Huyu ndiye Christopher Kasanga Tumbo (RIP) - Mwanasiasa Machachari

Je, wamfahamu mzee Obed Mgongo?
 
Last edited by a moderator:
Swali dogo tu, chama kilikuwa na uhai wa miaka 2, uliwezaje kukipima na kusema kilikuwa na nguvu saaana, wakati hata hakikushiriki kwenye uchaguzi? Hivi kipimo cha nguvu ni watu kufika mkutanoni? Kumbuka katika nchi zetu, ambazo watu kazi zao ni za msimu kama wakulima, mikutano, ni moja pa mahala kwenda kutoa stress, na kuona vimwana kama ngomani.

I really doubt your analysis
 
Nilibahatika kukutana na huyu Mzee na alikuwa anapenda sana kueleza historia yake.

Alikuwa mwakilishi wa kwanza wa serikali ya tanu nchini Uingereza kama balozi.

Lakini alirudi Tanganyika 1962 akaanza kudai vyama vingi na kuanzisha NDP ndipo akapelekwa detention gereza la Uyui tabora huyu mzee alikuwa ni mfungwa wa kwanza kuwekwa katika Gereza la Uyui wakati huo bado jipya kabisa. Ina maana ni mfungwa namba moja.

Kuanzia hapo akaitupa kadi yake ya TANU akawa mpinzani bila chama na hakuwahi kurudi tena TANU wala kuwa mwanachama wa CCM.

Alisema kuna siku alikuwa analima shambani kwake akawa anasikiliza taarifa ya habari saa 7 mchana kwenye redio yake akasikia Nyerere anatangaza kuwa Tanzania tunaingia kwenye mfumo wa vyama vingi.

Akarudi nyumbani kwake haraka sana akamwambia mke wake ampangie vitu viwili vitatu kwenye begi lake safari ikawa moja kwa moja Dar es salaam na akakutana na akina Chief Fundikira na kuanzisha UMD.

Alikuwa kiongozi mpinzani wa kweli na kwenye historia ya wakati ule ni kiongozi wa upinzani pekee ambaye hakuwahi kuwa mwanachama wa CCM.

Wengine wote walishawahi kuwa wanachama wa CCM kwa namna moja au nyingine. Sababu kubwa ilikuwa huwezi kupata kazi bila kuwa mwanachama wa CCM kwa maana nyingine uanachama ulikuwa lazima
.
 
Hii thread ndiyo kwanza naiona.

Kasanga Tumbo, Abdallah Fundikira Na nduguye Mtemi Lugusha wa Sikonge walionja kichapo cha Nyerere.

Fundikira yeye alikimbilia Kenya ila Lugusha Na Kasanga Tumbo walipata kifungo cha nyumbani.

Walikuwa hawaruhusiwi kukutana Na watu wengi bila idhini ya Polisi.

Kuna Siku nilimuona Nyerere akiongea Na Lugusha Chang'ombe karibu Na kajiji cha Mlogoro Na bandage akamfungulia mlango wa Benz, wakaagana Na akaufunga mlango yeye Na siyo Walinzi au Dereva.

Baada ya Miaka kadhaa, Lugusha akaja kuwa Mbunge wa Sikonge kwa CCM. Ila alikuwa bomu Sana.

 
Nawafahamu Watoto wake kadhaa ukianzia Dr wa SUA, L, A, M.... Na wajukuu kadhaa. Ar... Yuko Mwanza mama sikosei.

Mzee Obed sikuwahi kubahatika kumuona au kukutana naye. Ila nilikuwa namfahamu Baba yake Prof. Kategile kutoka Ipole pia.

Je, wamfahamu mzee Obed Mgongo?
 

Hapo vipi? Umetuchanganya.
 
Ni kweli alikuwa dikteta. Nakumbuka hata kura ya maoni iliyopigwa kuhusu kuruhusu mfumo wa vyama vingi ulikataliwa lkn yeye akalazimisha. Bila yy tungekuwa na chama kimoja.
Mnyonge mnyongeni.......
Kwasababu aliaminisha watu vyama vingi ni vita. Dikteta sana yule dingi
 
 
[QUOTEzinawezaunist, post: 6010545, member: 87184"]Ukweli ni kwamba histori ya Tanganyika imechakachuliwa sana na Baba CCM yaani Tanu, yapo mengi kama haya. Na miaka 20 ijayo yanaweza yasipatikane tena. Maana wale wazee waliokuwepo wakati huo wanaishia. Namkumbuka Zuberi Mtemvu, Michael Sanga, Patric Kunambi, Kasela bantu, Lifa Chipaka, Kassim Hanga, Oscar Kambona, Aboud Jumbe, Mwamwindi the Great, NK. Ni vizuri kujua upande wa pili wa historia.[/QUOTE]
Pasi zinaweza kupigwa na karibia wachezaji wote uwanjani including goalkeeper lakini finally atakayefunga goli ndo atakayebeba sifa zote.
 
Kinachosikisha ni namna treatment ilifanyika kwa wapinzani wa wakati huo; walionekana ni maadui wakubwa - its just the same what is happening now.

Watu wenye mawazo badala katika uongozi wa taifa lao ni watu muhimu sana; kazi yao kubwa ni kuonyesha watawala the 2nd option to rulling the nation; sasa kuwakandamiza hawa ni kuliua taifa. Hili ndilo lilifanyka enzi hizo na ndilo linafanyika sasa. Killing opposition.
 
At least I have seen someone who is unveiling the truth, What happened to him?
Kafa maskini kazikwa kienyeji; kaburi la udongo; just thinking kama wanafamilia watanikubalia basi nitalijengea. Huyu ndie balozi wetu wa kwanza nchini ui geleza baada tu ya uhuru wa nchi yetu 1961.Sidhani kama watanzania wengi wanajua h5istiria hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…