Huyu ndie wa kutuvusha salama mwaka 2025

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Mzalendo msikivu, Mwenye huruma, anaye jali utu wa watu wa hali zote, muungwana kwa maneno na vitendo, mchapakazi makini, mahiri na hodari wa kuhubiri Amani, Umoja, mshikamano na utangamano wa waTanzania.

Ni alama ya demokrasia, uhuru, haki, uwazi, uwajibikaji na usawa nchini. Mwenye maono ya maendeleo ya watu na vitu aliebeba matumaini ya uhakika ya waTanzania.

Hakika Mama Samia Suluhu Hassan ni pendekezo sahihi na la uhakika, kutuvusha salama uchaguzi mkuu 2025.

Neema na Baraka za Mungu zikuandame vema dominika ya leo .
 
Tujipangeje na tayari tunapigwa left and right na vibaraka wake.
unamzungumzia adv. Robert Amstardam wakili mbobezi wa mjamaa wa uhamishoni mwenye makazi yake ya kudumu na familia mpya huko ngamabo na huku tz anakuja kuwahadaa tu waTz, au mimi ndio sijaelewa vizuri?
 

Attachments

  • t.jpg
    57.7 KB · Views: 1
Atakuvusha wewe tu, Hafai kwa nchi yetu
 

Uchaguzi gani boss, Tanzania hakuna uchaguzi, bali Kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura.
 
Huo ndio ukweli wenyewe kuwa Rais samia ndio mtu sahihi aliyesheheni sifa zote zinazohitajika na watanzania juu ya kiongozi wanayemhitaji.,anastahili kuendelea kututumikia watanzania kwa kuwa amekata kiu yetu na kukidhi matarajio yetu watanzania.
Mbona hujaweka gazeti Leo, au simu inakaribia kukata charge kutokana na mgao Nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…