Huyu ndiye Christopher Kasanga Tumbo (RIP) - Mwanasiasa Machachari

Hivi waliompa paundi 60,000 ili ampindue Mwl. walihitaji nini kama mrejesho endapo angefanikiwa
 
Hivi waliompa paundi 60,000 ili ampindue Mwl. walihitaji nini kama mrejesho endapo angefanikiwa
Huyo mwalimu wenu kisingizio Cha kuficha ukatili na tamaa ya madaraja huwa ni kupinduliwa tu!?..kambona,titi Mohammed,kasanga tumbo,kasela bantu,fundikira nk
 
Huyo mwalimu wenu kisingizio Cha kuficha ukatili na tamaa ya madaraja huwa ni kupinduliwa tu!?..kambona,titi Mohammed,kasanga tumbo,kasela bantu,fundikira nk
Mtoa mada anasema kuwa Christopher Kassanga Tumbo mwenyewe alisema kuwa alipewa kiasi hicho cha pesa ili ampindue mwalimu. Je waliompa pesa walitaka wafaidike nini kupitia pesa walizotoa ?
 
Mtoa mada anasema kuwa Christopher Kassanga Tumbo mwenyewe alisema kuwa alipewa kiasi hicho cha pesa ili ampindue mwalimu. Je waliompa pesa walitaka wafaidike nini kupitia pesa walizotoa ?
Porojo hizo
 
Dah!...taifa letu limepitia mengi sana.
 
H Hakuna Mjamaa anayehubiri Demokrasia, ukikutana naye wa hivyo basi tambua kuwa huyo ni Mamluki, ni Kibaraka na mshenga wa wakoloni.
 
Umenikumbusha kitu kwenye wimbo huo "TANU jabela mitwe" wengine wakidai TANU imewahi kufanya mauaji ya waasi wake kwa kuwakata vichwa, kuna ukweli wowote? Wimbo huo ulimaanisha nini?
 
Yeah, lakini historia ya nchi imemuweka pembeni kabisa same as Kambona.
Fuso,
Namjua Kassanga Tumbo kwani yeye na babu yangu Salum Abdallah wameacha historia ya pekee katika historia ya vyama vya wafanyakazi Tanganyika.

Babu yangu Salum Abdallah mwaka wa 1947 aliongoza ''General Strike,'' (mgomo) Tanganyika nzima dhidi ya Waingereza.

Akafanya hivyo tena mwaka wa 1949 na mwaka wa 1960 wakati huo akiwa Chairman wa Tanganyika Railway African Union (TRAU) Katibu akiwa Christopher Kassanga Tumbo na wote ndiyo waasisi wa chama hicho cha wafanyakazi wa reli 1955.

Mwaka wa 1960 TRAU chini ya uongozi wao waliitisha mgomo uliovunja rekodi kwani ulidumu kwa siku 82.

Mgomo wa ulioitishwa na Makhan Singh, Kenya ulidumu kwa siku 62.
Angalia picha hapo chini:

Kulia ni Christopher Kassanga Tumbo na anaefuatia ni babu yangu Salum Abdallah
siku hiyo wanachama wa TRAU walimvisha huo mgogolole kama alama ya jemedari
anaongoza majeshi katika vita dhidi ya ukoloni hii ni miaka ya katikati 1950s.

Harakati hizi TRAU walifanya bega kwa bega na TANU na babu yangu ni katika waasisi wa TANU Tabora na alikuwa mjumbe katika kamati ya siri ya kuasisi TANU.

Mwaka wa 1964 babu yangu na Kassanga Tumo pamoja na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi kama Victor Mkello waliwekwa kizuizini baada ya maasi ya wanajeshi.

 
H
Hakuna Mjamaa anayehubiri Demokrasia, ukikutana naye wa hivyo basi tambua kuwa huyo ni Mamluki, ni Kibaraka na mshenga wa wakoloni.
Uko sahihi kwa maana halisi ya mjamaa ambayo tafsiri yake hasa ni mkomunisti. Ukomunisti hauendani na demokrasia. Ni socialists ndio wanatambua na kuzingatia demokrasia. Bila shaka, Tumbo alikuwa socialist. (huwa inachanganywa na ujamaa).

Nyerere aligoma hata kutoa tafsiri ya “ujamaa” kwa marafiki zake wa Mashariki na Magharibi walipotaka kujua endapo ujamaa ni socialism au communism. Yeye alidai ujamaa ni mfumo wa kipekee wa maisha wa kiafrika; hauna tafsiri nyingine!

Kwa jinsi ilivyojionyesha kwamba anafuata zaidi modeli ya China (PRC), hakukuwa na shaka kwamba ujamaa ni ukomunisti wenye sifa kuu zifuatazo: Mfumo wa chama kimoja cha siasa kilichoshikamanishwa kikamilifu na dola. Chama kushika hatamu kwenye mihimili na taasisi zote za umma ikiwa ni pamoja na za kiraia/kibinafsi. Uchumi kudhibitiwa na dola (command economy). Kutaifisha mali za mabepari (watu binafsi) bila fidia, kudhibiti/kuondoa sekta binafsi, kukusanya wananchi katika makazi na shughuli za uchumi za pamoja (vijiji vya ujamaa/collectivization), n.k.
 
Chumvi za waleta story..pound maana yake alipewa na waingereza, waingereza wampindue Nyerere ili iweje wakati alikua mtu wao!!?
Na ukizingatia baada ya kunusurika kupinduli na jeshi la nchi na kulivunja,aliikabidhi nchi chini ya jeshi la Uingereza kwa karibu mwaka mzima wakati ikiundwa JWTZ.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…