Huyu mwanamke ni sahihi kuniambia maneno haya?

Inategemeana, kama mahitaji yapo kama Mchele, unga n.k 30000, ni kubwa tu mbona, tatzo wanawake wengine wanacheza kikoba kwa hela matumizi

Kwani si kasema hapo mshahara wake laki tano tu ...au wew laki tano kwako ni pesa nyingi?
 
Unamtesa mwanamke wa watu mkipigiwa wake zenu mnakimbilia kujiua 30 kwa week huo unyanyasaji af unapokea laki tano kwa mwez broh kua na huruma
Jamani laki tano ni hela nyingi? Kumbuka hapo ukiachana na kula kuna kodi ,ada nauli, matibabu na matumizi mengine
 
Kama una pata laki tano tenga bajeti ya kununua vitu vya jumla.

Mfano; mchele kilo 10, unga kilo 10, maharage 10, mafuta ya kupikia lita 5, hapo bajeti ni 150k.

Halafu unakua unanunua vitu vidogo vidogo vinavyoharibika kadri unavyopata. Mf. Nyanya, vitunguu, nyama , mchicha etc.
 
Kwa kipato chake kinamuwezesha kukamilisha hayo mambo mkuu na ndiyo maana mkewe akaona kama anamzingua kumuachie elfu 30 kwa week maana alishampima kwamba ana uwezo zaidi ya huo.

Wanawake wanajua kukupima urefu wa kamba wa mwanamme.
 
Sio kweli mkuu. Jamaa anasema vitu basic vyote aliacha kanunua. It means hiyo 30k ni Kwa ajili ya mboga.

Jamaa kuwa na kipato cha 500k kwa mwezi, haimaanishi chote kitumike kwenye kula, imagine alikuwa kasafiri, pengine alitoa na nauli
 
Inategemeana, kama mahitaji yapo kama Mchele, unga n.k 30000, ni kubwa tu mbona, tatzo wanawake wengine wanacheza kikoba kwa hela matumizi
Umegusa penyewe. Vikoba na upatu ndio tatizo
 
Humu wengine wanaongea tu kuchangamsha Kijiwe, ila 30k ni kuwa Kwa watu watatu kwa wiki moja.
 
Elfu 4,500 kwa siku ina shida gani wakati makolombwezo mengine yotw yapo ndani?
Soma vizuri uzi wa jamaa mke wake alijitahidi kubana matumizi lakini kabla ya siku 2 jamaa arudi mke akampigia simu kuwa ile elfu 30 imeisha.

Kwa hiyo kwa mahesabu rahisi mke wa jamaa yetu kajibana bana katumia elfu 30 kwa siku 5

Hatujui kama wanapikia gesi mwanzo mwisho au huwa wananunua mkaa kupikia hayo maharage na mchele ambao jamaa kanunua? Hivyo vyote mume hajataja kwenye uzi wake au kama gesi ipo iliisha ikabidi akanunue, hatujui. Je, kuna siku umeme uliisha mke akanunua? Hatujui!

Ukiacha hayo pia nyumbani kunakuwa na matumizi ya dharura na ya ghafla wakati mwingine

Mke kajitahidi sana kosa lake ni kwenye kauli na hatujui ni nini kilipelekea mke aseme hivyo kwa sababu hapa tunasikiliza upande mmoja tu wa mume. Usikute mwanetu ndiye aliyeanza kumvuruga shemu

Ila kwenye matumizi elfu 30 kwa siku 5 mke kajitahidi kikweli
 
Mchele, maharage, sukari, unga na mafuta vyote vipo ndani. Unataka aache shilingi ngapi? Unatakiwa uishi kulingana na kipato. Shida ya wanawake baadhi anataka hiyo hiyo hela ya matumizi anunue nguo bado vikoba.
Kuna vitu vidogo vidogo, na kubadili mboga na vitafunwa vya chai

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Umenena vyema ,30000 inadhiakiwa kumbe wanodhiaki Ni mafisadi na wez was uume za watu

Ila 30000 huko ngara ,kagera Ni pesa ndevu mno

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Good point

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kitendo Cha kutaka wee upate ajali ufe au usadie mwambie nimekuelewa Sana .mkuu unapotoka safarini njoo na mazagazaga mengine

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Sio kweli mkuu. Jamaa anasema vitu basic vyote aliacha kanunua. It means hiyo 30k ni Kwa ajili ya mboga.

Jamaa kuwa na kipato cha 500k kwa mwezi, haimaanishi chote kitumike kwenye kula, imagine alikuwa kasafiri, pengine alitoa na nauli
Mkuu una familia kwanza? Mtu una kazi halafu unasafiri week nzima unaacha unga,maharage na mchele kisha unasema elfu 30 inatosha as if ni wafungwa wa kula maharagae kila siku ,mkaa ,mafuta ya kupikia ya kula etc? Mkaa kopo moja Tsh 1500 , Mafuta ya Taa lita rejareja 4000 ,nyanya nne buku.

Kama hawezi kulea familia bora amrudishe kwao..
 
Mhaya unakipato cha laki 5?

Si ukawe mfagiaji kwa mganyizi sr akulipe milioni 2.
 
watu wanamshambulia mtoa bandiko japo mimi sijaona kosa hapo

watu wa 2, mahitaji mengine yapo buku 30 ina shida gani?

fukuza huyo pimbi, tuone kama atapata wa kumpa laki kwa siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…