Huyu ndiye Muigizaji Brian Deacon, aliyeigiza kama Yesu na anachokifanya kwa sasa katika Maisha

Huyu ndiye Muigizaji Brian Deacon, aliyeigiza kama Yesu na anachokifanya kwa sasa katika Maisha

MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU YA #YESU AMBAYE BAADHI YA WATU HUDHANI KWAMBA NI YESU,

"MWENYEWE AMESHANGAZWA NA BAADHI YA WAUMINI KUWEKA PICHA ZAKE KWENYE MAKANISA, MAJUMBA YAO NA KUVAA ROSARI ZENYE SANAMU YAKE WAKIAMINI YEYE NI YESU KITU AMBACHO SI KWELI

Jamaa ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la ''JESUS'' mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel,

kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo YESU au ISSA BIN MARYAM kama wanavyomuita Waislamu .

hata yeye amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu. KARIBU.

BRIAN DEACON NDANI YA FILAMU YA ''JESUS''

Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,

ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.

Aliigiza filamu ya Yesu baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.

#Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.

Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.

Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho

Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo

Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga,

,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.

ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.

BRIAN ANAWAAMBIA WATU WOTE DUNIANI KUWA YEYE SI YESU BALI YEYE NI MUIGIZAJI TU, WALA HAFANANI NA YESU KWANI ENZI ZA YESU HAPAKUWEPO NA TEKNOLOGIA YA CAMERA HIVYO HATA SURA HALISI YA YESU HAIJULIKANI ZAIDI YA WATU KUOTEA NA KUBUNI JINSI YESU ALIVYOFANANA KAMA DIRECTOR WAKE ALIVYOBUNI KWA DEACON

BRIAN PIA AMESHANGAZWA NA BAADHI YA WAUMINI KUWEKA PICHA ZAKE KWENYE MAJUMBA YAO NA KUVAA ROSARI ZENYE PICHA YAKE WAKIAMINI YEYE NI YESU KITU AMBACHO NI MAKOSA

AMESEMA ILI KUTHIBITISHA KUWA YEYE NI MUIGIZAJI TU AMEZITAJA filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985, The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.

Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa filamu ya ''JESUS''iliyoigizwa mwaka 1979 huko nchini Israel.[emoji1426][emoji1426][emoji1426][emoji1426][emoji1426]View attachment 919657View attachment 919658View attachment 919659View attachment 919660View attachment 919661View attachment 919662View attachment 919663View attachment 919664
Naona picha ya mwisho yesu kavaa jinsi anapunga upepo kibarazani
 
Huu Uzi alishauleta Da'Vinci humu tena alielezea vizuri huyo Deacon anafanana na nani
 
Mambo mengine yanaeleweka tu hata kwa common sense sasa ñashangaa watu wakiwa hawataki kukubali kuwa lile movie ni igizo kama maigizo mengine

Nimeshtuka kidogo kuona hiyo kampuni iliyotengeneza muvi hiyo kwakuwa kuna stori ndefu kuhusu jina lake (jina la hiyo kampuni) na chimbuko la hao wanaomwabudu huyo jamaa

Mwandishi naomba uje umchambue pia na yule aliyeigiza kama maria-mama wa yesu bila kusahau na yule mtoto
 
Uyu bwege kachezea sana akil za waafrika
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
MNAPANIKI BURE!

Mi sioni sababu inayowafanya mpaniki.... maigizo yapo hakuna anaeibisha.

HOJA HAPA , JE ALICHOIGIZA AMEPOTOSHA AU HAJAPOTOSHA KULINGANA NA KITABU CHA LUKA??

Sasa kama hakupotosha ,,povu la nini?..

Hata Mimi sikatai wakati mdogo katika maisha yangu niliamini kabisa huyo ndo YESU mwenyewe nikijumlisha na maandiko matakatifu toka katika kitabu cha luka,,, Binafsi ilinisaidia kuwa karibu na Mungu.............ile hofu ya Mungu niliyokuwa nayo mapema ilinisaidia kutoshiriki matendo maovu au dhambi hata kama nikifanya ilikuwepo hali kujutia...na unyenyekevu huo Leo naona matunda yake hata baada ya kugundua sio YESU.

