Changamoto kubwa inayopelekea haya yote kuwepo ni kukipuuza Kiswahili.
Watoto wanajifunza kiswahili sanifu kwanzia kidato cha kwanza wakiwa tayari wamekomaa kwenye Kiswahili cha hovyo kinachozungumzwa mitaani kwasababu hawakufundishwa vyema kiswahili sanifu wakiwa shule ya msingi ambako mazingira ni rafiki kujifunza na kukiendeleza Kiswahili kwasababu lugha ya kufundishia na mawasiliano ni Kiswahili.
Wanapoanza kujifunza Kiswahili sanifu kidato cha kwanza, wanakutana na masomo magumu wasiyoyaelewa tena yakifundishwa kwa lugha wasiyoielewa, nguvu yao kubwa huielekeza huko kwenye hayo masomo na hatimae Kiswahili wanasoma kwa nguvu ndogo sana wakijipanga kujibu mtihani tu nasio kuielewa vizuri lugha husika.
Hata ufatiliaje kwa lugha husika ni mdogo sana na umejikita kwenye kufatilia mitihani nasio kufatilia ukomavu wa lugha husika kwa watoto kwenye nyanja mbalimbali kama mawasiliano na uandishi.
Hatimae huyu kijana anafika chuo hawezi kutofautisha herufi, matamshi na mengineyo yanayohusu Kiswahili.
Maoni yangu Kiswahili sanifu kianze kufundishwa kwanzia darasa la tatu tena kwa mkazo mkubwa ili mtoto apate muda wa kutosha kukiishi Kiswahili sanifu kwasababu sekondari mazingira si rafiki kujifunza na kukiendeleza Kiswahili, mawasiliano na mambo mengine yanaendeshwa kwa lugha ya kingereza kwa takribani 70%.