Huyu mwanamke ni sahihi kuniambia maneno haya?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Write your reply...pesa nxngi sna km mahitaji muhmu yapo km unga mchele mkaa upo.hyo ni km balance tu.huyo mwanamke hafai hajui nn maana ya maisha kaja kuchuna wala si kusaidiana ktk malezi.km sina nikaibe.ndyo matatizo yakuoa machangu
 
Watu mnasema 30 haitoshi..watu wawili? Sijajua kipato cha kila mtu lakin haya maisha jamani yatakushape tu usipojipanga..kama ndani kulikuwa na mahitaji necessary hiyo hela angeibana kwa upendo na consideration ingetosha.

Binafsi nimekulia katika familia iliyoishi katika hali zote. Kuna wakati ulikua mgumu sana kiuchumi na tuliishi kwa kipato kidogo sana. Maharage, dagaa, kisamvu vilitukoma. Ilikua ni bandika bandua.

Mwanamke anatakiwa awe mtu wa mahesabu makali sana. Bila ivyo kufeli ni fasta tu. Kwa mfano mkuu ameshasema hapa kila kitu ndani kilikuwepo.
 
nakushauri umfukuze haraka sana, akigoma kuondoka muachie gheto ukaanzishe maisha mengine
ni ana tamaa, hana kauli njema kwako pia amekuchoka sana
 
Unamtesa mwanamke wa watu mkipigiwa wake zenu mnakimbilia kujiua 30 kwa week huo unyanyasaji af unapokea laki tano kwa mwez broh kua na huruma
 
30000 kama kila kitu kipo ndani inatosha,na inategemea pia uko mji gani,,

Wanawake wasiowahi kutafuta ndiye atadhihaki hiyo hela ila ukishaonja mambo yaliyoko kwa ground aaah wee hata ukipewa buku 5 unaipigia mgoti kushukuru ndipo unasema sasa baba hii haitoshi nk
Labda hakufurahishwa na wewe kwenda kwenu kupeleka mazaga zaga nk huyo ni mchoyo na huyo mpwa wako hamtaki humo ndani,,

Kukuombea kifo kwa kisa kama hicho hilo ni bomu kakaa
 
Aisee kiukweli kabisa HUNA MKE HAPO
 
Thinking out loud;
Nanunua karoti 1000, hoho 1000, vitunguu maji 1000, Swaumu 1000, tangawizi 500, dagaa 2000, nazi 2 3000, nyanya 3000, mboga 5500, kabichi 1000, nyama ¹/² 5000, bamia na nyanya chungu 2000, viazi ulaya 500, ndimu 500, nauli 2000..1000 iwe reserve na usali sana kisitokee chochote ili hela itoshe kwa wiki hiyo ya kwaresma majinuni...

Ratiba ya msosi utapanga mwenyewe ila kwa ushauri..unapika mboga ya mchana na jioni kwa mara moja, ili kusave vitu. Like maybe,

J3; mchana- Ugali ndondo (nazi unatumia nusu kipande) na harage hili ni robo kilo..na mboga ya majani fungu moja...
Jioni- wali na ndondo la mchana na mboga fungu moja.
J4; mch- ugali dagaa na mboga
Jioni- wali na mboga za mchana.
J5; mch- ugali bamia na nyanya chungu na mboga.
Jio- wali wa mseto wa harage (no nazi) na mboga ya mchana ya majani.
Alh; mch- ugali na mboga ya majani
Jio- wali wa nyanya na mboga ya majani.
Iju; mch- ugali dagaa na majani
Jio- chapati harage la nazi kipande
J1- mch- wali kabichi ya nyanya
Jion- ugali nyama na ile kabichi
J2- pilau la nyama na viazi la mchana na jioni. Na kabichi
J3- hapo baby anarudi kwaiyo ni ugali ndondo na mboga na jion wali ndondo na mboga ya majani nazi kipande.

Kuna nyakat katika maisha yetu hatuli ili tuenjoy sweetness...tunakula tuishi, tusife..kwaiyo itabidi tuvumilie tu hakuna namna. Kama una maharage ndan tayari una mboga.

Ukiyachemsha yakaiva vizuri kwa kulainika, ukakatia kitunguu kimoja vimafuta na chumvi utakula ugali au wali na utakunywa maji, utalala ukimshukuru Mungu. Kuna wanaotafuta na wanakosa hayo wewe unacho.

Kuna wengne watasema "ooh ananipa kidogo af anakula na malaya zake.." sawa ni kweli lakin what does not kill you makes you stronger. Inawezekana baba zetu waliachaga budget ndogo nyumbani wakaendaga kuhonga kwa wanawake wengine lakin leo nimekua hata kama niliteseka kipind hcho, leo nina uwezo wa kuishi kwa mtu yoyote na nikala kinachopikwa hata ni mlenda wa bamia peke yake..tena kwa furaha na amani.

Kwaiyo mwanamke mwenzangu usihisi kwamba mtoto wako anateseka, ama sijui notions gani..hapana. unapoona ivyo, mwanao anakuwa shaped kuja kuwa mwanamke strong ama mwanaume strong. Let them live through the hard times...tulikula na hatukufa.

Kama uliona mwanaume mbaya, ama malaya..usingekubali kuwa nae in the first place. Mpaka umekubali kuolewa na kuzaa nae watoto..ulikubali yote..kama ni lawama jitukane mwenyewe, lakin usimdhihaki mtoto wa mwanamke mwenzio..hata wewe unae mtoto utapenda kuja kuona anatukanwa na kudhalilishwa?? Tuwe makin sana na vinywa vyetu...ukiona hasira imekuzid nakupa technique...jaza maji mdomon afu funga mdomo..afu katafute kazi kuwa busy...unaweza ukatoa maneno saiv yakaishi miaka 10 baadae..huwaga hayafutiki haraka, mwe na hasira lakin msitende......
 
Umemuelewa lakini hoja
1.kipato chake kidogo
2.Kauli chafu
 
Hao kauli chafu wanarithi toka kwa mama zao. Ukiwa na roho nyepesi mbona utaingia jela. Kama huna kipato hakiruhusu kausha hawatokufa kwa njaa.
 
Bro..ukiona hivyo ujue kuna mtu anaonekana ni bora kuliko wewe..shtuka
 
Maneno ya wanawake wasiofundwa kama ulikosea kuoa usipende kuyabeba yatakuletea umasikini, magonjwa, upungufu wa nguvu za kiume, ugonjwa wa akili, kushuka moyo sonona, nk. Ili usonge mbele ni kuyapuuza, maana watu aina hio hawana filter chujio la maneno wao kauli utoka kama zilivyo.
Hao dawa yao kama pesa inaruhusu ni kumletea mke mwingine.
Dawa ya mwanamke jeuri ni mwanamke mwenzake
 
Mtaftie mtaji wa biashara

Na utaendelea kumpa pesa za matumizi kidgo kidogo
 
Mwamba unajikuta bahir kwenye hamna[emoji16][emoji16] 30k ndogo mnoo. Hasa kpnd hik cha skukuu. Anii acha ubahr ataliwa huyo
 
Mijitu ya hovyo sana

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…