Huyu mdogo wangu yupo form four, oneni anavyoandika

Huyu mdogo wangu yupo form four, oneni anavyoandika

Apa kweli.......kizazi hiki kimeshindikana na huenda mpka kwenye mikataba wanasaini ivoivo , mwisho wa siku nchi imeuzwa
 
Walimu tuna taabu hii nchi🙆🙆🙆
Sasa hapo walimu wanahusikaje? Madaftari yake umekagua ukakuta kaandika huo upuuzi?
Ndio nimekagua nikakuta umemsahishia mtihani wake wa kiswahil kapata 90 halafu ukamwandikia "vixureee" badala ya vizuri 😂
 
Kuna siku nachati na wife tukamalizana nikamwambia badae akajibu 'P'. nikamuuliza p ndo nini? hajarudiaga tena huo upuuzi.
 
Siyo wanafunzi tu ingawa kwao ndiyo imekithiri. Wasichana wengi wanaojitia ujuaji huu ndiyo mwandiko wao. Unakuta una mtu ktk mahusiano ya kimapenzi lakini akikutumia SMS hadi unashangaa km wakati unamtongoza ulikuwa umelewa au ulipotea tu njia. Vibinti vingi vinaandika hovyo sana kuanzia vya sekondari hadi vyuo.

Huyo mbutue kabisa, yani anakuomba pesa za tuition kana kwamba anamuomba mpenzi/mshikaji wake. Kwa mwandiko huo tuition hiyo anaenda kuongeza ujinga. Ndiyo maan vinafeli mitihani maan mazoea hujenga tabia, siyo ajabu hata kwenye mtihani akaandika ujinga huo. Pole sn, hasara hiyo ktk familia.
 
Walimu wanawafundisha vizuri tu hao watoto
Tatizo wanaona kuandika maandishi ya kipuuzi ndio ujanja
Hiyo ni fashion
Ni upuuzi mumy!

Wanatakiwa wajue wanawasiliana na nani,,wao hawatofautishi mchizi wake na kaka yake,au wanashindwa kujua rika fulani niwasiliane nao vipi na rika fulani niwasiliane nao vipi
 
Kawaida ni utoto tu
Wengi tulikuwa hivyo mpaka form 5 na 6 nakumbuka
 
Back
Top Bottom