Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 12,826
- 17,371
Ona na wewe ulivyosimama kwenye upande!Hio october 7 ilikuwa ni kisasi cha Hamas dhidi ya mauaji na unyanyasaji wa jeshi la Israel, hao ugomvi wao hukuanza oct 7..
Ukirudi nyuma utagundua tu Israel ndiye tatizo, hadi hao Paleatinians wanafanya kile tarehe 7 Oct walikuwa wamechoka, na wao ni binadamu...
Kama mtu hapa Tanzania, tunasikia mtu kamuua mpenzi wake kwa kumpiga risasi au kumchoma moto, vipi mtu anayeua watoto wako, anakalia ardhi yako kimabavu, utafanya nini?
Hao Palestinians ni watu kama sisi, wanaumia na wana kikomo cha kuvumilia...
Ndio maana kina Nyerere waliiunga mkono Paleatine, kina Mandela, si kwa sababu ya udini la hasha, ila ule ni ukoloni.
Hata South Africa wananchi wamepambana sana na makaburu kudai ardhi yao. Ndio maana SA wengi ni Pro Palestine cause issue inawakumbusha pia wao nyakati zao na harakati za kupambania uhuru.
Israel akubali, Palestine itambulike taifa, vita haitosimama.
Kwa hiyo suluhu ama haki hutafutwa kwa kulipiza kisasi?
Mtu akikupiga nawe ukampiga tayari huo ni ugomvi.
Palestinians hawakustahili kutafuta suluhu kwa kufanya ugaidi.
Ugaidi kwa kingereza ni terrorist, kuwatisha mahasimu kwa kuteka watu wao ili watekeleze unachokitaka, hilo ni kosa la kisheria za kimataifa
Sasa uliyemtisha naye kajibu tishio kwa ukamilifu unaopaswa, matokeo ni mwendo wa kulia lia na kukimbizana kwenye mahandaki kama nyaga pamoja na kuwakinga raia kama ngao.
Mwana kulitafuta mwana kulipata, hivyo ni vita hatupaswi kuelekeza lawama ama upendeleo kwa upande wowote, wacha wapambane, mshindi ndiye atakayelibeba kombe.