Huyu mwanamke ni sahihi kuniambia maneno haya?

Kwa mshahara wa laki tano unataka nitoe kiasi gani? Au niibe ? Na sio mara ya kwanza .Mtu lazima atoe alichonacho kinachotakiwa na kupanga budget
 
Wewe ni mpumbavu babaako wakati anamuoa mama yako alikuwa Bakheresa? Unadhani anaepata 10,000 hatakiwi kuoa?
 
Tilia sana mkazo maneno yanayosemwa na mtu mwenye hasira au aliye lewa,hua yana ukweli kwa asilimia kubwa sana,huyo mke hakufai,usije kusema sikukwambia,wake up mkuu,kauli yake hiyo ya kukwambia utasaidiwa kulea familia ina ashiria kua huyo mtu yupo tayari,

Yangu ni hayo tu,
The rest it's up to you.
 
Mtu huyatoa yaliyojaa ndani ya moyo wake...

Kaa chini naye muongee, akueleze sababu ya msingi ya kutamka alivyotamka...
Mkuu,mtu wa aina hiyo hawezi kubadilika,kufikia kumuombea kifo Baba wa mwanae ni ukatili wa hali ya juu sana,huyo sio mke bali ni Adui,mleta mada asimame kama Mwanaume na asitetereke,huyo ni wakupiga chini tu,huwezi kukipulizia kinyesi perfume ili kinukie.
 
Maneno aliyoyatoa ni magumu na hayajengi, ila bajeti ya elfu 30/7 ni mtihani kwa maisha ya familia ya watu watatu.
Muelewe mleta mada. Kuwa kila kitu kiko ndani, Yaani mahitaji ya familia tayari yamenunuliwa, na hiyo 30,000 ameiacha kama emergence money in case umeme umekata.

Na sio matumizi ya kila siku kama ulivyo andika 30,000/7
 

Ni kweli ulichoandika...

Adhabu nzuri ni ili unayompa mtu baada ya kuleta utetezi, ili asijelalamika kuwa kaonewa...

Kauli kama hizo hutolewa na mwanamke mwenye dukuduku la muda mrefu...

Huenda kwa kisa hiki pekee mwanamke akawa mwenye makosa, lakini huko nyuma kuna kasoro nyingine nyingi baina yao...
 
30,000.00 kwa wiki ni ndogo sana....

Akinunua nyanya, vitunguu, karoti, mboga za majani, nyama kidogo angalau once for a week..... HIYO HELA NI NDOGO SANA.....
 
Pesa ni ndogo. Ila mwambie mkeo ajiongeze kua goal keeper changamoto
 
Sasa wewe jamaa elfu 30,000 kwa week kweli? Sisi tuko wailing na hyo hela haitutoshi na ni wanaume hauko serious mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…