Hapana Mkuu,
Kuna Braza wangu alikuaga akirekodi hizi nyimbo kwenye Audio cassette pale zinapopigwa redioni kisha anazisikiliza enzi hizo,
Sasa sababu alikua mkubwa basi ilibidi nami nizisikilize tu maana redio ndio hiyo hiyo moja, akiweka yeye hakuna mtu kutoa.
Alinifundisha hata ku-scratch kwa kutumia normal radio cassette,
Yaani kile kidude cha "Pause" ndio kilikua kinasugua inafanania kama na CD ilikua scratched,
Nikajikuta napenda tu nyimbo za kina aina hii kina Saigon, Afro reign, Underground Souls, W10N, 2proud, hadi zile Saleh Jabir aki rap kwenye beats za nje nilikuaga nazo