Comrade si bora wewe una usingizi, mimi macho makavu😂
Duh inaonekana Unapenda sana udaku umefungua uzi haraka kutaka kujua huo ujinga alofanya juma lokole ni upi😁😁😁
Hahaha comrade uka surrender, mimi niko hivi kila siku😁Comrade jana nilikuwa na usingizi usio wa mchezo
Heri wewe macho yalikuwa makavu 🤣
Swala la wizi hata lisinge kuwa kwe ye biblia au vitanu vya dini still lingejulikana kama ni jambo baya tu, haiitaji hata ahadi ya mbingu ndk uaache😂😂😂 Kama maisha hayo ndio ujinga, basi heri niitwe mjinga x 100000000000000 🔥🔥
- Huyu mlokole anafanya kazi ya uhasibu kwenye shirika kubwa, lakini hajawahi kuiba hata senti. Eti anasema wezi hawataingia mbinguni. Mtu ana nafasi ya kutajirika haraka kwa pesa za shirika, yeye anakomalia uaminifu. Ujinga mtupu!
- Akipanda magari ya abiria, akizidishiwa chenji, anamrudishia konda pesa iliyozidi. Kweli huyu mtu hana akili! Wengine wangetumia nafasi hiyo kufurahia "baraka za ghafla," lakini yeye anang'ang'ana na uaminifu.
- Ukikutana naye, anajisifia eti hajawahi kuugua kisonono wala kaswende. Hayo magonjwa ndiyo "stori za mjini"! Eti yeye anajivunia maisha ya usafi. Mjinga sana huyu!
- Akikosewa au mtu akimtukana, hajibu matusi wala kupigana. Anaamini eti "kisasi atalipa Bwana," badala ya kujitetea kwa ngumi kama mwanaume. Ujinga mtupu!
- Huyu mlokole tangu aoe hajawahi kumpiga mke wake. Mke akimkosea, anamsamehe badala ya kumpiga na kumfundisha "adabu." Hii kweli siyo mental illness?
- Hawezi kusema uongo hata kidogo, hata kama uongo unamsaidia kukwepa matatizo. Eti anasema waongo watatupwa motoni. Huyu amewehuka!
- Akipata mshahara wake, anatoa fungu la kumi na kuwasaidia maskini. Jamani, badala ya kujilimbikizia mali yake, anawaza kusaidia wengine! Kweli huyu hana akili.
- Ana watoto wazuri, eti anawalea kwa maadili ya Kikristo badala ya kuwaacha "waende na wakati." Anawazuia wasitazame picha chafu kwenye mitandao, eti Mungu hapendi. Huyu mtu amepitwa na wakati!
Hahaha comrade uka surrender, mimi niko hivi kila siku😁
Mimi sijawahi kumwona mlokole hai hapa JF.Pole, mkuu. Kuna mahali nimesema wana JF wamepotoka? Unaweza ku-quote hiyo kauli? Nitai-edit nifute kauli hiyo.
Ila kama uzi huu umekufanya ujisikie hatia, dawa ya kuwa na dhamiri safi ni kutubu dhambi, kumwamini Yesu na kumpokea moyoni mwako. Ukifanya hivyo atakuwezesha kuishi maisha matakatifu yasiyo na hatia.
Omba (kwa kufuatisha kwa moyo wako wa dhati) sala hii ya toba, utaokoka sasa hivi na kujisikia amani.
“Ee Mungu Baba, nimetambua mimi ni mwenye dhambi. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen.”
Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Hutasikia tena hatia ya dhambi, maana Mungu amekusamehe. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuishi maisha matakatifu. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu, ujiunge nalo, watakuelekeza zaidi jinsi unavyopaswa kuenenda katika dunia hii. Ubarikiwe sana ndugu yangu.
huo usingizi nautamani Sana, ila hata niki upata bado routine yangu ita leta jeuri 😂.Kuna mimi ambaye ukiona nakesha ujue mchana nimelala sana 😂😂
Mie nina usingizi kila muda hadi kuna muda najishangaa 🤣
unafikiri kila alitajae jina la YESU ataokoka!Soma Biblia kwa muktadha. Kama hakuna mwandamu mkamilifi, umafikiri Yesu atakuja kuwanyakua waliopotoka?
Unahubiri kishetanishetani. Kuna wajinga wenzio wanaweza wasikuelewe. Hongera kwa walokole wazuinzi.Huyu Mlokole kweli ana matatizo! Tufanyeje tuondoe ujinga wake?
😂😂😂 Huyu mlokole ni mjinga au ndiye mwenye hekima? 🔥🔥
- Akiishiwa, hakubali kupokea rushwa ili apate utajiri wa haraka. Anaamini eti baraka zinatoka kwa Mungu, si kwa njia za mkato! Huyu mtu hafai dunia hii!
