Huyu mwenye nyumba sasa anatunyanyasa. Rais/Serikali iingilie kati jambo hili wanaichonganisha na wananchi

Huyu mwenye nyumba sasa anatunyanyasa. Rais/Serikali iingilie kati jambo hili wanaichonganisha na wananchi

Nimesoma coment zote, hakuna hata mmoja aliyemuelewa Minjingi jingu. Bandiko lake ni lugha ya picha, hamaanishi uhalisia wa maneno aliyoyatumia bali kile kinachowasilishwa na hiyo lugha yake ya picha. Kodi, kodi, kodi, kodi............. Mpaka Serikali ikamilishe miradi.
 
Nyumba ya kupanga tupo hapa Buguruni Mnyamani ni shida sana. Ni manyanyaso kwa sisi ambao ni mambo safi. Maana naona vijana hapa tunashindana sana kuweka madish ya visimbusi mbalimbali. Na kutumia masabuwufa ya sauti kubwa. Tuliwasha jioni hatusikilizani na hatuna shobo na mtu. Mi nimenunua seapiano kubwa sana kwa sasa nawafunika mbaya madogo.

Mimi niliweka Dstv ,nikaweka na azam na star times. Na wenzangu wamefanya hivyo hivyo na mwingine ana decoder 5 mpaka makampuni mengine siyafahamu. Tumepanga watu 9 hii nyumba tunashindana sana sasa natafuta madish mengine ya kampuni kali kama 4 ili jumla niwe nayo 7 nimshinde huyu dogo mwenye 5. Maana naona kama anajiona yeye ndo mwamba hapa.

Shida jana mwenye nyumba katuita. Anasema tutaangusha ukuta wa nyumba yake. Madishi yamekuwa mengi sana. So anataka kila mtu abaki na dish moja moja tu. Kama ukitaka kuongeza kila dish unalipia tsh 10 kwa mwezi.maana anasema yanalegeza ukuta.

So dish moja bure linalozidi kila moja tsh 10,000. Na tunaanza mwezi huu. Hapo maana yake tsh 60,000 kama ntaweka madish 7. Sasa jamani huu si unyanyasaji wa ki...nini sijui. Maana kuna unyanyasaji wa kijinsia, kiitikadi na kadhalika.

Hii siyo haki tunaomba rais aingilie jambo hili si sawa. Huku ni kama kutaka mchonganisha rais na watu wake. Ionekane rais au serikali haijali watu wake. Kumbe ni watu kadhaa wachache tu wanataka ichafua.
Mdishi saba unapata muda wa kuangalia hayo yote hayo,Are u a house wife?
 
Ndio hapa
Screenshot_20250613-105849.jpg
 
Back
Top Bottom