Mods
Moderator naomba msiunganishe huu uzi🙏
Tumshukuru sana Mungu kwa zawadi ya uhai wa John Pombe Joseph Magufuli kwa nchi yetu. Ametutoa pagumu sana, ametuthubitishia yaliyoambiwa hayawezekani yanawezekana kwa vitendo
Ametuachia viongozi makini aliowapika kuwa wazalendo kama yeye mwenyewe na ameacha wananchi wengi walio maskini wakiwa na cha kujivunia kwa nchi yao
Ameiheshimisha Tanzania duniani kote kwa kuondoa uhuru wa bendera na kurudisha misingi ya uhuru halisi
Ametuachia serikali makini chini ya aliyekua msaidizi wake makini Rais Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote
Ametuachia jamhuri ya muungano wa Tanzania iliyo imara, bunge imara, mahakama imara na jeshi imara.
Hotuba ya Samia siku ya kuapishwa waziri mkuu, waziri wa fedha na waziri wa mambo ya nje. Hii ni baada ya Samia kuteiliwa na Magufuli kuwa makamu wa rais kwa mara ya pili. Samia alimhakikishia rais amenyooka na kumshukuru sana. Aliahidi kufanya kazi na rais apumzike akifanya mambo makubwa
Hotuba ya rais Magufuli siku ya kuapishwa waziri mkuu, waziri wa fedha na waziri wa mambo ya nje.
🙏🙏🙏
Pole tanzania yangu
Tumuombe Rais wetu Samia Suluhu Hassan aendeleze yale waliyoyaanza pamoja, na Mungu aendelee kumjaza hekma, ampe afya ya mwili, roho na akili katika kulitumikia taifa hili
Rest well our hero President John Pombe Magufuli 💔😭🙏