Huyu mtangazaji wa TBC1 wa michuano ya AFCON anatuongelea kiarabu kwa misingi ipi?

Huyu mtangazaji wa TBC1 wa michuano ya AFCON anatuongelea kiarabu kwa misingi ipi?

Acha kuchukulia kila kitu serious mambo madogo hayo mkuu
 
Siyo wewe tu anayekuboa. Na kama sikosei nimewahi kumsikia mwingine Azam au ndiyo huyo huyo? Angetokea mtangazaji akachomekea viingereza angenangwa hadi akome ila huyu inaonyesha kuna tabaka linaendana naye
 
Kama ukiona ww hupendi utangazaji wake na wengine wanapenda bc ujue jamaa yupo vizuri, ht ww binafsi hakikisha jambo unalofanya kuwe na watu wanalikubali na wengine kulikataa.
 
Kama ukiona ww hupendi utangazaji wake na wengine wanapenda bc ujue jamaa yupo vizuri, ht ww binafsi hakikisha jambo unalofanya kuwe na watu wanalikubali na wengine kulikataa.
Hoja ni lugha mkuu elewa mada basi. Sijakataa kuwa kuna watu wanaelewa kiarabu,ila mimi nisieelewa kwanini nisiseme? Kiarabu ni lugha yetu? TV ya taifa unaruhusiwa kuongea lugha yoyote unayoipenda kisa tu unaijua?
 
Acha kuchukulia kila kitu serious mambo madogo hayo mkuu
Lugha anayotumia siielewi mkuu,kama unaelewa kiarabu bado sio sawa,hii ni TV ya taifa huwezi ongea lugha yoyote kisa tu we ni mtangazaji unajua lugha. Ndio maana nikahoji their professionalism
 
Leo naangalia fainali ya AFCON kupitia TBC1 kutokana na mazingira niliyopo. Ila cha ajabu huyu mtangazaji somebody Upete anaboa anatuongelea kiarabu, hivi ndio professionalism yenu hii TBC1?

Au hamjui sio wote wanaelewa hiyo lugha? Mnawatoa wapi hawa watangazaji wanajifanya mamwinyi waarabu wa kuokota?

Yaani TV ya taifa kabisa? Ingekua kama Azam au Wasafi angalau isingekua na shida.
Vitu vya bure vina gharama
 
Huu ujinga wa kujifanya kila mtu mwarabu umetamalaki Sana awamu hii ya kizmkazi.
Au usikute wanajaribu kumuimpress wawe ili kwenye zile safari za arabuni...🤣
 
Mbona yule mtangazaji somebody Mathayo wa Upendo Tv akipandisha midadi anatangaza mpaka kiebrania na kunena kwa lugha goli likifungwa na hamlalamiki?
 
.......na tayari mchungaji wako alishakuambia kiarabu lugha ya majini!
 
Afadhali ya huyo, kuna mwingine muda wote anaongea matusi tu.
Utasikia, ''anaitumbukiza kuuubwa, anamwaga maji mengi'', na matusi mengine mengi.
Hii sio, wengine tunatazama tukiwa na familia, tunahitaji maneno yasiyo na ukakasi
 
Hoja ni lugha mkuu elewa mada basi. Sijakataa kuwa kuna watu wanaelewa kiarabu,ila mimi nisieelewa kwanini nisiseme? Kiarabu ni lugha yetu? TV ya taifa unaruhusiwa kuongea lugha yoyote unayoipenda kisa tu unaijua?
Kwani Kiingereza ni lugha yetu mkuu? Mbona kuna sehemu ulisema bora angeongea kingereza?
 
Hata mechi ya simba na azam Mtangazaji wa azam tv naye alikuwa anaongea kiarabu hii ni fedheha sana kulipwa mshahara atangaze Kiswahili halafu anaenda kinyume na masharti ya kazi yake .
 
Hoja ni lugha mkuu elewa mada basi. Sijakataa kuwa kuna watu wanaelewa kiarabu,ila mimi nisieelewa kwanini nisiseme? Kiarabu ni lugha yetu? TV ya taifa unaruhusiwa kuongea lugha yoyote unayoipenda kisa tu unaijua?
Mm sielewi Kiarabu na napenda utangazaji wake.
 
Back
Top Bottom