Huyu mjasiramali "Sirjeff" anapewa mashitaka ya uhujumu uchumi siku chache tu baada ya kuanza kampeni ya No reforms No election!

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
12,505
Reaction score
40,002
Vijana wa umri wa 30s ambao wanajipambanua kiuchumi kwa ujasiriamali then from No where wanapewa kesi za uhujumu uchumi.

Hivi hili rika letu lina nini cha kuhujumu nchi? Kijana ndo kwanza unajitafuta kimaisha ila kutokana na mambo tu ya kisiasa mmetofautiana unatafuta kesi popote pale ili mradi tu kurudishana kwenye ufukara na kupoteza kabisa malengo ya watu.

Nakumbuka pia enzi za jiwe kuna vijana wengine Tito Magoti na mwenzake walikamatwa wakiwa kwenye boda boda wanaenda kununua Tecno Makumbusho ghafla wanawekwa chini ya ulinzi na kushtakiwa eti ni wahujumu uchumi wakati kwenye akaunti zao hata laki tano walikuwa hawana. Hatimaye wakapotezewa malengo kimaisha na leo wameishia kuwa wakimbizi wa kisiasa.

Haya mambo ya kushtaki vijana kwa makesi makubwa makubwa kisa tu mambo ya siasa kusema kweli hayaja kaa vizuri. Hivi kuna mtanzania ambao siyo mhujumu uchumi? Maana hata kukojoa hadharani au mafichoni eneo lisilo sahihi ni uhujumu uchumi. Kuendesha boda boda sehemu isiyo sahihi ni uhujumu uchumi. Kimsingi wengi wanasaidiwa na ama kukaa tu kimya au uchawa.

Kijana anauza zake mbao huko Mafinga na kucheza forex leo utashangaa atashtakiwa kwa kukausha misitu na kutakatisha fedha kisa tu kaandika No reforms No election? How? Tunajenga nchi ya aina gani kwa kizazi hiki?
 
Huyo unaemtetea inaweza kuws humjui vizuri
Basi angekuwa chawa kama ni mbaya au angekaa kimya. Mbona siku zote alikuwa anajiweka wazi?
 
Itakuwa alikuwa anatafuta huruma ya wananchi kwa kusema no reform no election
 
Vijana wa umri wa 30s ambao wanajipambanua kiuchumi kwa ujasiriamali then from No where wanapewa kesi za uhujumu uchumi.

Hivi hili rika letu lina nini cha kuhujumu nchi? Kijana ndo kwanza unajitafuta kimaisha ila kutokana na mambo tu ya kisiasa mmetofautiana unatafuta kesi popote pale ili mradi tu kurudishana kwenye ufukara na kupoteza kabisa malengo ya watu.

Nakumbuka pia enzi za jiwe kuna vijana wengine Tito Magoti na mwenzake walikamatwa wakiwa kwenye boda boda wanaenda kununua Tecno Makumbusho ghafla wanawekwa chini ya ulinzi na kushtakiwa eti ni wahujumu uchumi wakati kwenye akaunti zao hata laki tano walikuwa hawana. Hatimaye wakapotezewa malengo kimaisha na leo wameishia kuwa wakimbizi wa kisiasa.

Haya mambo ya kushtaki vijana kwa makesi makubwa makubwa kisa tu mambo ya siasa kusema kweli hayaja kaa vizuri. Hivi kuna mtanzania ambao siyo mhujumu uchumi? Maana hata kukojoa hadharani au mafichoni eneo lisilo sahihi ni uhujumu uchumi. Kuendesha boda boda sehemu isiyo sahihi ni uhujumu uchumi. Kimsingi wengi wanasaidiwa na ama kukaa tu kimya au uchawa.

Kijana anauza zake mbao huko Mafinga na kucheza forex leo utashangaa atashtakiwa kwa kukausha misitu na kutakatisha fedha kisa tu kaandika No reforms No election? How? Tunajenga nchi ya aina gani kwa kizazi hiki?
Chanzo cha habari please! Acha umbeya!
 
Mkuu Marekebisho kidogo hapo Forex haichezwi ni Taaluma kabisa
Kwenye mada husika sasa
Yawezekana waliopo kwenye madaraka wamepoteza utu wanachojali wao ni maslahi yao yatimie
 
Alikua anaona anakaribia kudakwq akaanza kuposti no reform No election Ili apate huruma ya wananchi

..basi huyo ni mjinga.

..alitakiwa ajifanye chawa.

..yeyote mwenye mazongezonge akijiunga na nrne amelenga kukamatwa na polisi.
 
Back
Top Bottom