wa kipang'ang'a sana. Yeyote akiniandikia hivyo, huwa simjibu.
usipomjibu maana yake hujakamilisha maana ya Communication

Communication is a two way process..

sawa umpigie mtu simu apokee halafu asiongee!
 
Back
Top Bottom