Ndugu zangu Watanzania,
Jana hapa nilileta andiko langu nikasema kuwa nimefanya uchunguzi wa kina sana tena sana wa kuchunguza watu hawa wawili kati ya yule komandoo aliyekuwa kiongozi wa kikosi maalumu cha makomando pamoja na yule kijana muuza madafu wa ikulu. Ambapo watu walikuwa wanasema ni mtu mmoja.jambo ambalo mimi nililipinga sana japo andiko langu likaja kuunganishwa na lingine na hivyo kuzima hoja yangu kwa njia hiyo.
Sasa ukweli ni ukweli tu hata ukipingwa na watu wengi lakini unabakia kuwa ukweli tu. Mimi jana nilipingwa na kushambuliwa sana humu jukwaani na wengine kunitukana matusi kuwa mimi nimekurupuka,wengine kusema mimi ni chawa nisiye na akili na wengine kusema mimi ni hasara na aibu hata kwa wazazi walionizaa. Nilivumilia hali na udhalilishaji wote kwa kuwa mimi ni mvumilivu na mtu mwenye ngozi ngumu .hivyo nikaamua kuwasamehe tu kama kawaida yangu.
Sasa leo Ayo Tv wamemtafuta yule muuza madafu wa ikulu na kumfanyia mahojiano ambapo kwa sasa ameweza kununua boda boda mpya kutokana na pesa aliyoipata siku ile Ikulu ,ambapo ameongezea kwenye ile aliyokuwa nayo kama akiba yake.amesema hata yeye alishangaa sana watu walipoanza kumfananisha na yeye mwenyewe aliangalia maadhimisho yale na kushangaa.
Ndugu zangu Watanzania tusipende kufuata mikumbo na kusombwa na ujinga unaokuwa umeanzishwa na mtu mmoja na kuufanya kusambaa kama moto wa petroli na kila mtu kuanza kuiamini bila kufanya utafiti.Mimi huwa sikurupuki na kuanza kuamini jambo na kulisambaza bila kujilidhisha ukweli wa jambo husika.ndio maana jana baada ya uchunguzi wangu wa kina na Elimu yangu ya kumsoma mtu katika uso wake juu ya mfanano ,hasa kwa kuangalia macho,pua,mdomo,paji la uso,upana wa sura ,umbile la mdomo wakiwa wamefumba mdomo ,mkao wa pua kutoka juu pamoja na muonekano wao kwa ujumla nikaja kugundua kwa haraka haraka kuwa ni watu wawili tofauti kabisa.
Ninashangaa watu wengine wenye heshima zao nao waliingia kwenye mkumbo huo wa kuamini taarifa zile za kizushi kabisa.tujifunze kuwa watafiti na watulivu katika mambo mbalimbali na siyo kumezeshwa tu Matango pori au kuimbishwa kama makasuku. Kukumbwa kamwe na katu usimuamini mtu katika habari au taarifa yoyote ile bila ya wewe kujiridhisha ndio ukaitoa.
Leo mimi ni shujaa japo jana nilionekana kama mjinga na mwehu.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.