Huyu mwanamke alikuwa anaonyesha u-wife material ila baada ya kumwambia sitafuti business partner nataka mke basi kaanza kutafuta njia ya kuondoka

Sasa kumbe mnajua kuwa biashara siyo ya kila mtu sasa mbona wakikaa nyumbani mnasema hawana akili na mnawaita magolikipa na ombaomba
 
Usitumie hasira utakuja kulia. Sheria nyingi zinawapa kombe.
1: Mfungulie biashara ya kwake na wala usiifuatilie ila ukiweza weka katika maandishi, fedha , vifaa na kodi ulizowekeza hapo na wala usimpe maneno magumu bali ya kumtia moyo.
2: Mpe uhuru na wala usimfuatilie ila mshauri vile ungetaka familia yenu iwe.
3: Ukiona hana muelekeo, wekeza katika kesho ya watoto wako (fungua akaunti za ada zao, nk)
4: Kama hata penzi unateseka, TULIZA kichwa na utafute demu mmoja mwelewa sana( jitahidi uchuje ili umpate mwenye vigezo utakavyo), huyu atakusaidia usiue au kumng'oa mtu meno.
5: Jitahidi usirudi nyumbani ukiwa na njaa sana au umekasirika ikibidi pitia pahala ule japo kidogo na taraaaatibu rudi nyumbani
 
Unaonekana ni Mnyanyasaji wa hali ya juu

Hauna heshima kwa Mwanamke wako

Umejawa dharau na kiburi uko na full EGO

Hutopata Mke bora..unless otherwise upate zwazwa wako wa kumburuza atakaekubali kejeli zako na kuridhika na dharau zako
 
badala ya kumuacha mkeo afanye biashara asiwe tegemezi unakuwa mbabe
Maisha yanabadilika haraka sana Kuna leo na kesho haupo unafikir
Ataishije na watoto bila ya kipato
Hebu na hilo ukalitizame
 
Unaonekana ni Mnyanyasaji wa hali ya juu

Hauna heshima kwa Mwanamke wako

Umejawa dharau na kiburi uko na full EGO

Hutopata Mke bora..unless otherwise upate zwazwa wako wa kumburuza atakaekubali kejeli zako na kuridhika na dharau zako
kasema ana michepuko 3 inachukua shift 24/7 πŸ˜‚
 
Kuna kitu jamaa kaongea kuna mda aliamua kupima DNA na watoto hapa kuna kitu kinakujia kichwani shemeji ni wa aina gani kiufupi tabia zake zinamfanya awe na uaminifu mdogo kwa bwana yake

Kingne kuruhusu mwanamke kuwa na biashara inayomlipa na kuwa na uwezo wa kujikimu hilo ni bomu kwenye ndoa ndugu yangu ni bora mke wako afanye biashara zako wewe mme uwe boss sharti hela ya matumizi ya nyumbani asichukue kwenye biashara. Kwenye biashara ifungwe hesabu ili kujua faida au hasara. Ila matumizi ya nyumbani pesa atoe mme nasisitiza na sio mwanamke kuchukua ya kwenye biashara utalizwa mapema sana.

Wanawake wanaojiweza kwenye ndoa ni mwiba sana na wengi wao ni wachepukaji wakubwa sana katika deal zao za business huku akikwepa majukumu fulani. Ipo hivi wanaume wanaomliki frame, business connection, car transportation goods wanawala sana hawa wanawake ndo hapo nipoanzaga kumdharau mwanamke hata kama nimezaliwa nao
wanaume tunataka mke mwenye sifa ya kuwa mke kama hizi...

Kinachotufikirisha kingne wanaume ni kwamba hawa wanawake wa business mara nyingi wanatumia ngono kurahisha mambo kwenye biashara zao tunawaona na wengi wao wameolewa. swali linakuja namana hata mke wangu atafanya hivi hapo ndo ukiwa na uwezo wa kumkontrol asifanye biashara unafanya ivo

Mwisho heshima kwa mwanamke mwenye pesa ni maji na mafuta kwa sababu biashara yoyote ikisimama lazima uwe bussy nayo na hapa mwanamke anapoteza ule u mke hata unyumba huwa tunaanza kupata kwa shida ukipata napo unapimiwa ila mlipa kodi atakula ajichokee maana anajua akizingua kodi hailipwi kikamilifu

Tutaendelea............
 
Vipo vichwa hatari sana havifundikishi, vinamiliki biashara na madeni tunalipa sisi tuone huruma, hahahaha
 
Ngoja jioni nitajibu comment zenu wote. Ila kiufupi mie nimekulia kwenye family mzee alikua na wake watano na wote aliwamanage vizuri sana hadi leo wanaheshimiana, na watoto tuko 13. Nitawajibu vizuri jion
Ooh basi usitafute mchawi tatizo lipo hapo hata akija mwanamke mwingine bado tatizo litakuwepo tu kutokana na kutoka kwenye familia ya polygamy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…