Huyu mtu hafai atakutesa sana na kufanya usione thamani yako

Huyu mtu hafai atakutesa sana na kufanya usione thamani yako

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
471
Reaction score
1,217
1.Ambaye muda wote anakukosoa kana kwamba hakuna hata siku moja umewahi kupatia hii ni dalili kuwa wewe sio yule akutakaye

2.Muda wote anakulaumu tu kana kwamba hakuna hata siku moja umewahi kuwa mwema kwake hii ni dalili HANA MUDA NA MAZURI YAKO

3.Mara nyingi anakutishia kuwa kuna watu wenye hadhi zaidi yako aliwakataa ili awe na wewe hivyo hata mkiachana bado SOKO LAKE LIKO JUU hii ni dalili kuwa ALIKUCHAGUA TU BAHATI MBAYA HUKUWA HADHI YAKE.

4.Haoni bahati kuwa na wewe bali anaona wewe ndio UMEPATA bahati ya kuwa na yeye hapa hata siku moja hatakuomba MSAMAHA

5.Hana hofu ya kukupoteza muda wote mkipishana anadai MUACHANE.


6.Anakuona kama vile wewe ndio UNAMUHITAJI zaidi ya ANAVYOKIHITAJI


7.Ukikosea ni makusudi ila akikikosea yeye BAHATI MBAYA

8.Anadharau ndugu zako

9.Mara nyingi mawasiliano yanakuwa hai kama tu UMEANZISHA WEWE au akiwa na UHITAJI fulani tu


10.Mkipishana tu kidogo anaanza kujutia maamuzi yake kukuchagua


#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako
 
Back
Top Bottom