* NI MOJA WA WANASIASA WENYE ITIKADI YA UJAMAA/UJIMA WALIOBAKI NCHINI...
DR. Emmanuel Nchimbi alizaliwa tarehe 24.12.1971 mkoani Mbeya ambapo Mzee wake alikuwa mtumishi katika mkoa huo. Dr. Nchimbi ni moja wa vijana walio shupavu ambalo Taifa hili linajivunia kuwa nao.
1994~1997 alipata shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha MZUMBE. 2001~2003 akafanikiwa kupata shahada yake ya pili katika masuala ya Finance & Banking (Mzumbe) na 2008~2011 alifanikiwa kupata doctorate degree (Phd) katika chuo cha Mzumbe..
Dr. Nchimbi anatafsiriwa kama kiongozi makini. Jasiri. Mtulivu. Na mara zote amekuwa akisimamia kile anachokiamini. Dr. Nchimbi ana uzoefu mkubwa katika mambo ya sheria na utawala, na sehemu zote alizopita katika utumishi wake alifanikiwa kufanya makubwa sana.
Dr. Nchimbi amewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi (2012~2013). Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo (2010~2012). Naibu waziri wa ulinzi (2008~2010). Naibu waziri wa kazi, Ajira, na maendeleo ya vijana (2006~2008). Naibu wa habari (2006~2006). Mkuu wa wilaya (2003~2005). Na Afisa Tawala Mwandamizi katika Baraza la Mazingira (1998~2003).
Dr. Nchimbi amekuwa mjumbe wa vikao vikubwa vya maamuzi katika chama chake, amekuwa mjumbe ndani ya Kamati Kuu kwa miaka 15, na mjumbe wa Halmashauri Kuu kwa miaka 15 kitendo kinachomfanya kuwa moja wa watu waliotoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa.
Uzoefu wake na mchango wake katika chama ni jambo lisiloelezeka. Dr. Nchimbi ndio alikuwa kinara wa kuonyesha viongozi wakubwa wa nchi kwamba vijana ni Taifa la leo na sio la kesho. Na hili alilifanya chini ya uongozi wake ndani ya UVCCM kwa kuandaa na kuwajenga vijana wengi kitaaluma, kimaadili, na hata kisaikolojia.. Wengi wa viongozi vijana tuliowashuhudia mwishoni mwa awamu ya tatu na katika kipindi chote cha awamu ya nne waliandaliwa na kupikwa vyema ndani ya UVCCM iliyokuwa chini ya Dr. Nchimbi..
Tutakuwa wezi wa fadhila, kwamba unapozungumzia mafanikio ya serikali ya awamu ya nne usipolitaja jina la Dr. Nchimbi. Tutakuwa wezi wa fadhila, kwamba unapozungumzia mafanikio ya vijana wengi waliokuwa UVCCM na leo hii ni viongozi wakubwa usipolitaja jina la Dr. Nchimbi. Tutakuwa wezi wa fadhila, kwamba unapomzungumzia vijana wengi wa CCM walioingia bungeni mwaka huu usipolitaja jina la Dr. Nchimbi. Wengi wao waliandaliwa na uongozi wa Dr. Nchimbi ndani ya UVCCM...
Hakuna asiyekubali labda awe mwizi wa fadhila, kwamba kazi aliyoifanya Dr. Nchimbi serikalini, bungeni, UVCCM, katika chama na kwenye vyombo mbalimbali vya maamuzi ni vya viwango vya kupigiwa mfano na kwa maana hiyo yeye ni sehemu ya mafanikio tutayoyaona katika nyanja hizo...
* KWA NINI DR. NCHIMBI?..
1. Elimu na uzoefu wake wa kutekeleza majukumu anayopewa
2. Mchango wake katika chama na jumuiya zake
3. Anaungwa mkono na kundi kubwa la vijana
4. Ndiyo mgombea pekee mwenye nguvu kwa wabunge wateule
5. Kuwa mfuasi wa itikadi za ujamaa au ujima zinamfanya kuwa mtu sahihi katika hii awamu
6. Uwezo wake wa kuunganisha makundi mbalimbali. Hii itamfanya aweze kuunganisha wabunge wote pasipo kuangalia itikadi zao
7. Ugwiji wake katika mikakati
*CHANGAMOTO
Kuwepo kwa hofu la jina lake kutokurudi. Ingawa kwa hali ya chama ya sasa sio rahisi jambo hilo kutokea. Lazima tukubali, kutokurudi kwa jina la Dr. Nchimbi litaongeza mpasuko usio wa lazima. Ana kundi kubwa sana la vijana nyuma yake. Ana kundi kubwa la wabunge wateule wanaomuunga mkono.
Nimefanya utafiti binafsi, kwa wabunge wateule. Lazima tukiri kwamba Dr. Nchimbi wanamtafsiri kama mtu sahihi kwao katika kurithi kiti cha uspika na wameeleza kuridhishwa kwao kwa sifa zake, uzoefu wake, elimu yake, haiba yake, itikadi yake (ideology), personality yake na kubwa zaidi dhamira ya kuwatumikia watanzania wote kwa ujumla wao...
NB: Haya ni mawazo huru, hayana muingiliano na kundi lolote!...
Mchambuzi huru...
B.A Sociology. M.A Development Management. Phd (on progress)