Wengi mtakuwa mnamjua ndege tai anapomfundisha kinda wake kuruka. Ni kama anamtesa lakini anakuwa nia njema huo ni mfano mzuri wa maisha ya Mungu na Mwanadamu.

WAKATI mwingine ni njia anazotumia MUNGU katika harakati za kumrudisha mwanadam kwake.....MUNGU anakuanzia mbali anapotaka kukusaidia.......imani yako inapokomaa hapo anakuacha ujitegemee na hapo ndo unagundua Huyo kwenye filamu sio YESU lakini pia unagundua MAKUSUDI ya Mungu kwako.

Sasa hatua ya mwanzo kabisa tunapaswa kuamini kwa sababu kila neno lenye pumzi ya MUNGU lafaa kwa mafundisho ....Hivyo kadri tunavyokua ndivyo MUNGU anavyotuimarisha katika imani zetu.

Sasa kwenye hiyo filamu yamehubiriwa mambo mengi yanayotuasa,,

Umetajwa UPENDO, UCHOYO, UZINZI, ULAFI , CHUKI , TAMAA n.k

lakini bado miujiza mingi imefanyika kuthibitisha nguvu za Mungu.......yote hayo hatujifunzi sisi tunakomaa kwamba aliyeigiza sio Yesu sidhani kama inasaidia.

Wale wahenga zamani mtakumbuka tulikuwa tunaonyeshwa sinema za maigizo kuhusu ugonjwa wa ukimwi...unashuhudia mwanzo mwisho mpaka Mtu anavyokonda na kufa.
Yote yalikuwa ni maigizo lakini yanaleta hisia mpaka unabadili mwenendo ,, ..kama una ile hofu inakusaidia kukuokoa hata kama ni igizo.

Kwaio mi nafikiri tunapaswa kuamini kwanza yaliyomo kwenye hiyo filamu.

Hoja ya aliyeigiza sio Yesu ni nyepesi mno na haisaidii.
 
Umetoa Maelezo marefu lakini yenye kufikirisha lakini hoja apa niupotoshwaji mkubwa wa wahubiri asa Wakristo kumtumaini nawakati mwingine kuchukulia picha zake kuziabudu nk. Kwanini hatukuambiwa kuwa yule ni muigizaji aliyesoma kitabu cha Luka? Kwanini tulifichwa ukweli huu asa Mapadri/Wachungaji!
Naumia sana kwakudanganywa.Wakatoriki ni mabingwa wa kukwepa kuhubiri ndo maana waliamua kutimkia kwenye sinema.
Wale wote waliobariki filamu hii nakushindwa kuitolea Maelezo wote niwanafiki na dawa ya wanafiki mnaijua.
Nataka Mapadri/Wachungaji nje mtuombe radhi kwakutulisha matango pori.
Uyu muhuni aliyecheza hii filamu alikaa kimia uku akijua fika kuwa yeye sio YESU.
Namwamini sana Mungu ataendelea kujitukuza na kujifunua ili watu wote wamjue yeye.

Ndugu hoja zako niza kidini sio za Kiroho lazima tuseme ukweli kwamba hakuna mwanadamu anayetambua sura ya YESU zaidi wale waiokuwepo maana ata wachoraji wawakati ule naona hawakufunuliwa ikizingatiwa camera hazikuwepo.
Uyu nimsanii kama kina Wema, Kanumba nk. Kwani uyu kahaba (Wema sepetu) akiigizaa kama mlokole nikweli atakua kaokoka?

Acheni kutetea ujinga nakusudia kufungua Shauri Mahakamani kupinga mikanda hii kuoneshwa mpaka watakapoamua kuwaeleza watazamaji kuwa yule sio YESU bali ni comedian.
 
Uyu bwege kachezea sana akil za waafrika
Kweli kabisa. Kuna mfia dini mmoja aliweka kwenye mitandao eti kanisa limeungua lote ikabaki picha ya Yesu. Kumbe ni huyu jamaa ambaye ukimchunguza unawezamkuta hata ni shoga
 
Kwa hamjui kuwa hiyo ni filamu tu.
Kwamba wahusika wote ni wa kuigiza.
Kwamba hakuna aliyempiga picha Yesu halisi.
Kwamba hakuna Mkristo anaye abudu Sanamu au picha.
 
