Huyu mtangazaji wa TBC1 wa michuano ya AFCON anatuongelea kiarabu kwa misingi ipi?

Huwa ananiboa sana yule... niliamua kuachana kuangalia mpira TBC... nikaja kwa kina Mbwaduke huku na kina Nyembere...

Hata Evans Muhando ni muhuni tu kwenye kuchambua soka... ujanja ujanja tuu...[emoji38][emoji38][emoji38]
Evans ujanja mwingi kumbe umemstukia anarukia rukia data
 
Tumekula mkuu, ila TBC1 wanatuletea njaa tu saizi yaani limefungwa goli jamaa anatiririka kiarabu na kushusha dua mwanzo mwisho. Mwanzoni wakati mechi inaanza sikujali nikajua anachomekea tu
Saa hivi ni kawaida nadhani ni matokeo ya kiarabu kufundishwa kwenye baadhi ya shule na watu kutaka kujiweka ki utofauti ili waonekane wanajua lugha nyingi
Kingereza kiarabu kifaransa na kiswahili
 
Sasa mpira nao unataka utafsiriwe kwani macho yako hayaoni, kama kiarabu kinakukera punguza sauti uangalie picha tu
 
Soma kwa makini ulichoandika kisha lia kwa muda uliopoteza shule.
 
Hii Kamba Sawa Na Kunena Kwa Lugha Sijui Kiarabu Ila Ukisikiliza Unasikia Kabisa Ile Ni Lugha Sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…