- Hajawahi kusema maneno machafu wala matusi. Eti kinywa chake ni kwa ajili ya kumtukuza Mungu, si kwa kulaani watu! Wengine "wanamwaga sera" kwa lugha kali, lakini yeye eti anasema "maneno ya neema"!
- Ameamua kuishi maisha ya uaminifu kazini kwake hata kama atabaki maskini. Eti anasema heri apate kidogo kwa haki kuliko utajiri wa dhuluma! Weh, kweli huyu hajielewi!
- Anawaheshimu viongozi wa serikali na kuwaombea badala ya kuwakashifu. Eti anasema Biblia imeagiza kuwaombea wenye mamlaka na kuwaheshimu! Huyu jamaa zimefyatuka?
- Anaishi kwa furaha hata kama hana vitu vya kifahari. Eti anasema "furaha ya Bwana ndiyo nguvu yake." Ana kigari kidogo na hata nyumba hajajenga lakini anacheka tu! Mjinga kweli!
- Hataki kutumia "mchezo mchafu" ili apate zabuni au kandarasi. Eti anasema anategemea Mungu amfungulie milango! Hajui duniani ni “toa kitu kidogo” ili mambo yaende?
- Anaweza kumsaidia mtu bila kutegemea malipo au shukrani. Eti anasema anafanya mema kama kwa Bwana, si kwa wanadamu! Hajui watu wa siku hizi hutoa msaada kwa masharti?
- Hapendi kujionyesha wala kuwaringishia watu mali zake. Eti anasema majivuno ni ya dunia na hayampendezi Mungu! Sasa utajulikanaje una mali kama hujioneshi mitandaoni?
- Akipewa pesa ampelekee mtu, hata kama ni nyingi, atazilinda na kumpelekea kama zilivyo. Eti anasema uaminifu ni bora kuliko dhahabu! Hajui siku hizi watu wanaita pesa ya mtu “mali ya bure”?
- Akisikia jirani yake ana shida, anaenda kumsaidia hata bila kuitwa. Eti anasema "Mpende jirani yako kama nafsi yako" Dunia ya sasa ni “kila mtu na maisha yake”
- Anawapenda hata wale wanaomchukia na kumdhihaki. Eti anasema "Mpende adui yako, umwombee." Yaani mtu anakudhalilisha, badala ya kumlima kibao, unamwombea?
Hii hadithi za Abunuwasi waandikie watoto😂😂😂 Kama maisha hayo ndio ujinga, basi heri niitwe mjinga x 100000000000000 🔥🔥
- Huyu mlokole anafanya kazi ya uhasibu kwenye shirika kubwa, lakini hajawahi kuiba hata senti. Eti anasema wezi hawataingia mbinguni. Mtu ana nafasi ya kutajirika haraka kwa pesa za shirika, yeye anakomalia uaminifu. Ujinga mtupu!
- Akipanda magari ya abiria, akizidishiwa chenji, anamrudishia konda pesa iliyozidi. Kweli huyu mtu hana akili! Wengine wangetumia nafasi hiyo kufurahia "baraka za ghafla," lakini yeye anang'ang'ana na uaminifu.
- Ukikutana naye, anajisifia eti hajawahi kuugua kisonono wala kaswende. Hayo magonjwa ndiyo "stori za mjini"! Eti yeye anajivunia maisha ya usafi. Mjinga sana huyu!
- Akikosewa au mtu akimtukana, hajibu matusi wala kupigana. Anaamini eti "kisasi atalipa Bwana," badala ya kujitetea kwa ngumi kama mwanaume. Ujinga mtupu!
- Huyu mlokole tangu aoe hajawahi kumpiga mke wake. Mke akimkosea, anamsamehe badala ya kumpiga na kumfundisha "adabu." Hii kweli siyo mental illness?
- Hawezi kusema uongo hata kidogo, hata kama uongo unamsaidia kukwepa matatizo. Eti anasema waongo watatupwa motoni. Huyu amewehuka!
- Akipata mshahara wake, anatoa fungu la kumi na kuwasaidia maskini. Jamani, badala ya kujilimbikizia mali yake, anawaza kusaidia wengine! Kweli huyu hana akili.
- Ana watoto wazuri, eti anawalea kwa maadili ya Kikristo badala ya kuwaacha "waende na wakati." Anawazuia wasitazame picha chafu kwenye mitandao, eti Mungu hapendi. Huyu mtu amepitwa na wakati!
Sasa hayo maandiko yako yanatofauti gani na methali za wahenga, au kisa hizo katunga Mzungu😆Mithali 12:1
"Apendaye mafundisho hupenda maarifa; Bali achukiaye kukaripiwa ni mjinga."