Sasa nataka kufafanua yule kahaba anayefananishwa na Bikira Mariam aliyemzaa yesu wengi wetu mnatembea naye kwenye magari ndo maana mnapata ajari, wengine mmemjengea vihekalu vidogo nyumbani kwenu ndomaana migogoro haiishi,wengine mmnamwomba kanisani ndomaana familia zenu zimeparaganyika. Subirini naandaa dawa yenu. Hatuwezi kuwaacha mkaarifu na kumfananisha Mungu na miungu.
 
Kwa hamjui kuwa hiyo ni filamu tu.
Kwamba wahusika wote ni wa kuigiza.
Kwamba hakuna aliyempiga picha Yesu halisi.
Kwamba hakuna Mkristo anaye abudu Sanamu au picha.
Hapo ndipo utajua tofauti ya kusoma na kuelimika.
Kuna watu huwa wanajisifu sana kuwa wamesoma na kuwadharau wengine lakini wanaabudu picha
 
Kwa hamjui kuwa hiyo ni filamu tu.
Kwamba wahusika wote ni wa kuigiza.
Kwamba hakuna aliyempiga picha Yesu halisi.
Kwamba hakuna Mkristo anaye abudu Sanamu au picha.
Kama hakuna Wakristo wanaohabudu picha mbona ziko makanisani? Mbona wanazo majumbani kwenye magari nk.
Wakatoriki wanaongoza kwa kuhabudu sanamu.
 
Umetoa Maelezo marefu lakini yenye kufikirisha lakini hoja apa niupotoshwaji mkubwa wa wahubiri asa Wakristo kumtumaini nawakati mwingine kuchukulia picha zake kuziabudu nk. Kwanini hatukuambiwa kuwa yule ni muigizaji aliyesoma kitabu cha Luka? Kwanini tulifichwa ukweli huu asa Mapadri/Wachungaji!
Naumia sana kwakudanganywa.Wakatoriki ni mabingwa wa kukwepa kuhubiri ndo maana waliamua kutimkia kwenye sinema.
Wale wote waliobariki filamu hii nakushindwa kuitolea Maelezo wote niwanafiki na dawa ya wanafiki mnaijua.
Nataka Mapadri/Wachungaji nje mtuombe radhi kwakutulisha matango pori.
Uyu muhuni aliyecheza hii filamu alikaa kimia uku akijua fika kuwa yeye sio YESU.
Namwamini sana Mungu ataendelea kujitukuza na kujifunua ili watu wote wamjue yeye.

Ndugu hoja zako niza kidini sio za Kiroho lazima tuseme ukweli kwamba hakuna mwanadamu anayetambua sura ya YESU zaidi wale waiokuwepo maana ata wachoraji wawakati ule naona hawakufunuliwa ikizingatiwa camera hazikuwepo.
Uyu nimsanii kama kina Wema, Kanumba nk. Kwani uyu kahaba (Wema sepetu) akiigizaa kama mlokole nikweli atakua kaokoka?

Acheni kutetea ujinga nakusudia kufungua Shauri Mahakamani kupinga mikanda hii kuoneshwa mpaka watakapoamua kuwaeleza watazamaji kuwa yule sio YESU bali ni comedian.
Mkuu sidhani kama wachungaji au mapadri wanapohubuiri na kumtaja Yesu wanamaanisha huyu jamaa aliyeigiza...

Yanibhauna sababu ya kutaharuki
 
Tujikite kwenye mada jamani.........Yesu halisi alikuwepo na huyu ni muigizaji tu.
 
Kama hakuna Wakristo wanaohabudu picha mbona ziko makanisani? Mbona wanazo majumbani kwenye magari nk.
Wakatoriki wanaongoza kwa kuhabudu sanamu.
Anaye abudu sanamu sio Mkristo,
Kuna makanisa mengi ambayo siyo ya Kikristo.
Hujawahi liona
The Satanic Church,
The Mormon Church
The Rastafalian Church.
Sasa hebu wewe niambie hapa, hilo kanisa ulilo ona wanaabudu sanamu linaitwaje.
Soma kwenye bango lake utaona walipoandika.
Kanisa la Kristo haliabudu sanamu.
Wakristo hawaabudu sanamu hata siku moja.
Usichanganye kati ya kanisa la Kristo na Makanisa mengine.

Ushanielewa jamaa yangu.
 
Back
Top Bottom