Huyu ndiye Kiongozi

Huyu ndiye Kiongozi

Hamia kenya bac kama vip, ukakutane na mngik wabongo bwana
Issue sio kuhamia Kenya..
The matter here ni kwamba Tanzania inaongozwa ovyo..
Hilo wala halina mjadala..
Pogba amesambaratisha kila kilichokuwa walau kimesimama sasa kimelala..
Demokrasia, Uchumi, hali za wafanyakazi, investors wote hoi..
Kingunge alisema huyu ni nyapara wa Barabara Hakupaswa kuongoza Nchi.
 
Hamia kenya bac kama vip, ukakutane na mngik wabongo bwana

Mwenye akili timamu angeisikiliza halafu kama ameongea ujinga ndipo ungecomment.Wabunge wetu hawana tofauti na hao anaowapasha hapo.Lakini yawezekana na wewe ni Mbunge hivyo unaona heri wananchi waliokupigia kura wakose ila wewe uendelee kuongezewa,shame on you
 
Huyu jamaa amekulia ikulu, amemuona babake akiongoza, amekulia maisha ya kifahari, amekuzwa na amemuona na kujifunza uongozi pia kwa Moi ana exposure ya kutosha kwenye mambo ya uongozi unategemea aongoze kama mtu aliekulia kijijini ambaye muda wote anataka aonekane ni Raisi wakati tayari ni raisi.
Umenena vyema. Hamna mtu mpenda sifa kama mtu aliyeokota hela ata mwambia kila mtu ana hela wakati hela anazo. Lakini ukizaliwa kwenye hela wala huna haja ya kusema unazo kwani zinaonekana zenyewe
 
Niliwahi kusema awali kuwa huyu wa kwetu anazidi kuharibika kwa sababu yapo mavuvuzela yamekaa kumsifia hata anapoharibu. Na kwa vile hajitambui yaani ushamba umetamalaki, basi anavimba kichwa kwa sifa hizo na kuona anafanya sawa. Lakini haya ya madeni na kamata kamata ya mali ndio akili inaweza kumrudia
 
Nimezunguka usukumani kwa miaka mingi.

Nakumbuka matukio mengi ya wachimba dhahabu, wenyewe wanawaita wachoji. Wale huweza kutafuta dhahabu hata kwa miakan10 wakikilishwa maharage, wakivuta bangi, na bila ya kupewa hata elfu 1. Siku ikatokea wakapata hata milioni 20 tu, wakagawiwa japo milioni 2 kila mmoja, utadhani Dunia nzima wao ndiyo walio na pesa kuliko mtu yeyote.

Wengine watakodi wabodigadi wa kuwalinda. Wengine wataingia baa na kuwapa bia wote waliomo humo. Wengine wataenda 9kuwatafuta malaya na kuwaamuru wavue nguo zote, wanawachungulia tu, na kisha kuwalipa pesa.

Ukikulia mazingira ya namna hii, ndiyo ule msemo wa maskini akipata matako hulia mbwata utaelewa maana yake.

Viongozi wakuu wapo wengi lakini wa kwetu anadhani amekuwa kiongozi mkuu pekee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenena vyema. Hamna mtu mpenda sifa kama mtu aliyeokota hela ata mwambia kila mtu ana hela wakati hela anazo. Lakini ukizaliwa kwenye hela wala huna haja ya kusema unazo kwani zinaonekana zenyewe
Na huu ndio uhalisia, malimbukeni wengi hutoka katika familia duni...mara chache sana ukute mtu aliekulia kwenye pesa ni limbukeni!
 
Back
Top Bottom