Huyu mdogo wangu yupo form four, oneni anavyoandika

Huyu mdogo wangu yupo form four, oneni anavyoandika

Kuna mtu yupo chuo,chuo kikuuu cha Dar es salaam,na anaandika pumba kama hizo,huwa najiuliza chuo kikuu kafikaje?
 
Tumeshachoka kuamua ugomvi JF juzi kuna mmoja kamtia mwenzake vidole sehemu mbaya sana we imagine anamuingiza mwenzake kidole jichoni
Daah nilifikiri kafika makunduchi huko kwa mchamba wima
 
Angekuwa wakike nngemuelewa kutokana na kuwa kwenye umri wa upuuzi mwingi, ila kwa kuwa n mwanaume aisee nimechoka 🗑️
 
Mimi akiniandikia Hivyo Huwa sijibu chochote.nampuuza.
 
Wahariri wetu wa Habari, Tamthilia na Vitabu wajao.
 
Muandikie msg mwambie marufuku kumtumia msg zenye xxxxxx Kama hawezi kuandika vzr apige vinginevyo atajilaumu
Mimi niliwahi kukomesha hiyo tabia kwa wadogo zangu wote. Akiandika tu hivyo sijibu akipiga anauliza kama nimeona text namwambia nimeona lakini sielewi.

Halafu namuambia kama huwezi kuniandikia kiswahili au kiingereza tafadhali naomba usiniandikia kitu kingine.

Walinyooka mpaka leo hii hamna huo ujinga.
 
Dog kanzngua kinym xi unajua ten watot mxameh 2
Kuna boda wangu akikuta missed call huwa ananiandikia 'PG' akimaanisha Piga.

Mimi huwa nikiliona hilo neno haraka akili inanikumbusha PG Clamps au Parental Guidance.
 
Huo uandishi unatia kinyaa sana, sijui fasheni gani hii nayo....
Utoto tu. Nadhani huu uandishi ulichochewa na hizi simu za button keypad miaka ya nyuma kidogo.

Unakuta herufi tatu au nne zipo kwenye button moja kwenye keypad ya simu. Sasa ile ku type moja usubiri sekunde mbili utafute nyingine ndio watu wakabuni njia rahisi ya kutype haraka kwa ku skip na ku substitute baadhi ya herufi katika maneno ndio hiyo sasa ime evolve hivyo hivyo mpaka enzi hizi za smartphone zenye full keyboard.
images (8).jpeg
 
Back
Top Bottom