Karugendo alikiuka kiapo cha useja kwa kuwa na mahusiano na mwanamke nje akijua fika kufanya hivyo lilikuwa ni kosa, usifanye Askofu Niwemugizi aonekane mbaya kwa kumchukulia hatua mtu ambaye alikiuka kiapo hiki muhimu.
Mtu akikosea lazima aadhibiwe kwa kosa lake, ni adhabu ya aina gani atakayopewa huo ni uamuzi wa kiongozi wake, na zaidi kwa nafasi aliyokuwa nayo alionesha udhaifu dhidi ya imani yake, na pia zaidi, kwa wale waliokuwa waumini wake, huyu kama angesamehewa angeweza kuweka "precedence" mbaya kwa Kanisa Katoliki.
Kwangu nasimama na uamuzi wa Askofu Niwemugizi kumvua cheo cha upadri, lakini pia, nilikuwa napenda nipate wasaa wa kukutana nae nimuulize kwanini alikuwa bado anatumia jina la "Padri" kama nilivyokuwa nikisoma makala zake kwenye magazeti mbalimbali licha ya kuwa alishavuliwa hicho cheo na kanisa?