Huyu mlokole ni wa ajabu sana. Anafanya mambo ya ajabu! Msaidieni jamani

Setfree hajawahi kujamiiana hata siku moja maishani mwako.
Naomba nijibu bila kudanganya maana unatuona Wana JF kama watu walioopotoka wasiomcha mola hata kidogo.
 
Yote umeenda SAWA ila hapo pa kupiga mke sijakuelewa hao bila kipigo utakufa kwa stress
1 Petro 3:7
Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; maana wao pia ni warithi wa neema ya uzima, ili maombi yenu yasizuiliwe na chochote.

Badala ya kutumia ngumi ku-solve matatizo ya ndoa, tumia akili.
 
Kupanga ni kuchagua. As long as anaishi wewe inakuuma nini sasa.
 
unatuona Wana JF kama watu walioopotoka
Pole, mkuu. Kuna mahali nimesema wana JF wamepotoka? Unaweza ku-quote hiyo kauli? Nitai-edit nifute kauli hiyo.

Ila kama uzi huu umekufanya ujisikie hatia, dawa ya kuwa na dhamiri safi ni kutubu dhambi, kumwamini Yesu na kumpokea moyoni mwako. Ukifanya hivyo atakuwezesha kuishi maisha matakatifu yasiyo na hatia.

Omba (kwa kufuatisha kwa moyo wako wa dhati) sala hii ya toba, utaokoka sasa hivi na kujisikia amani.

“Ee Mungu Baba, nimetambua mimi ni mwenye dhambi. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen.”

Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Hutasikia tena hatia ya dhambi, maana Mungu amekusamehe. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuishi maisha matakatifu. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu, ujiunge nalo, watakuelekeza zaidi jinsi unavyopaswa kuenenda katika dunia hii. Ubarikiwe sana ndugu yangu.
 
Hamna mlokole wa hivyo acha kutunga story,walokole ninao wajua huwa wamepitia matatizo ndo wanapata akili ya kuokoa,ila tabia zao hazibadiliki
 
Tumekushtukia unatumia CHATGPT
 
Mnajaza bure server za jf
Mkuu, uko nyuma ya wakati. Tangu lini ulisikia Youtube server zimejaa? Watu wana-post kila siku videos zenye MBs/GBs kibao, lakini servers hazijai. Hizi "text only threads" ndio zitajaza server?
Kwanini unachukia ninapo-discourage maovu? Ningewahimiza watu wafanye uasi ndio ungefurahia? Ila kama wewe ni Atheist, siishangai kauli yako. Nakuombea tu Mungu akusamehe bure.
Luka 23:34
“Baba, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!”
 
Tumekushtukia unatumia CHATGPT
Wow, kumbe chatGPT inaweza kuhubiri Injili? Ah, basi itanipunguzia kazi, na unabii huu utatimia haraka.
Mathayo 24:14
Injili hii ya ufalme itahubiriwa[hata kwa chatGPT] ulimwenguni kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utakapokuja.
 
Akili na kibano vinaenda sambamba kwa kawaida akili ya binadamu hubadilika kutokana na mazingira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…