Huyu mjasiramali "Sirjeff" anapewa mashitaka ya uhujumu uchumi siku chache tu baada ya kuanza kampeni ya No reforms No election!

Huyu mjasiramali "Sirjeff" anapewa mashitaka ya uhujumu uchumi siku chache tu baada ya kuanza kampeni ya No reforms No election!

No Reforms ni mwiba mkali kwa CCM. Mwaka huu watajichagua wenyewe.
 
Vijana wa umri wa 30s ambao wanajipambanua kiuchumi kwa ujasiriamali then from No where wanapewa kesi za uhujumu uchumi.

Hivi hili rika letu lina nini cha kuhujumu nchi? Kijana ndo kwanza unajitafuta kimaisha ila kutokana na mambo tu ya kisiasa mmetofautiana unatafuta kesi popote pale ili mradi tu kurudishana kwenye ufukara na kupoteza kabisa malengo ya watu.

Nakumbuka pia enzi za jiwe kuna vijana wengine Tito Magoti na mwenzake walikamatwa wakiwa kwenye boda boda wanaenda kununua Tecno Makumbusho ghafla wanawekwa chini ya ulinzi na kushtakiwa eti ni wahujumu uchumi wakati kwenye akaunti zao hata laki tano walikuwa hawana. Hatimaye wakapotezewa malengo kimaisha na leo wameishia kuwa wakimbizi wa kisiasa.

Haya mambo ya kushtaki vijana kwa makesi makubwa makubwa kisa tu mambo ya siasa kusema kweli hayaja kaa vizuri. Hivi kuna mtanzania ambao siyo mhujumu uchumi? Maana hata kukojoa hadharani au mafichoni eneo lisilo sahihi ni uhujumu uchumi. Kuendesha boda boda sehemu isiyo sahihi ni uhujumu uchumi. Kimsingi wengi wanasaidiwa na ama kukaa tu kimya au uchawa.

Kijana anauza zake mbao huko Mafinga na kucheza forex leo utashangaa atashtakiwa kwa kukausha misitu na kutakatisha fedha kisa tu kaandika No reforms No election? How? Tunajenga nchi ya aina gani kwa kizazi hiki?
Wangapi wanaandika kuhusu NRNE? Na hawakamatwi

Martin wa CHADEMA anaandika karibu kila siku, ila lini alikamatwa kwa ajili ya kuandika hivyo?
kuna wale watoto sijui vijana akina Nguti na Msuya ambao wanaendaga Nairobi wanaandika kila siku ila hawajawahi kukamatwa.

Huyo Sirjeff kaandika NRNE mara ngapi kwenye akaunti yake ya Twitter mpaka ifikie hatua amakamatwa kwa ajili ya kuandika hivyo? yawezekana hata mara 10 haijafika na anaweza asifike hata robo ya namna MMartin anaandika
 
Aliowachomesha enzi za Jangid Plaza wanasema Karma is real.😁.
 
Back
Top Bottom