The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Mwanangu, kituko ni kituko bila kujali imani ujue.Kumwona mwenzako kituko kwenye mambo ya imani hiyo sio sawa. Ndio maana tumetofautiana, u
Mwanangu, kituko ni kituko bila kujali imani ujue.Kumwona mwenzako kituko kwenye mambo ya imani hiyo sio sawa. Ndio maana tumetofautiana, u
Amen kubwa.Sifa kwa Yesu! Haleluya!
Sifa stahiki kwa Father of All mwanangu. Yesu mwenyewe yuko wapi?Amen kubwa.
Labda , kurudi nyumbani saa 12.Kumwona mwenzako kituko kwenye mambo ya imani, hiyo sio sawa. Ndio maana tumetofautiana, unataka wote tuwe-wezi kama wewe.
1 Petro 3:7Yote umeenda SAWA ila hapo pa kupiga mke sijakuelewa hao bila kipigo utakufa kwa stress
Baba wa wote ni yupi? Maana YESU mwenyewe anasema mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi!Sifa stahiki kwa Father of All mwanangu. Yesu mwenyewe yuko wapi?
Baba wa wote ni mimi mwenyewe bingwa wa kufungua akili za watu walioingizwa kwenye utumwa wa kiroho na kisiasa hadi wanaitwa kondoo na wengine chawa.Baba wa wote ni yupi? Maana YESU mwenyewe anasema mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi!
Hebu fafanua vizuri nipate iyo concept.Mwanangu, kituko ni kituko bila kujali imani ujue.
Wewe mwenyewe bakora zinakusubilia usipo badilikaBaba wa wote ni mimi mwenyewe bingwa wa kufungua akili za watu walioingizwa kwenye utumwa wa kiroho na kisiasa hadi wanaitwa kondoo na wengine chawa.
Are you serious? Nani anichape aone kilichomzuia kuku kukojoa?Wewe mwenyewe bakora zinakusubilia usipo badilika
Kupanga ni kuchagua. As long as anaishi wewe inakuuma nini sasa.Huyu Mlokole kweli ana matatizo! Tufanyeje tuondoe ujinga wake?
😂😂😂 Huyu mlokole ni mjinga au ndiye mwenye hekima? 🔥🔥
- Akiishiwa, hakubali kupokea rushwa ili apate utajiri wa haraka. Anaamini eti baraka zinatoka kwa Mungu, si kwa njia za mkato! Huyu mtu hafai dunia hii!
- Hajawahi kusema maneno machafu wala matusi. Eti kinywa chake ni kwa ajili ya kumtukuza Mungu, si kwa kulaani watu! Wengine "wanamwaga sera" kwa lugha kali, lakini yeye eti anasema "maneno ya neema"!
- Ameamua kuishi maisha ya uaminifu kazini kwake hata kama atabaki maskini. Eti anasema heri apate kidogo kwa haki kuliko utajiri wa dhuluma! Weh, kweli huyu hajielewi!
- Anawaheshimu viongozi wa serikali na kuwaombea badala ya kuwakashifu. Eti anasema Biblia imeagiza kuwaombea wenye mamlaka na kuwaheshimu! Huyu jamaa zimefyatuka?
- Anaishi kwa furaha hata kama hana vitu vya kifahari. Eti anasema "furaha ya Bwana ndiyo nguvu yake." Ana kigari kidogo na hata nyumba hajajenga lakini anacheka tu! Mjinga kweli!
- Hataki kutumia "mchezo mchafu" ili apate zabuni au kandarasi. Eti anasema anategemea Mungu amfungulie milango! Hajui duniani ni “toa kitu kidogo” ili mambo yaende?
- Anaweza kumsaidia mtu bila kutegemea malipo au shukrani. Eti anasema anafanya mema kama kwa Bwana, si kwa wanadamu! Hajui watu wa siku hizi hutoa msaada kwa masharti?
- Hapendi kujionyesha wala kuwaringishia watu mali zake. Eti anasema majivuno ni ya dunia na hayampendezi Mungu! Sasa utajulikanaje una mali kama hujioneshi mitandaoni?
- Akipewa pesa ampelekee mtu, hata kama ni nyingi, atazilinda na kumpelekea kama zilivyo. Eti anasema uaminifu ni bora kuliko dhahabu! Hajui siku hizi watu wanaita pesa ya mtu “mali ya bure”?
- Akisikia jirani yake ana shida, anaenda kumsaidia hata bila kuitwa. Eti anasema "Mpende jirani yako kama nafsi yako" Dunia ya sasa ni “kila mtu na maisha yake”
- Anawapenda hata wale wanaomchukia na kumdhihaki. Eti anasema "Mpende adui yako, umwombee." Yaani mtu anakudhalilisha, badala ya kumlima kibao, unamwombea?
Pole, mkuu. Kuna mahali nimesema wana JF wamepotoka? Unaweza ku-quote hiyo kauli? Nitai-edit nifute kauli hiyo.unatuona Wana JF kama watu walioopotoka
Tumekushtukia unatumia CHATGPTPole, mkuu. Kuna mahali nimesema wana JF wamepotoka? Unaweza ku-quote hiyo kauli? Nitai-edit nifute kauli hiyo.
Ila kama uzi huu umekufanya ujisikie hatia, dawa ya kuwa na dhamiri safi ni kutubu dhambi, kumwamini Yesu na kumpokea moyoni mwako. Ukifanya hivyo atakuwezesha kuishi maisha matakatifu yasiyo na hatia.
Omba (kwa kufuatisha kwa moyo wako wa dhati) sala hii ya toba, utaokoka sasa hivi na kujisikia amani.
“Ee Mungu Baba, nimetambua mimi ni mwenye dhambi. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen.”
Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Hutasikia tena hatia ya dhambi, maana Mungu amekusamehe. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuishi maisha matakatifu. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu, ujiunge nalo, watakuelekeza zaidi jinsi unavyopaswa kuenenda katika dunia hii. Ubarikiwe sana ndugu yangu.
Mkuu, uko nyuma ya wakati. Tangu lini ulisikia Youtube server zimejaa? Watu wana-post kila siku videos zenye MBs/GBs kibao, lakini servers hazijai. Hizi "text only threads" ndio zitajaza server?Mnajaza bure server za jf
Wow, kumbe chatGPT inaweza kuhubiri Injili? Ah, basi itanipunguzia kazi, na unabii huu utatimia haraka.Tumekushtukia unatumia CHATGPT
Akili na kibano vinaenda sambamba kwa kawaida akili ya binadamu hubadilika kutokana na mazingira1 Petro 3:7
Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; maana wao pia ni warithi wa neema ya uzima, ili maombi yenu yasizuiliwe na chochote.
Badala ya kutumia ngumi ku-solve matatizo ya ndoa, tumia akili.